Content-Length: 106565 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Ukurasa_wangu_na_kurasa_za_kamusi

Wikipedia:Ukurasa wangu na kurasa za kamusi - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Ukurasa wangu na kurasa za kamusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ukurasa wa mtumiaji ni ukurasa wako. Humo uko huru kuandika juu yako mwenyewe unavyopenda.

Kanuni ni tofauti katika kurasa za kawaida yaani kurasa za kamusi (kwa Kiingereza: Article space). Humo ni marufuku kuandika juu yako mwenyewe. Kuna ruhusa moja tu: kama wewe uliandika kitabu au kutoa wimbo na kazi hizo zimetajwa katika gazeti, kitabu au blogu, hapo unaweza kuingiza kiungo kwa habari hiyo kama marejeo katika makala iliyopo tayari. Lakini usiianzishe wewe mwenyewe! Wala usitumie ukurasa wako kama tangazo la biashara au kwa matusi dhidi ya wengine.

Maana hapa tupo katika kamusi elezo, si Facebook au mtandao mwingine wa kijamii. Sisi wachangiaji tunawasiliana kati yetu kwa kutumia kurasa za majadiliano na ukurasa wa jamii, pia kwa barua pepe.

Afadhali ulizia maswali yako kwanza kwa yeyote kati yetu Wakabidhi, tuko tayari kukusaidia!

Kuhariri ukurasa wako

Nenda kwa "Mapendekezo" hapo juu kwenye ukurasa wako.

Ukibofya hapo unaweza kuamulia tabia mbalimbali jinsi unavyoonekana na kupatikana kwa watumiaji wengine wa Wikipedia.

Unaweza kuchagua

  • Maelezo ya msingi (pamoja na kubadilisha neno la siri)
  • Lugha
  • Hitiari za barua pepe (hapa unaruhusu wengine kukuandikia email): Tunashauri ukubali kwa kuwa anwani yako haitaonekana. Wengine wataweza kukutumia baruapepe kupitia Wikipedia pekee.

Tahadhari kuhusu ukurasa wako

Tahadhari moja kuhusu ukurasa wako: tafakari vema unachotaka kutangaza juu yako! Tafakari kama ni vema kutaja jina lako halisi. Ukifanya kazi na kuwa na mwajiri - labda itakusaidia au kuleta hasara kama bosi wako anajua unatumia muda wako kwenye Wikipedia (hasa kama unahariri ukiwa ofisini! - wengine hawapendi au muda wa kazi). Basi utaamua mwenyewe!

Ukiwa huru kujieleza, huruhusiwi kutumia nafasi hii kwa matangazo ya kibiashara au kwa matusi.









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Ukurasa_wangu_na_kurasa_za_kamusi

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy