Content-Length: 78624 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/Malighafi

Malighafi - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Malighafi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malighafi zikiwa tayari kupakiwa katika meli.

Malighafi (kutoka maneno ya Kiarabu "mali" + "ghafi"; kwa Kiingereza "raw material") ni kitu chochote ambacho kinatumika katika utengenezaji wa bidhaa.

Mfano wa bidhaa na malighafi zake ni ngozi ambayo hutumika kutengenezea viatu, mkanda, begi na kadhalika.

Mfano mwingine ni matunda ambayo hutumika kutengeneza vinywaji mbalimbali.

Vilevile mbale hutumika kupata metali safi; mfano kuyeyusha mbale wa chuma kupata chuma na feleji.

Bara la Afrika lina 30% za akiba zote za malighafi zisizo nishati duniani, lakini utajiri huo umeathiri vibaya wakazi wake. Tatizo hilo linaitwa kwa Kiingereza "Dutch disease" au "resource curse" (yaani laana ya kuwa na vyanzo vya maliasili).

Laana hii imekuwa wazi hasa katika eneo ambalo kwa sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambalo lina malighafi nyingi ajabu, ambazo zimesababisha ukoloni, dhuluma, vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa wingi n.k. hadi leo (ukoloni mamboleo).

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Malighafi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/Malighafi

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy