Content-Length: 95563 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/Mto_Ohio

Ohio (mto) - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Ohio (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Ohio)
Mto Ohio
Ramani ya beseni ya mto Ohio
Mto Ohio kwa macho ya ndege

Mto Ohio ni tawimto muhimu wa mto Mississippi katika mashariki ya Marekani.

Urefu wake ni kilomita 1,579 kuanzia chanzo chake kwenye maungano ya mto Allegheny na mto Monongahela karibu na mji wa Pittsburgh hadi mdomo kwenye mto Mississippi. Njia ya mto ni mpaka kati ya majimbo sita ya Marekani na beseni yake inajumlihsa eneo la majimbo 14. Tawimto kubwa ya kuingia ni mto Tenessee.

Katika historia ya Marekani ilikuwa njia muhimu ya mawasiliano kabla ya kujengwa kwa barabara na reli. Wakati wa karne ya 19 Ohio ilikuwa mpaka kati ya maeneo yaliyoruhusu utumwa na majimbo yaliyokataa utumwa.

Mto huu umepakana na majimbo ya Ohio, Kentucky, Illinois, Indiana, West Virginia na Pennsylvania. Miji muhimu kando la mto ni Louisville, Kentucky, Paducah, Kentucky, Cincinnati, Ohio na Pittsburgh, Pennsylvania.


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ohio (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/Mto_Ohio

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy