Content-Length: 105234 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/Rasi_ya_Sinai

Rasi ya Sinai - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Rasi ya Sinai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rasi ya Sinai, Ghuba ya Suez (magharibi), Ghuba ya Aqaba (mashariki) inavyoonekana kutoka angani.

Rasi ya Sinai (kwa Kiarabu: سيناء, sina') ni rasi yenye umbo la pembetatu nchini Misri upande wa kaskazini wa Bahari ya Shamu inayounganisha mabara ya Afrika na Asia. Inahesabiwa kuwa sehemu ya mwisho wa Asia ya Magharibi.

Eneo la Sinai ni takriban km² 60,000, hasa jangwa. Imepakana na Ghuba ya Suez upande wa magharibi na Ghuba ya Aqaba upande wa mashariki. Upande wa magharibi Mfereji wa Suez unaunganisha Bahari ya Shamu na Mediteranea. Kaskazini ya mwisho wa Ghuba ya Aqaba ni mpaka kati ya Misri na Israel.

Mahali panapojulikana zaidi ndani ya eneo al rasi ni mlima Sinai (pia: mlima Horeb, Jabal Musa) unaoaminiwa ni mahali ambako Musa alipokea amri kumi za Mungu.

Kati ya Raffa (Kaskazini) na Tabba (Kusini) kuna mfereji wa Taabah - Raffah Straight (Bar Lev Line kwa Kihebrania).

Kwenye pwani ya rasi utalii ni sehemu muhimu ya uchumi.









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/Rasi_ya_Sinai

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy