Nenda kwa yaliyomo

Mhusika (fasihi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wahusika)

Mhusika (kwa Kiing. character) katika fasihi simulizi ni kiumbehai au kisichokuwa na uhai, anayechorwa na msanii wa kazi ya fasihi kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa hadhira.[1]

Mfano wa wahusika hao ni binadamu, wanyama, miti, mawe, mapango n.k.

Aghalabu wahusika wa fasihi simulizi ni wengi kwani wanahusisha viumbe wote, wenye uhai na wasiokuwa na uhai.

Kuna namna mbalimbali za kuainisha wahusika[2]

1. Wahusika wakuu. Hawa hutawala visa katika kazi za kifasihi maana hadithi huwahusu wao na athari yao ni kubwa hivi kwamba kama hawangekuwa, basi nayo hadithi haingekuwa. Wakitenda mema, huitwa "nguli" ilhali wa maovu huitwa "hasidi".

2. Wahusika wadogo/wasaidizi ambao huwa karibu na wakuu ili kusaidia kuwaelewa vyema. Hukuza msuko/ploti na maudhui.

3. Wahusika wajenzi. Hawa huwa karibu na wahusika wakuu na wadogo kwani husaidia kuzijenga sifa na umuhimu wa wahusika wakuu na wadogo.

4. Wahusika bapa hushikilia misimamo yao katika kazi husika. Hawabadiliki. Wakiwa hasidi hubaki hivyo hadi mwisho na wakiwa nguli vivyo hivyo.

5. Wahusika duara huakisi tabia zote za kibinadamu, njema na mbaya.

Ni vyema kufahamu kuwa mhusika mmoja anaweza kuingia katika makundi tofautitofauti ya uhusika.

  1. Omukabe wa Omukabe: Dhana ya Wahusika https://www.academia.edu/37693895/Dhana_ya_Wahusika
  2. Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI inataja: mhusika bapa; ~ nguli; ~ mkuu; ~ msaidizi; ~ sugu; ~ wa mikoba minne/duara bapa.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mhusika (fasihi) kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy