Hifumi Abe
Hifumi Abe (amezaliwa 9 Agosti 1997) ni mwanajudo[1] wa Japani.
Hifumi Abe alipata umaarufu baada ya kuwa bingwa wa Michezo ya Olimpiki ya Vijana mnamo mwaka 2014. Alishinda Tokyo Grand Slam baadaye akiwa na umri wa miaka 17 tu, alishinda pia ubingwa wa Dunia wakati huo. Alikuwa mshindi wa medali ya fedha katika Mashindano ya Vijana ya Dunia huko Fort Lauderdale. Abe ndiye bingwa wa sasa wa taifa katika Mashindano yote ya Judo nchini Japan lakini pia, alishinda medali ya dhahabu katika shindano la kilo 66 katika Olimpiki ya mwaka 2020 iliyofanyika Tokyo, Japani.[2][3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Hifumi ABE / IJF.org". www.ijf.org. Iliwekwa mnamo 2021-12-03.
- ↑ IOC. "Tokyo 2020 Men -66 kg Results - Olympic judo". Olympics.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-12-03.
- ↑ "Hifumi ABE". Olympics.com. Iliwekwa mnamo 2021-12-03.