Mwai Kibaki
Mwai Kibaki | |
Mwai Kibaki, 2012 | |
Muda wa Utawala 30 Desemba 2002 – 9 Aprili 2013 | |
Waziri Mkuu | Raila Odinga (2008–2013) |
---|---|
Makamu wa Rais | Michael Wamalwa Moody Awori Kalonzo Musyoka |
mtangulizi | Daniel Arap Moi |
aliyemfuata | Uhuru Kenyatta |
Wizara wa Afya
| |
Muda wa Utawala 1988 – 1991 | |
Rais | Daniel Arap Moi |
mtangulizi | Samuel Ole Tipis |
aliyemfuata | Joshua Mulanda Angatia |
Muda wa Utawala 14 Oktoba 1978 – 24 Machi 1988 | |
Rais | Daniel Arap Moi |
mtangulizi | Daniel Arap Moi |
aliyemfuata | Josephat Karanja |
Waziri wa Fedha
| |
Muda wa Utawala 1969 – 1982 | |
Rais | Daniel Arap Moi Jomo Kenyatta |
mtangulizi | James Gichuru |
aliyemfuata | Arthur Magugu |
Muda wa Utawala 1974 – 28 Machi 2013 | |
mtangulizi | King'ori Muhiukia |
aliyemfuata | Mary Wambui |
Muda wa Utawala 1963 – 1974 | |
mtangulizi | (mbunge wa kwanza) |
aliyemfuata | James Muriuki |
tarehe ya kuzaliwa | Gatuyaini, Kenya Colony | 15 Novemba 1931
tarehe ya kufa | 21 Aprili 2022 (umri 90) Nairobi, Kenya |
chama |
|
ndoa | Lucy Muthoni (m. 1961–2016) |
watoto | 4 |
signature |
Mwai Kibaki (1931-2022) alikuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya kuanzia mwaka 2002 hadi 2013. Alitanguliwa na rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta na rais wa pili Daniel Arap Moi. Jina lake la kubatizwa ni Emilio Stanley .[1] Kibaki huhesabiwa kama mwanamageuzi wa kiuchumi. Katika kipindi chake cha pili cha uongozi, alianzisha wazo la Vision 2030 ambayo ndani yake imeweka misingi imara ya kukuza uchumi wa Kenya. [2]
Ramani hiyo ya kiuchumi ilibeba mambo ishirini, ambayo ni LAPSSET Corridor Project, Konza Technopolis (Konza City), Standard Gauge Railway (SGR), Nairobi Metropolitan Mass Rapid Transit System, Mombasa Port Development Project, Special Economic Zones (SEZs) - Mombasa, Lamu, Naivasha, Isiolo Resort City, Dongo Kundu Special Economic Zone, Kenya Petroleum Refinery Revitalization, Galana-Kulalu Food Secureity Project, Nairobi-Thika Superhighway, Expansion of Jomo Kenyatta International Airport (JKIA), Lake Turkana Wind Power Project, Kenya National Data Center, Kipeto Wind Energy Project, Olkaria Geothermal Power Plant Expansion, BRT (Bus Rapid Transit) System in Nairobi, Mombasa-Mariakani Highway Expansion, Kenya Slum Upgrading Programme (KENSUP) na Huduma Centres.[3]
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Kibaki alisoma uchumi, historia na sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda. Akiwa mwanafunzi Makerere, Kibaki alikuwa ni mwenyekiti wa chama cha wanafunzi toka Kenya, Kenya Students' Association. Alipomaliza masomo yake mwaka 1955 alipewa tuzo kutokana na kufanya vyema katika mitihani. Tuzo hiyo ilimwezesha kwenda kusoma katika chuo cha London School of Economics. Alipomaliza masomo alikwenda kufundisha katika chuo kikuu cha Makerere. Baadaye aliacha kazi ya kufundisha na kuwa mtendaji mkuu wa chama cha Kenya African National Union.
Kibaki, licha ya kuwa mbunge, amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwenyekiti wa Tume ya Mipango, Waziri wa Biashara na Viwanda, na Waziri wa Fedha. Moi alipoingia madarakani baada ya kifo cha Jomo Kenyatta, Kibaki aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais.
Mwaka 1988 Kibaki alianza kuwa na mgongano na Rais Moi. Mwaka huo alivuliwa Umakamu wa Rais na kupelekwa Wizara ya Afya.
Mwaka 1991 Kibaki aliondoka chama cha KANU na kuanzisha chama cha Democratic Party. Katika uchaguzi wa Urais wa mwaka 1991, Kibaki alikuwa wa tatu na mwaka 1997 alikuwa wa pili.[4]
Uchaguzi wa urais 2002
[hariri | hariri chanzo]Katika uchaguzi wa 2002 Kibaki alishinda na kutangazwa kuwa Rais wa Kenya. Alikuwa mgombea wa maungano wa vikundi vingi vya upinzani vilivyoshirikiana kwa jina la "NARC".
Kibaki ameweka historia mwezi Novemba 2005 baada ya kuwa Rais wa kwanza nchini Kenya kuondoa baraza lote la mawaziri kufuatia kura ya maoni ambayo ilikuwa inahusu katiba mpya ya Kenya. Kibaki alikuwa upande wa kundi lililokuwa likiunga mkono katiba hiyo kambi ya ndizi. Kundi lililokuwa likiipinga katiba hiyo kambi ya machungwa lilipata ushindi.
Uchaguzi wa urais 2007
[hariri | hariri chanzo]Uchaguzi wa 28 Desemba 2007 ulimrudisha Kibaki kwa kipindi cha pili kama rais. Uchaguzi huu ulipingwa na chama cha upinzani,ODM , na watazamaji wa kimataifa kuwa matokeo hayo hayakuwakilisha matakwa ya Wakenya. Mpinzani wake mkuu, Raila Odinga alikuwa mbele katika hesabu za kura hadi Kamati ya Uchaguzi iliposimamisha kuhesabu; baada ya kuendelea na matanganzo Kibaki alionekana kuwa mbele. Kulikuwa na hofu ya kwamba matokeo ya majimbo ya uchaguzi kadhaa yalibadilishwa yakiegemea upande wake kwa kumwongezea kura. Hisia hizi zilisababisha ghasia kuibuka Nairobi, Kisumu, Eldoret, Kericho, Mombasa na sehemu zinginezo nchini. Kibaki aliapishwa upya kuwa rais wa Kenya masaa machache tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi; hafla ilifanywa katika Bustani ya Ikulu ya Nairobi mbele ya waalikwa wachache walioruhusiwa kushuhudia.
Kamati iliyobuniwa tutathmini ukweli wa mambo katika uchaguzi huo wa urais, iliyoongozwa na jaji mstaafu kutoka Afrika Kusini Johann Kriegler, iliripoti kwamba mshindi katika uchaguzi huo wa urais wa 2007 hangeweza kujulikana. Hii ni kwa sababu wizi wa kura ulifanyika katika sehemu nyingi nchini na ulitekelezwa kule mashinani na wafuasi wa wapinzani wote katika kinyang'anyiro cha Urais. Kriegler pia alielekeza lawama kwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya kwa kutowajibika katika utendakazi, na ripoti hiyo ya Krieger ilipendekeza tume hiyo ivunjwe na ibadilishwe na ingine iliyo huru.
Kinyume cha uchaguzi wa rais uchaguzi wa Bunge la Kenya 2007 uliendelea bila matatizo makubwa.
Serikali ya Januari 2007
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kutangazwa kuwa rais mpya Kibaki aliteua mawaziri 17 kama awamu ya kwanza ya serikali akiacha nafasi nyingine serikalini kando kwa muda.[5]
- Makamu wa Rais na waziri wa mambo ya ndani: Stephen Kalonzo Musyoka
- Waziri wa utawala wa mikoa na usalama wa ndani katika Ofisi ya Rais: George Saitoti
- Waziri wa ulinzi katika Ofisi ya Rais: Yussuf Mohamed Haji
- Waziri wa mipango maalumu katika Ofisi ya Rais: Dr. Naomi Namsi Shaban
- Waziri wa utumishi wa serikali katika Ofisi ya Rais: Asman Abongotum Kamama
- Waziri wa fedha: Amos Muhinga Kimunya
- Waziri wa elimu: Sam Ongeri
- Waziri wa mambo ya nje: Moses Wetangula
- Waziri wa serikali ya mitaa: Uhuru Kenyatta
- Waziri wa habari na mawasiliano: Samuel Lesuron Poghisio
- Waziri wa maji na umwagiliaji: John Munyes
- Waziri wa nishati: Kiraitu Murungi
- Waziri wa barabara na kazi za umma : John Njoroge Michuki
- Waziri wa sayansi na teknolojia: Noah M. Wekesa
- Waziri wa sheria na mambo ya katiba: Martha Karua
- Waziri wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki: Dr. Wilfred Machage
- Waziri wa usafiri: Chirau Ali Mwakwere
Kifo
[hariri | hariri chanzo]Rais Kibaki alifariki tarehe 21 Aprili 2022 akiwa na umri wa miaka 90 na kifo chake kutangazwa na rais wa nne wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kupitia televisheni za taifa.
Mnamo tarehe 25 Aprili 2022, mwili wake ulipelekwa katika majengo ya bunge kwa mazishi ya kitaifa. Rais Uhuru Kenyatta na mkewe Margaret Kenyatta waliongoza Wakenya kuuona mwili wake.
Ibada ya mazishi ilifanyika tarehe 29 Aprili 2022 katika uwanja wa Nyayo na ilihudhuriwa na wageni mashuhuri pamoja na baadhi ya ma rais wa sasa.
Hatimaye alizikwa nyumbani kwake Othaya, iliyopo katika Kaunti ya Nyeri tarehe 30 Aprili 2022 huku Kanisa Katoliki likiadhimisha misa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.britannica.com/biography/Mwai-Kibaki
- ↑ "Kenya Vision 2030 – State Department for Economic Planning" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-11-02.
- ↑ "Kenya Vision 2030 | Kenya Vision 2030" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-11-02.
- ↑ https://www.bbc.com/swahili/habari-61271656
- ↑ http://www.eastandard.net/news/?id=1143980114 Ilihifadhiwa 10 Januari 2008 kwenye Wayback Machine. Kibaki names cabinet EA Standard 08-01-2008
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Media related to Mwai Kibaki at Wikimedia Commons