Darubini
Darubini (kutoka Kiajemi: دوربين, dorbin) ni kifaa cha kutazamia vitu ambavyo viko mbali. Kutegemeana na kusudi lake kuna aina mbalimbali:
- Darubini ndogo za mkononi ni vyombo vinavyotumiwa na wapenda mazingira asilia, wawindaji, polisi na jeshi.
- Darubini kubwa hupatikana mara nyingi katika paoneaanga (vituo vya elimuanga); kuna hasa aina mbili:
- darubininuru (optical telescope) kubwa hutumiwa na wataalamu wa anga kwa kutazama magimba ya angani kama jua, mwezi, nyota, sayari au nyotamkia. Darubini hizo huwa ama
- darubinilenzi (refracting telescope)
- darubiniakisi (reflecting telescope).
- darubininuru (optical telescope) kubwa hutumiwa na wataalamu wa anga kwa kutazama magimba ya angani kama jua, mwezi, nyota, sayari au nyotamkia. Darubini hizo huwa ama
- darubiniredio hutumiwa pia na wanaastronomia zikikusanya mawimbi ya sumakuumeme zinazofaa kutupa picha za violwa vya mbali sana isizoonekana kwa njia ya nuru ya kawaida. Zinafaa pia kuonyesha tabia za violwa vya angani vya karibu zaidi zisizotambulika kwa njia ya nuru.
Historia ya darubini
[hariri | hariri chanzo]Darubini ya kwanza inayojulikana ilitengenezwa mwaka 1608 na Mholanzi Hans Lipperhey aliyekuwa fundi miwani akaunganisha lenzi mbili katika bomba.
Mfano wake ulichukuliwa na kuboreshwa na mwanaastronomia Mwitalia Galileo Galilei aliyeanza kuitumia mwaka 1610 kwa kuangalia nyota. Aligundua mara moja miezi ya sayari Mshtarii.
Muundo tofauti uligunduliwa na padre Nicolaus Zucchius mwaka 1616 uliotumia kiakisi parabola kwa kukusanya mishale ya nuru.
Katika karne zilizofuata vyombo hivyo viliendelea kuboreshwa.
Mtambo mpya ulipatikana katika karne ya 20 kwa kutumia mnururisho wa sumakuumeme kutoka nyota iliyoendelezwa kuwa darubiniredio.
Elimu ya ulimwengu wetu ilipanuka sana tangu kupelekwa kwa darubini za angani kwenye anga-nje zinazopokea nuru na mawimbi ya sumakuumeme bila athari ya angahewa ya Dunia.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- http://www.eso.org/projects/owl/
- The Resolution of a Telescope Ilihifadhiwa 5 Aprili 2004 kwenye Wayback Machine.
- http://www.eurocosm.com/Application/images/telescopes/525-telescope-lg.jpg
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Hadubini (au darubini ya vidudu)