Mto Magdalena
Mto Magdalena ni mto muhimu zaidi katika magharibi ya Kolombia. Una urefu wa km 1,538. Njia yake inafuata mwelekeo kutoka kusini kwenda kaskazini. Karibu asilimia 80 ya wakazi wa Kolombia huishi kwenye kingo za mto huu au mmoja wa matawimto yake, pamoja na Barranquilla ambayo ni jiji kubwa la Kolombia.
Mto huo unaweza kutumumiwa na meli hadi mji wa Honda uliopo mnamo km 1,000 kutoka mdomo wake baharini.
Pale Honda kuna maporomoko ya maji yasiyopitika. Baada ya kizuizi hiki mto unaweza kutumiwa tena na meli za mizigo kwa km 240 za ziada.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Magdalena kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |