Content-Length: 86958 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/El_Aai%C3%BAn

El Aaiún - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

El Aaiún

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa El Aaiún, Moroko
Mji wa El Aaiún, Moroko

El Aaiún (pia Laâyoune, العيون = al-ʿUyūn) ni mji mkubwa wa Sahara ya Magharibi kwenye bonde la Saguia el Hamra karibu na mwambao wa Atlantiki.

Hadi mwaka 1976 ilikuwa makao makuu ya utawala wa kikoloni wa Hispania. Baadaye mji ulivamiwa na Moroko pamoja na sehemu kubwa ya Sahara ya Magharibi.

Idadi ya wakazi ni takriban 200,000 wengi wao ni walowezi kutoka Moroko walioingia tangu mwisho wa 1976.

Katika muundo wa utawala wa Moroko El Aaiun ni makao makuu ya wilaya ya Laâyoune-Boujdour-Sakia El Hamra. Machoni pa wafuasi wa Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu mji unstahili kuwa mji mkuu wa nchi hii ikipata uhuru wake.

"El Aaiún" ni umbo la maandishi ya Kihispania kwa ajili ya jina la Kiarabu kinchomaanisha "chemchemi". Maandishi katika kawaida ya Kifaransa ni "Laâyoune" yanayotumika zaidi upande wa Moroko.









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/El_Aai%C3%BAn

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy