Content-Length: 102474 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/Akina_Grimm

Akina Grimm - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Akina Grimm

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wilhelm Grimm (kushoto) na Jakob Grimm. Taswira ya mwaka 1885 na Elisabeth Maria Anna Jerichau-Baumann

Akina Grimm (Jer.: Die Brüder Grimm, pia Gebrüder Grimm; ing. "Brothers Grimm") ni namna ya kutaja kwa pamoja wataalamu na ndugu kaka Jakob Grimm na mdogo wake Wilhelm Grimm. Wamekuwa mashuhuri hasa kwa kukusanya hekaya, ngano na hadithi nyingine za Ujerumani na kuzilinganisha na masimulizi kutoka nchi nyingine. Wanahesabiwa kati ya waanzilishaji wa fani ya isimu au sayansi ya lugha.

Katika Ujerumani na kwa wataalamu wa lugha za Kigermanik wanajulikana pia kwa kuanzisha kazi ya kamusi kubwa ya lugha ya Kijerumani inayoendelea kuhaririwa hadi leo na kufikia vitabu 32.

Mkusanyiko wao wa ngano unasomwa hadi leo hii. Kwa kazi hii walitembelea vijiji vingi na kuandika hekaya na ngano jinsi zilivyosimuliwa na wazee (Grimms Märchen).

Kati ya ngano walizokusanya ni Mweupe Theluji ("Schneewittchen"), "Sinderella" "(Aschenputtel)", "Hansel na Gretel" ("Hänsel und Gretel") na takriban 200 mengine.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Kigezo:Wikiquote-en

Wikimedia Commons ina media kuhusu:








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/Akina_Grimm

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy