CHOIR SONGS - Do - 084844

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 38

WIMBO UKURASA

I LEFT THE WORLD…………………………………………………………………………………………………………………………………..3


I’VE A MESSAGE……………………………………………………………………………………………………………………………………...3
MWOKOZI POKEA……………………………………………………………………………………………………………………………………4
NENO LA BWANA…………………………………………………………………………………………………………………………………….4
PENDO LANGU…………………………………………………………………………………………………………………………………………5
BWANA MUNGU SEMA NAMI…………………………………………………………………………………………………………………5
NASHUKURU MUNGU……………………………………………………………………………………………………………………..………6
REHEMA YA BABA YETU…………………………………………………………………………………………………………………..………6
FURAHIA BWANA…………………………………………………………………………………………………………………………………….7
BWANA UMEKAWIA………………………………………………………………………………………………………………………………..7
NICODEMO KAENDA………………………………………………………………………………………………………………………………..8
BWANA NIPE UWEZO……………………………………………………………………………………………………………………………...8
BWANA YESU ALITAMKA…………………………………………………………………………………………………………………………9
TUMWAGALANYO YESU………………………………………………………………………………………………………………………….9
YESU KWETU NI RAFIKI…………………………………………………………………………………………………………………………...9
BABA YANGU ANA MALI NYINGI……………………………………………………………………………………………………………10
BWANA U SEHEMU YANGU…………………………………………………………………………………………………………………..10
SIKIA NIWAAMBIENI……………………………………………………………………………………………………………………………..11
MSHUKURUNI MWOKOZI……………………………………………………………………………………………………………………..11
EWE ROHO WA BWANA…………………………………………………………………………………………………………………………11
MUNGU BABA MUNGU MWANA…………………………………………………………………………………………………………..12
MLANGONI PA MOYO……………………………………………………………………………………………………………………………12
KUMBUKA SIKU ZILE ZA NUHU………………………………………………………………………………………………………………13
JITAYARISHE NDUNGU YANGU……………………………………………………………………………………………………………..13
NIMEWEKEWA TAJI NA BWANA…………………………………………………………………………………………………………….14
WIVU NI MBAYA…………………………………………………………………………………………………………………………………….14
AMINI AMINI NAWAMBIA……………………………………………………………………………………………………………………..15
HERI KUWA NA YESU……………………………………………………………………………………………………………………………..15
NIMELEMEWA NA HATIA ZANGU…………………………………………………………………………………………………………..16
ALFA NA OMEGA……………………………………………………………………………………………………………………………………16
NIMEAHIDI YESU……………………………………………………………………………………………………………………………………17
BWANA NIMULIKIE………………………………………………………………………………………………………………………………..18
BINADAMU NI MAVUMBI……………………………………………………………………………………………………………………..18
GANA GANANGA MU MWOYO……………………………………………………………………………………………………………..19
NIJAPOSEMA KWA LUGHA…………………………………………………………………………………………………………………….19
HARUSI YA MUNGU……………………………………………………………………………………………………………………………….20
NDOA IPEWE HESHIMA………………………………………………………………………………………………………………………….20
KIJITO CHA UTAKASO…………………………………………………………………………………………………………………………….21
NILIKUWA NIMEPOTEA…………………………………………………………………………………………………………………………21
NDIYO DHAMANA…………………………………………………………………………………………………………………………………22
NIMEVIPIGA VITA………………………………………………………………………………………………………………………………….22
HAYA TUBUNI NYOTE…………………………………………………………………………………………………………………………….23
BWANA ASEMA……………………………………………………………………………………………………………………………………..23
UNIREHEMU EE BWANA………………………………………………………………………………………………………………………..24

1
KUNA NURU…………………………………………………………………………………………………………………………………………..24
ALITUPENDA SANA YESU……………………………………………………………………………………………………………………….25
WAKUU WA MAKUHANI………………………………………………………………………………………………………………………..25
BWANA WA MAJESHI ASEMA………………………………………………………………………………………………………………..26
MWAMBA WENYE IMARA……………………………………………………………………………………………………………………..26
KARIBU NA WEWE…………………………………………………………………………………………………………………………………27
BABA YETU…………………………………………………………………………………………………………………………………………….27
SALAMA………………………………………………………………………………………………………………………………………………...28
WAVUVI…………………………………………………………………………………………………………………………………………………28
KIMBIA…………………………………………………………………………………………………………………………………………………..29
NABII ISAYA …………………………………………………………………………………………………………………………………………..30
TUMEPATA HABARI ……………………………………………………………………………………………………………………………...30
SIKIA SAUTI ……………………………………………………………………………………………………………………………………………30
LAKINI NAJUA HAKIKA …………………………………………………………………………………………………………………………..31
MUNGU AMECHAGUA ………………………………………………………………………………………………………………………….31
TWAENDA …………………………………………………………………………………………………………………………………………….32
BABA YETU ……………………………………………………………………………………………………………………………………………32
PONGEZI KWA BWANA NA BI ARUSI ……………………………………………………………………………………………………..33
TUKUTENDEREZA YESU …………………………………………………………………………………………………………………………33
BULIJJO TUTENDEREZA EKIBUGA KYAFFE ………………………………………………………………………………………………34
KATIKA MJI MWEMA …………………………………………………………………………………………………………………………….35
FURAHA KWA ULIMWENGU ………………………………………………………………………………………………………………….36
KUTAKUWA MWANGA ………………………………………………………………………………………………………………………….36
SAUTI YA BWANA ………………………………………………………………………………………………………………………………….37
NI SIKU TUKUFU ……………………………………………………………………………………………………………………………………37
HARUSI YA MUNGU ………………………………………………………………………………………………………………………………38

2
I LEFT THE WORLD
1. I left the world to have the cross,
The way I choose was good for me,
Troubles to me have grown a lot,
Carry me home my gentle Lord x2

Carry me home my gentle lord x3


My home is not on this rough world x2

2. The journey is long with trouble,


Told but I praise you my Lord,
I’ll have my fruit to you I cry,
Carry me home my gentle Lord x2

3. In heaven I’ll have my lord around,


The devil will sit in my sorrow,
Way and l’ll be free from all,
Carry me home my gentle Lord x2

I[VEAMESSAGE
1. I’ve a message from the lord (halleluyah)
The message unto you I’ll give,
It’s recorded in his word (halleluyah)
It’s only that you look and live x2

Look and live, my brother live


Look to Jesus now and live,
I[}]vR]`}~Rooo˙R
I[}vo˙R˙} look and live x2

2. I’ve a message full of love (halleyuyah)


A message from my friend for you,
It’s a message from above (halleluyah)
Jesus said it and I know it’s true x2

3. Life is offered unto you (halleluyah)


Eternal life your soul shall have,
If you only look to him (halleluyah)
Look to Jesus who alone can save x2

3
MWOKOZI POKEA
1. Mwokozi pokea roho yangu,
Nazama pekee yangu-uuu,
Matopeni mwa Yule shetani,
Ee bwana nakuomba x2

Ee mungu baba yangu,


Nishike nisizame,
Roho yangu ya umia,
Bwana na kulilia x2

2. Wakristo shetani yu karibu,


Ili ku—tujaribu-uuu,
Ushindi neno lake mungu,
Tukeshe na kuomba x2

3. Sisi tu napozitenda dhambi,


Yesu twa msulubisha-aaa,
Tukumbuke siku ile ya mwisho,
Tukitupwa motoni x2

NENO LA BWANA
1. Neno la bwana litatimiza,
Kama jinsi alivyosema,
Na mataifa yataokoka,
Hizi ni nyakati za mwisho x 2

Bwana, bwana, bwana,


Bwana yesu tuhurumie,
Bwana, bwana, bwana,
Yesu mwokozi utuokoe x2

2. Vita na njaa na ukavu mwingi,


Tetemeko kila mahali,
Ndugu na dada wanang’ombana,
Yesu mwokozi utuokoe x2

3. Twaiomboea siku hiyo,


Isiwe ya baridi sana,
Kwa wenye mimba wanyonyeshao,
Wasije wakateta sana x2
4
PENDO LANGU
1. Pendo langu mimi nakupa sababu,
Ewe mungu wangu unanipenda x2

Pendo langu nakupa


Pendo langu x2

2. Pendo langu mimi nakupa sababu,


Ewe mungu wangu uliniponya x2

3. Pendo langu mimi nakupa sababu,


Ewe mungu wangu ulinifia x2

4. Pendo langu mimi nakupa sababu,


Ewe mungu wangu ndiwe mwokoxi x2

BWANA MUNGU SEMA NAMI


1. Bwana mungu sema name,
Nami nitakutumikia x2

Moyo wangu moyo x2


Moyo wangu nenda daima x2

2. Na mavuno ndiyo mengi,


Na wavunaji ni wachache x2

3. Nitaomba mungu baba,


Mwana na roho mtakatifu x2

4. Wakosefu ndio sisi,


Twakuomba uturudishe x2

5
NASHUKURU MUNGU
1. Nashukuru mungu, kwa upendo wake,
Alionionyesha mimi, kaacha yote juu,
Akashuka chini, kunirudisha mimi kwake x2

Sop: Upendo t ananipenda x2


All: Upendo t ananipenda x2
Ijapo mimi ni mnyonge na mwenye dhambi tele,
Ninajua ananipenda x2

2. Asipokuwepo, sina raha kamwe,


Ni rafiki wangu mkuu mno, nikaapo mbali,
Yeye hunirudisha, kifuani na pumzika x2

3. Pale msalabani, dhambi zetu sisi,


Bwana yesu katusamehe, humu duniani,
Sisi twasubiri, kurudi kwake bwana yesu x2

4. Bado ananipenda, japo mimi mkosa,


Nashukuru kwa pendo lake, mengineyo sijui,
Ila neno hili, bwana yesu ananipenda x2

REHEMA YA BABA YETU


1. Rehema ya baba yetu, yaangaza nchi yake,
Lakini ametuweka, tuwe walinzi wake x2

Taa zenu na ziwake, nuru zenu tumeni,


Msafiri asizame, mwokoeni majini x2

2. Taa zitengenezeni, mwokoeni msafiri,


Aangukae majini, na asife gizani x2

3. Giza ya dhambi twaona, mawimbi twasikia,


Wengine wanatafuta, nuru za kutulia x2

6
FURAHIA BWANA
1. Furahia bwana akupenda, aliyekuweka duniani,
Kuishi kwa raha na amani, uwapende wote duniani x2

Masha, mashaka mashaka twayaona,


Huzu, huzuni huzuni umeingi,
Niki, nikimbie wapi nijifiche,
Kimbi, kimbilio langu ni kwa bwana x2

2. Mimi kama picha duniani, nikimbie wapi nijifiche,


Kimbilio langu ni kwa bwana, yeye ndiye aniongozaye x2

3. Mimi kama picha duniani, sijui wakati wala siku,


Ooh nikimbie wapi nijifiche, kimbilio langu ni kwa bwana x2

BWANA UMEKAWIA
1. Bwana umekawia, utatujia lini,
Tumechoka maovu, twaomba uje bwana x2

Sop: Nili- nilini bwana wetu,


Sop: Nili-nilini utakuja rafiki,
Sop: Kwaku-kwakuwa ulimwengu,
Waonyesha dalili za mwisho,
Sop: Haki-hakikia tunakuomba, tunakuomba baba,
Bwana uteremke x2

2. Maovu yamezidi, vifo magonjwa na njaa,


Hizi zote dalili, kuja kwake karibu x2

3. Hizi zote dalili, zinatimia sasa,


Kilichobaki ndugu yangu, bwana atarejea x2

4. Na sisi wakristo, tushike neno lake,


Na tena tusimame, imara halleluyah x2

7
NICODEMO KAENDA
1. Bass: Nicodemo kaenda usiku kwake yesu,
All: Yesu twajua wewe ndiwe mwalimu, uliyetoka juu kwa mwenyezi mungu,
Hakuna awezae kufanya haya (yote), nifanye nini bwana niokolewe x2

Sop:Yesu akamjibu akamwambia (amini)


All: Amin Amin ninakuambia, usipozaliwa tena mara ya pili (hauta),
Hautauona ufalme wa mungu x2

2. Bass: Nicodemo kaona ni jambo ngumu sana,


All: Inawezekana mtu mzima kuingia tumboni mwa mama yake,
Kisha azaliwe tena mara ya pili (hauta), hautauona ufalme wa mungu x2

3. Bass: Ewe-ewe amini vile ninakwambia,


All: Ukisikia yale ninakwambia utaingia je tumboni mwa mama yako,
Kisha uzaliwe tena mara ya pili (hauta), hautauona ufalme wa mungu x2

BWANA NIPE UWEZO


1. Bwana nipe uwezo, kama Petro Simoni,
Nipite juu ya maji, bwana nipe imani x2

Ewe mwenzangu umajini tembea,


Ewe tembea, eeh mwenzangu tembea,
Kweli ninatembea, lakini bado nazama,
Ni kwa sababu, imani yangu haba x2

2. Duniani bahari, dhambi nazo mawimbi,


Chunga sana mawimbi, usizame majini x2

3. Ukimshinda shetani, umeshinda mawimbi,


Ukilemewa na dhambi, utazama majini x2

8
BWANA YESU ALITAMKA
1. Bwana yesu alitamka, mimi ndimi njia ya kweli,
Mtu haji kwa baba yangu, ila kwa njia yangu mimi x2

Hebu jiulizeee, njia gani uifuatayo,


Nawe waelekea wapi, na wafuata njia ya kweli x2

2. Ngamia ni rahisi sana, kuingia tundu la shindano,


Kuliko mtu mwenye dhambi, kuingia ufalme wa mbinguni x2

3. Njia nyembamba yenye taabu, ndiyo iendayo mbinguni,


Nayo pana na ya anasa, ndiyo iendayo jehanamu x2

4. Mimi ni alfa na omega, mimi ndimi mwanzo na mwisho,


Mtu haji kwa baba yangu, ila kwa njia yangu mimi x2

TUMWAGALANYO YESU
1. Tumwagalanyo yesu yatufilila, naye kovirwa vitifwa na vileka,
Na kovirwa yesu na kovirwa yesu, wange mulokosi x2

Tulisisikana naye muvanga, tulisanyika kumwanisa yesu,


Tuligenda naye wefwe mwigulu, yesu wange mulokosi x2

2. Mbuyari muno banji bamumanya, omukirizi kwene kwavalema


Na kovirwa yesu na kovirwa yesu, wange mulokosi x2

YESU KWETU NI RAFIKI


1. Yesu kwetu ni rafiki, huambiwa hajapia,
Tukiomba kwa babaye, maombi asikia,
Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya,
Kwamba tukimwomba mungu, dua angesikia.

2. Una dhiki na maonjo, una mashaka pia,


Haifai kufa moyo, dua atasikia,
Hakuna mwingine mwema, wakutuhurumia,
Atujua tudhaifu, maombi asikia.

3. Je hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,


Ujapodharauliwa, ujaporushwa pia,
Watu wangekudharau, wapendao dunia,
Hukwambata mikononi, dua atasikia.
9
BABA YANGU ANA MALI NYINGI
1. Baba yangu ana mali nyingi, hushika hazina zote mkononi,
Fedha zote na mawe dhamani, na dhahabu zote ulimwenguni x2

Ni mwana wa mfalme, mwana wa mfalme,


Pamoja na yesu, ni mwana wa mfalme x2

2. Mwana wa baba mwokozi wangu, alitembea humu ulimwenguni,


Bali anatuombea sasa, ili tuwe watu wake kabisa x2

3. Nilitupawa mbali duniani, nikakubali kuwa mwenye dhambi,


Bali sasa nimeokolewa, kweli jina langu limeandikwa x2

4. Hema au nyumba sioni shaka, makao mazuri nitayapata,


Nikihamishwa na watu wangu, nitafurahi na mwokozi wangu x2

BWANA U SEHEMU YANGU


1. Bwana u sehemu yangu, rafiki yangu wewe,
Katika safari yangu, tatembea na wewe x2

Pamoja na wewe bwana, pamoja na wewe,


Katika safari yangu, tatembea na wewe x2

2. Mali hapa sikutaka, ili niheshimiwe,


Na yanikute mashaka, sawa sawa na wewe x2

Pamoja na wewe bwana, pamoja na wewe,


Heri nikute mashaka, sawa sawa na wewe x2

3. Niongoze safarini, mbele unichukue,


Mlangoni mwa mbinguni, niingie na wewe x2

Pamoja na wewe bwana, pamoja na wewe,


Mlangoni mwa mbinguni, niingie na wewe x2

10
SIKIA NIWAAMBIENI
1. Sikia niwaambieni, Maisha yangu ya kale,
Wakati sijamjua yesu, shetani alinichezea x2

Naenda: Naenda mbinguni kwa baba, Kumuona mwokozi yesu,


Ya dunia nimeshayaacha,mimi naenda mbinguni kwa baba x2

2. Nilikuwa na Maisha mabaya, yasiyo mpendeza mungu,


Yasiyo pendeza wazazi, pamoja na majirani x2

3. Siku moja siku ya ajabu, sitaisahau kamwe,


Mwokozi yesu aliponikomboa, na sasa nimeokolewa x2

MSHUKURUNI MWOKOZI
1. Njoni tumwimbie bwana, mwamba wa wokovu wetu,
Mikononi mwake zimo pande za dunia,
Bahari ni yeye ndiye aliyeumba,
Na mikono yake ilituumba sisi x2

Mshukuruni mwokozi, enyi mataifa,


Pigeni vigelegele, pigeni makofi x2
Tangazeni rehema zake, leo asubuhi,
Semeni ya kuwa bwan ni mwenye adili x2

2. Bwana ametamalaki, mataifa yatasema,


Ameketi juu ya makerubi mbinguni,
Yeye mungu katika sayuni ni mkuu,
Atukuka juu ya mataifa yote x2

EWE ROHO WA BWANA


1. Ewe roho wa bwana, mungu wa utatu,
Niumbie imani, na upendo wako x2

Na upendo, wako bwana, na huruma, yako bwana,


Niumbie imani, na upendo wako x2

2. Uje roho wa bwana, mfariji mwema,


Udumu kwetu sisi, hata milele x2

3. Fadhili zako bwana, twaziona wazi,


Upole wako bwana, tumaini letu x2
11
MUNGU BABA MUNGU MWANA
1. Mungu baba, mungu mwana,
Mungu roho mtakatifu,
Wastahili sifa zote, toka moyo wangu x2

Umenipa nguvu nguvu, umenipa uzima,


Umenipa cheo cheo, cha kuwa mwana wako x2

2. Mtakatifu, mtakatifu,
Mungu baba wa majeshi,
Makerubi, maserafi, wakuimbia x2

Hakuna mwingine tena, mwenye enzi kama wee,


Utukufu wako baba, ni wa kipekee x2

3. Furaha yangu ni kujua,


Yote chini yakiisha,
Kuna taji la uzima, laningojea x2

Shikilia sana sana, kile ulicho nacho,


Mwovu shetani asije, kakunyang[v˙˘

MLANGONI PA MOYO
1. Mlangoni pa moyo, mgeni (amesimama x2),
Amesimam pale, mgeni (amesimama x2),
Umkaribishe sasa, umkaribishe mwana,
Wa baba wa upendo, mgeni (umkaribishe x2)

2. Moyo wako kwa bwana, fungua (fungulieni x2),


Asikuache mbali, fungua (fungulieni x2)
Umkubali rafiki, roho atafariji,
Naye atakutunza, fungua (fungulieni x2)

3. Usikie sauti ya bwana (uisikie x2)


Uyachague mambo ya bwana (mambo ya bwana x2)
Ufungue mlango, usimwambie bado,
Jina lake tumai ya bwana (jina la bwana x2)

4. Na ufungue moyo kwa bwana (fungulieni x2)


Utapewa msaada kwa bwana (msaada wetu x2)
Uzuri utavikwa dhambi ataondoa,
Ukifungua moyo kwa bwana (fungulieni x2)

12
KUMBUKA SIKU ZILE ZA NUHU
1. Kumbuka siku zile za Nuhu (garika x2)
Kumbuka siku zile za Nuhu
Garika ilimwagika x2

Wanadamu wote, viumbe vyote,


Kumbuka siku zile za Nuhu,
Nuhu ndiye aliokoka x2

2. Kumbuka siku zile za Rutu (sodoma na gomora)


Kumbuka siku zile za Rutu,
Rutu ndiye aliokoka x2

Wanadamu wote, viumbe vyote,


Kumbuka siku zile za Rutu,
Rutu ndiye aliokoka x2

3. Kumbuka siku zile za Musa (Misiri x2)


Kumbuka siku zile za Musa,
Misiri walitatizwa x2

Wanadamu wote, viumbe vyote,


Kumbuka siku zile za Musa,
Mapigo makubwa Misiri x2

JITAYARISHE NDUGU YANGU


1. Jitayarishe ndugu yangu, kumpokea mwokozi,
Mungu wangu aje kwako, jitayarishe ndugu x2

Sop: Yule atakaye,


All: Kula mwili wangu
Tena akunywe t damu yangu mimi,
Yeye atapata t uzima wa milele,
Kweli asema t bwana mwokozi x2

2. Bwana Yesu uje kwangu, uingie rohoni mwangu,


Usikubali Yule mwovu, aingie rohoni zetu x2

3. Yesu bwana naja kwako, saasa unipokee,


Mungu wangu anasema, jitayarishe ndugu x2

13
NIMEWEKEWA TAJI NA BWANA
1. Nimewekewa taji na bwana,
Sitapotea nikitazama,
Sawa na vyote vitakuwepo,
Siku hiyo ya uzima x2

Sop: Simama wee- simama mbele yake bwana,


Utaje ee- utaje vyote vya dunia,
Simama wee t simama sana kwake bwana,
utapokea uzima x2

2. Nikikumbuka makosa yangu,


Ninamwendea msalabani,
Ee bwana Yesu unikumbuke,
Siku hiyo ya uzima x2

3. Hebu tukeshe na tukiomba,


Tukiingojea siku hiyo,
Ya kuja kwake mwokozi Yesu,
Siku hiyo ya uzima x2

WIVU NI MBAYA
1. Wivu ni mbaya ndugu nakuonya,
Ulimfanya Yusufu wa Yakobo,
Akauzwa kule Misiri,
Na ndugu zake walimuonea x2

Bass: Yakobo alia


All: Ah Yusufu mwana wangu sijaamini macho yangu
Bass: Yakobo alia
All: Kama ni wewe uliye kufa na kumbe uko Misiri

2. Walipofika nyumbani kwa baba,


Walimdanganya kwamba ni Yusufu,
Ameliwa na mnyama mkali,
Yakobo alihuzunika sana x2

3. Alipofika kule Misiri,


Akawa mtumishi wa nyumbani,
Mwanamke wa nyumbani humo,
Alitamani kuzini naye x2

14
AMINI AMINI NAWAMBIA
1. Amini Amini nawambia, niinawambia,
Amini Amini mmoja wenu, atanisaliti x2

Nitampiga mchungaji wa kondoooo


Na kondoo wa kundi lake, watatawanyika x2

2. Twaeni mle mwili wangu, uwe ukumbusho,


Twaeni mnywe damu yangu, iwe ukumbusho x2

3. Mwana wa Adamu aenda zake, ilivyoandikwa,


Ole ni wake mtu Yule, amsalitie x2

Ole wangu, ole wako, umsalitie, bwana,


Ingekuwa heri, kwetu tusingelizaliwa x2

HERI KUWA NA YESU


1. Heri kuwa na Yesu kuliko mali,
Heri niwe mali ya bwana Yesu,
Heri kuwa na Yesu kuliko vyote,
Nampenda Yesu aliyenifia.

Yesu ni bora kushinda wafalme,


Mamlakani enzi ii,
Heri kuwa na Yesu kuliko mali,
Nampenda Yesu aliyenifia x2

2. Heri kuwa na Yesu ni ngao yangu,


Heri niwe mali ya bwana Yesu,
Heri kuwa na Yesu ni taa yangu,
Nampenda Yesu aliyenifia.

3. Heri kuwa na Yesu ni uzima wangu,


Heri niwe mali ya bwana Yesu,
Heri kuwa na Yesu ni nuru yangu,
Nampenda Yesu aliyenifia.

4. Heri kuwa na Yesu ni njia yangu,


Heri niwe mali ya bwana Yesu,
Heri kuwa na Yesu kuliko vyote,
Nampenda Yesu aliyenifia.

15
NIMELEMEWA NA HATIA ZANGU
1. Nimelemewa na hatia zangu,
Nami nataka kufika mbinguni,
Ingawa mwenye dhambi haingii,
Iko sauti yaniita nije x2

Naja kwako Yesu bwana,


Nisafishe dhambi zangu x2

2. Mimi mchafu nitaenda wapi,


Katika kwenye nchi takatifu,
Kitini kwa mwenyezi nisimame,
Iko mikono yanivuta vuta x2

3. Ingawa natamani kuifuata,


Njia ya haki dhambi yanipinga,
Lakini nasikia neno jema,
Tubu ingawa utasamehewa x2

4. Sauti yako Yesu nasikia,


Mikono yanivuta vuta,
Na damu yako yasafisha dhambi,
Na kuniweka safi mble yako x2
ALFA NA OMEGA
1. Mimi ndimi wa kwanza tena na wa mwisho,
Kusiwe na miungu wengine kabisa,
Ndivyo anavyosema bwana wa majeshi,
Mungu mtakatifu mwenye nguvu zote x2

Mimi nitampa Yule, taji ya uzima ule


Yule atakayeshinda ya dunia hayo yote
Atakuwa ndani yangu, hata nami ndani yake,
Kwenye utukufu ule tutaimba halleluyah x2

2. Mimi nilikuumba unitumikie,


Katika siku zote hapa duniani,
Mbona sasa waacha njia ile nzuri,
Wamfuata shetani atakupoteza x2

3. Machozi yetu yote bwana atafuta,


Tutakapo mwendea na kutubu dhambi,
Acha udanganyifu uje kwake leo,
Mungu mtakatifu mwenye nguvu zote x2

16
NIMEAHIDI YESU
1. Nimeahidi Yesu, kukutumikia,
Wewe u bwana wangu, urafiki pia,
Sitaogopa vita, wewe ndiwe mweza,
Sitaicha njia, ukiniongoza.

Imbeni alleluia, alleluia imbeni,


Shangwe kwa bwana Yesu,
Ndiye mweza wetu x2

2. Dunia I karibu, bwana siniache,


Na mengi majaribu, yako pande zote,
Siku zote adui, ni ndani na nje,
Bwana Yesu nivute, karibu na wewe.

3. Nikusikie wewe, nena nami bwana,


Kelele za dunia, ndizo nyingi sana,
Nena kunihimiza, au kuniponya,
Nena nikusikie, mwenye kuniponya.

4. Umewapa ahadi, wakufuatao,


Kwenda uliko wewe, wawe huko nawe,
Nami nimeahidi, kukutumikia,
Nipe nehema bwana, ya kukuandamia.

5. Hatua zako bwana, nikizikanyaga,


Wewe u mwenye nguvu, mimi ni mnyonge,
Niongoze nivute, nishike daima,
Mwishoni niwasili, mbinguni salama.

17
BWANA NIMULIKIE
1. Nitamwandama bwana aliyeniokoa,
Yesu mwenye huruma unisaidie x2

Sop: Bwana zimulike njia zangu


All: mwanga wako bwana niangazie x2
Alto: Bwana mulika mulika njia zangu
Tena: Bwana mulika mulika njia zangu
Bass: Bwana angaza angaza njia zangu
All: Mwanga wako bwana niangazie x2

2. Yesu ninakuomba mimi mwenye dhambi,


Sijawa mwema bado nateseka sasa x2

3. Bwana ninakuomba waite na wengine


Waja waimbe kwako wakusifu wewe x2

BINADAMU NI MAVUMBI

1. Binadamu, binadamu ni mavumbi,


Mavumbini, mavumbini atarudi,
Mwili wake, mwili wake wayeyuka,
Kama ua, kamau a la kondeni.

Na tukifika huko,
Tutaimba halleluiah,
Makao ya raha (ya Starehe),
Yako huko mbinguni.

2. Ndugu yangu, ndugu yangu kwaheri,


Ya dunia, ya dunia kwaheri,
Ninaenda, ninaenda mbinguni,
Ya dunia, ya dunia kwaheri.

3. Ninaona, ninaona kwa mbali,


Ya dunia, ya dunia kwaheri,
Ninaenda, ninaenda mbinguni,
Ya dunia, ya dunia kwaheri.

18
GANA GANANGA MU MWOYO
1. Gana gananga mu mwoyo,
Lwangendanga kuinzira,
Mwoyo gwange gurizia hai,
Kwa muviri guruhanga x2

Ndayona, oh ndayona,
Sameha mwami ndayona x2

2. Ndoranga mugera niguvita,


Gwa masai go muhonyi,
Sigaveye ge tsinyama,
Gaza kwogiza mwoyo gwange x2

3. Logendo norutambi muno,


Niviguru nivinyingi,
Zinzira nitsia magina,
Nduhi mwami oh ndayona x2

NIJAPOSEMA KWA LUGHA


1. Nijaposema kwa lugha,
Za wanadamu na malaika,
Kama sinao upendo,
Mimi si kitu kabisa.

Sifai mbele za bwana x2


Kama sinao upendo,
Mimi si kitu kabisa.

2. Hata nikiwa nayo mali,


Ya kuwalisha masiskini,
Kama sinao upendo,
Mimi si kitu kabisa.

3. Hata nikiwa na imani,


Ya kuhamisha milima,
Kama sinao upendo,
Mimi si kitu kabisa.

19
HARUSI YA MUNGU
Sop: (Harusi ya Mungu)
All: Harusi ni siri kubwa kwa wale waliotimiza x2
Sop: (Mnapoahidi)
All: Wakristo wote wanashuhudia yale mnayosema x2
Bass: (Ni dhahabu yenu)
All: Muitunze kila siku isije chafuka x2
Alto: (Naye Mungu) wa uwezo (Maishani) mwenu awasaidie x2

Sop: (Mlioooana)
All: Kumbukeni siri hii ni siri ya ndoa ya rohoni x2
Sop: (Kujipamba kwenu)
All: Kusiwe kwa nje tuu bali mjipambe roho zenu x2

Sop: (Mtakatifu Paulo)


All: Katika waraka wake kwa waefeso sura ya tano x2
Sop: (Aliwaambia)
All: Waume wapendeni wake zenu kama miili yenu x2
Sop: (Nanyi wanawake)
All: Mtii waume zenu kama vile apendavyo bwana x2

NDOA IPEWE HESHIMA


Sop: Ndoa ipewe heshima x2
All: Ndoa ipewe heshima x2

Cana ya galilaya, Yesu kageuza maji,


Hata yakawa divai.

Mungu ibariki harusi hii,


Inayofungwa leo.

Sop: Ya Isaka na Rebbeca


All: Ya Isaka na Rebbeca

Mungu ibariki harusi hii


Inayofungwa leo (majina)

20
KIJITO CHA UTAKASO
1. Kijito cha utakaso,
Ni damu ya Yesu,
Bwana anao uwezo,
Kunipa wokovu x2

Kijito cha utakaso,


Nizame kuoshwa humo,
Namsifu bwana kwa hiyo,
Nimepata utakaso x2

2. Viumbe vipya naona,


Damu ina nguvu,
Imeharibu uovu,
Imeharibu uovu , Uliodumu x2

3. Naondoka kutembea,
Nuruni mwa mbingu,
Na moyo safi kabisa,
Kumpendeza mungu x2

4. Ni neema ya ajabu,
Kupakwa na damu,
Na bwana Yesu kumjua,
Yesu wa msalaba x2

NILIKUWA NIMEPOTEA
1. Nilikuwa nimepotea,nilikuwa muovu sana,
Bwana Yesu akanifia, nimepata wokovu tena x2

Sop: Kama si pale


All: Kama si pale kalivary x3
Sop: Jehanamu
All: Jehanamu ingekuwa yangu.

2. Marafiki hawakuamini,wazazi walinishangaa,


Kama si pale kalivary, Jehanamu ingekuwa yangu.

3. Sasa ninaishi na Yesu,maisha ya raha kabisa,


Bibilia ni nguzo yangu, nimepata wokovu tena.

21
NDIYO DHAMANA
1. Ndiyo dhamana Yesu wangu,
Hunipa raha za mbinguni,
Mrithi wa wokovu wako,
Nimezaliwa kwa roho yake.

Habari njema raha yake,


Yesu ndiye mwokozi wangu,
Habari njema raha yangu,
Yesu ndiye mwokozi wangu x2

2. Kumsalimu moyo wangu,


Mara namwona malaika,
Aniletea habari njema,
Wananilinda taokoka.

3. Sina kinyuma nashukuru,


Mchana kutwa huja kwangu,
Usiku kucha kuna nuru,
Mwokozi wangu ndimi huru.

4. Hali na mali aniitwaa,


Mara namwona anifaa,
Nami nangoja kwa subira,
Akiniita nije mara.

NIMEVIPIGA VITA
Sop:Nimevipiga vita
Nimevipiga vita vilivyo vizuri x2
Sop: (Mwendo) All: Mwendo nimeumaliza,
Sop: (Imani) All: Imani nimeilindaa,
Mwendo nimeumaliza, imani nimeilindaa x2

1. Baadaya hayo, nimewekewa tajii,


Nimewekewa tajii, tajii ya ushindii

2. Neno lake bwana, linasema njooni,


Linasema njooni, tumlaki bwanaa.

3. Ewe ndugu yangu, tukazane mwendoni,


Tukazane mwendoni, tutavishwa taji.

4. Kwaheri sasa, ninaenda,


Nimeshafikisha siku zangu, kwa taabu.

22
HAYA TUBUNI NYOTE
1. Sop: Haya tubuni nyote (nyote)
All: Haya tubuni dhambi, mkaihubiri bibilia,
Sop: Kisha mkabatizwe (nyote)
All: Kisha mkabatizwe kwa jina lake mwenyezi mungu x2

Sop: M}l}R}~uuuYX
S}WR}R}ul](~uuuYXX
All: Atawaongoza Maisha ya utukufu
S}WH]˙}}}}YXX
All: Hiyo ni ahadi yake bwana Yesu,
Aliowaahidi wote wamwaminio x2

2. Sop: Ndipo mtapokea (nyote)


All: Ndipo mtapokea msamaha wa dhambi zenu

3. Sop: Kisha mwamini Yesu (nyote)


All: Kisha mwamini Yesu, yeye ni bwana mwokozi wetu x2

BWANA ASEMA
1. Bwana asema, nimtume nani,
Na ni nani, atakaye kwenda badala yangu,
Na ni nani, atakaye kwenda badala yangu.

Nitume mimi bwana x2


Nitume mimi bwaana,
Nitume mimi bwaana.

2. Ninaogopa…. Umri mdogo,


Kuhubiri neno lake bwana, huko niendako,
Kuhubiri neno lake bwana, huko niendako.

3. Mdomo wangu, ni mchafu sana,


Uuchome kwa kaa la moto, unitakase,
Uuchome kwa kaa la moto, unitakase.

4. Aliniambia, usiogope,
Nitakupa ujasiri mwingi, kutoka kwangu,
Nitakupa ujasiri mwingi, kutoka kwangu.

23
UNIREHEMU EE BWANA
1. Bass: Unirehemu ee mungu,
All: Unirehemu mimi,
Bass: Maana nafsi yangu imekukimbilia,
All: Imekukimbilia wewe x2

Bass: Hata misiba hii t itakapo


All: Hata misiba hii itakapopita
Nita Mwita mungu aliye juu.

2. Bass: Wanadamu meno yao,


All: Ni mikuki na mishale,
Bass: Na ndimi zao ni upanga,
All: Ni upanga mkali x2

3. Bass: Wameweka wivu,


All: Ili kuninasa miguu,
Bass: Nafsi yangu imeinama,
All: Wamechimba shimo mbele yangu x2

4. Bass: Wametumbukia ndani yake,


All: Ee mungu moyo wangu uthabiti,
Bass: Moyo wangu uthabiti,
All: Nitaimba, nitaimba zaburi x2

KUNA NURU
1. Kuna nuru kubwa ya ajabu, iangazayo ndiye Yesu,
Kutuangazia walimwengu, tusipotee dhambini.

Tre: Njoo kwenye nuru ndugu yangu


All: Huko ndiko kwenye raha
Tre: Usitangetange kwenye giza
All: Huko hakuna Amani

2. Mungu Baba ni mwenye upendo, alimtuma mwana wake,


Aangaze kote duniani, ili watu waokoke.

3. Mimi na wewe zote twaitwa, tuangaze kwa mataifa,


Ili watu wasipotee dhambini, wakaupate uzima.

24
ALITUPENDA SANA YESU

1. Alitupenda sana yesu, aliweza toka mbinguni,


Aje hapa atuokoe, Ee Bwana Bwana ni wa kweli x2

Ewe Bwana, Ee Bwana x4


Ewe Bwana, Bwana ni wa kweli x2

2. Je ndugu mje tumwimbie, msije mkafika kesho,


Wakati wetu umekwisha, Ee Bwana Bwana ni wa kweli x2

3. Siku tutafika mbinguni, sijui namna itakuwa,


Furaha na kushangilia, Ee bwana utupe nguvu x2

Ewe Bwana, Ee Bwana x4


Ewe Bwana, utupe nguvu x2

WAKUU WA MAKUHANI

1. Wakuu wa makuhani, walimshika Yesu,


Wala hakukuwa na kosa, walimusulubisha x2

Bass/Sop: Msalaabani
All: Mateso mengi yalimpata
Bass/Sop: Msalaabani
All: Mateso mengi yalimpata
Bass/Sop: Msalaabani
All: Mateso mengi yalimpata msalabani x2

2. Wakati huu ndio wetu, wakuandamana naye,


Ili tupate kuokoka, na kuishi milele x2

3. Mateso mengi yalimpata, pale msalabani,


Hata kupigwa alipigwa, aliteseka sana x2

25
BWANA WA MAJESHI ASEMA

1. Bwana wa majeshi asema hivi leo,


Kwamba uende kule mwituni
Bass: Mwituni
Ukaniletee miti ukalijenge kanisa langu, Bwana asema x2

Sop: Hilo hilo


All: Hilo ni langu x2
Sop: Hilo x2
All: Hilo ni langu jenga kanisa

2. Bwana wa majeshi asema hivi leo,


Kwamba uende kule shambani ,
Bass: Shambani
Ukaniletee vyakula ukalijengee kanisa langu, Bwana asema x2

3. Bwana wa majeshi asema hivi leo,


Kwamba uende kule nyumbani,
Bass: Nyumbani
Ukaniletee ujuzi ukalijenge kanisa langu, Bwana asema x2

MWAMBA WENYE IMARA

1. Mwamba wenye imara, kwako nitajificha,


Maji hayo na damu, yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi, hunifanya mshindi.

2. Kwa kazi zote pia, sitimizi sheria,


Nijapofanya bidii, nikilia na kudhii,
Hayaishi makosa, ndiwe wa kuokoa.

3. Sina cha mkononi, naja msalabani,


Nili tupu nivike, nimnyonge nishike,
Nili mchafu naja, nioshe nisijafa.

4. Nikungojapo chini, nakwenda kaburini,


Nipaapo mbinguni, na kukwona enzini,
Roho yangu na iwe, rahani mwako wewe.

26
KARIBU NA WEWE
1) Karibu na wewe, Mungu wangu, Karibu zaidi, Bwana wangu,
Siku zote niwe, Karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.

2) Nami nasafiri, duniani, Pakupumzika, Sipaoni,


Nilalapo niwe karibu na wewe,Karibu zaidi Mungu wangu.

3) Yote unipayo, yanivuta, Pakukimbilia, Nitapata,


Na nielekezwe karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.

4) Na kwa nguvu zangu, Nikusifu, Mwamba uwe maji ya wokovu,


Mashakani niwe karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.

5) Na nyumbani mwa juu, Baba yangu, Zikikoma hapa siku zangu,


Kwa furaha niwe pamoja na wewe, Karibu kabisa Mungu wangu.

BABA YETU

1. Baba yetu aliye mbinguni, Amenifurahisha yakini,


Kuniambia mwake chuoni, Ya kuwa nami yesu pendoni x2

Anipenda mwokozi yesu, Anipenda, Anipenda,


Anipenda mwokozi yesu, Anipenda mimi x2

2. Nimuachapo kutanga mbali, Yeye yu hivyo hupenda kweli,


Hunirejeza kwake moyoni, Kweli yu nami yesu pendoni x2

3. Anipenda nami nampenda, Kwa wokovu alionitenda,


Akanifia msalabani, Kwa kuwa nami yesu pendoni x2

4. Haya kujua yanipa raha, Kumuamini kuna furaha,


Humfukuza mara shetani, Kuwa yu nami yesu pendoni x2

5. Sifa ni nyingi asifiwazo, Moja ni sana katika hizo,


Wala siachi hata mbinguni, Kwamba yu nami yesu pendoni x2

27
SALAMA

1. Nionapo Amani kama shwari, Au nionapo shida,


Kwa hali zote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu x2

Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu x2

2. Ingawa shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani,


Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu x2

3. Dhambi zangu zote wala si nusu, Zimewekwa msalabani,


Wala sichukui laana yake, Ni salama rohoni mwangu x2

4. Ee bwana himiza siku ya kufa, Panda itakapolia,


Utakaposhuka sitaogopa, Ni salama rohoni mwangu x2

WAVUVI

1) Bwana Yesu alipokuwa akienda,


Kando ya bahari ya Galilaya,
Alikuwa akitazama wavuvi,
Wavuvi wa watu x2

Aliwaona wandugu wawili,


Simoni Petero na ndugu yake,
Na ndugu yake aitwae Anderea,
Wavua samaki x2

2) Bwana Yesu anatuita tuache,


Yote ya dunia na tumfuate,
Tufanane na wanafunzi wa bwana,
Waliomfuata x2

3) Nawe ndugu umkubali mwokozi,


Atakusamehe makosa yako,
Atakuosha utakuwa mweupe,
Kuliko theluji x2

28
KIMBIA
1) Bwana Yesu atakaporudi, Siku hiyo ni furaha tele,
Waliookoka watashangilia, Na wenye dhambi nikusaga meno.

Bass: Kimbia, Kimbia,


All: Mwenye dhambi kimbia,
Bass: Hukumu,
All: Hukumu yaja,
Bass: Kimbia,
All: Kimbia mwokozi Bwana Yesu atakuokoa x2

2) Ee ndugu yangu, Yesu akuita, Uje kwake akubadilishe,


Atakuosha utakuwa safi, Kisha akufanye uwe mwana wake.

3) Damu ya Yesu huosha kabisa, Dhambi zote na kukutakasa,


Jaribu leo ujue ya kwamba, Ndani ya Yesu kuna raha tele.

NEARER, MY GOD, TO THEE

1) Nearer, my God, to Thee, Nearer to Thee,


E’en though it be a cross, That raises me,
Still all my song shall be, Nearer, my God, to Thee,
Nearer, my God, to Thee, Nearer to Thee.

2) Though like the wanderer, The sun gone down,


Darkness be over me, My rest a stone,
Yet in my dreams I’d be, Nearer, my God, to Thee,
Nearer, my God to Thee, Nearer to Thee.

3) Then, with my waking thoughts, Bright with Thy praise,


Out of my stony griefs, Bethel I’ll raise,
So by my woes to be, Nearer, my God, to Thee,
Nearer, my God to Thee, Nearer to Thee.

4) Or if on joyful wing, Cleaving the sky,


Sun, moon, and stars forgot, Upward I fly,
Still all my song shall be, Nearer, my God, to Thee,
Nearer, my God to Thee, Nearer to Thee.

29
NABII ISAYA
1) Nabii isaya, katabiri kuwa
Bikira maria, atachukua mimba x2

Sop: O O O Bikira
All: Tachukua mimba x2
Bass: Jina lake ataitwa Emmanuel
All: Furaha duniani, shangwe na nderemo x2

2) Mwokozi Yesu, kristo kazaliwa


Mle ndani, “Zizini” mwa ng’ombe x2

3) Sisi sote, na tufunge safari,


Twende sote, tukamwone Bwana x2

TUMEPATA HABARI
1) Tumepata habari, bwana Yesu amezaliwa,
Katika Bethlehemu ya Uyaudi x2

Tre: Aya
All: Shangilia x3 Yesu kazaliwa.

2) Mama juzi kutoka, mashariki walifika,


Manemane na dhahabu, walimtolea x2

3) Ewe ndugu yangu, uje kwake Yesu,


Umpokee Yesu, ili akuokoe x2

SIKIA SAUTI
1) Sikia sauti yake bwana,Yaita kwa upole urudi,
Tena ya kulilia mwenzangu,Uwache ya dunia utubu x2

Ukikubali leo utapona,Tena utakuwa safi kama theluji,


Ijapo dhambi zako ni nyekundu, Na zitakuwa kama vile safi

2) Sauti ni neno lake bwana, Yaita kwa upole urudi,


Tena ya kulilia mwenzangu,Uwache ya dunia utubu x2

3) Na ewe ndugu yangu, Sikia maneno yake bwana mungu,


Yaita kwa upole urudi, Uwache ya dunia utubu x2

30
LAKINI NAJUA HAKIKA

1) Lakini najua hakika, mtetezi wangu yu hai,


Hatimae atasimama, na kutawala juu ya nchi x2

Maisha haya ni ya muda, yamejaa matatizo,


Karibu tutawasili furaha, ni kwa wateule x2

2) Bila Yesu sina faida, Maisha yangu yanapita,


Ni furaha kuwa na Yesu, kwake kuna uzima tele x2

3) Duniani sisi wageni, hatuna mji hudumuo….,


Makao yetu ni mbinguni, mahali pa watakatifu x2

MUNGU AMECHAGUA

1) Mungu amechagua, leo siku ya furaha,


Ya kufunga ndoa, yenu ya Imani x2

Mmeacha wazazi wenu, kuishi pamoja katika ndoa,


Neno lake mwenyezi Mungu, liwe nuru maishani mwenu x2

2) …….Amechagua ataishi na nani,


Mungu akaamua ataishi na ……x2

3) …..Amechagua ataishi na nani,


Mungu akaamua ataishi na …..x2

4) Adam alifikiri ataishi na nani,


Mungu akaamua ataishi na Hawa x2

5) Hawa alifikiri ataishi na nani,


Mungu akaamua ataishi na Adam x2

31
TWAENDA
1) Bass: Twaenda x2
Mbinguni kuketi kule milele x2
All: Twaenda mbinguni kuketi kule milele x2

Bass: Bwana Yesu x2 (Ndiye Yesu mkombozi wetu x2)


Ndiye mkombozi bwana mkombozi wetu
All: Ndiye Yesu mkombozi wetu x2
Bwana mkombozi wetu x2

2) Bass: Twaimba x2
All: Twaimba kwa shangwe kumsifu Yesu mwokozi x2

3) Bass: Ni usiku x2
All: Ni usiku war aha ambao tunasubiri x2

BABA YETU
1) Tre: Baba yetu aliye juu mbinguni
All: Uturehemu
Tre: Watu wako maelefu mingi
All: Waokoke
Ten: Duniani x2
All: Wamujue baba x2

Bass: Sina shida x4


Tre: Kama ninaye Yesu mwenzangu
All: Sina shida
Tre: Kama nimetubu makosa
All: Sina shida
Tre: Baba ataniponya x2
All: Baba ataniponya x2
All: Namakosa yangu yote baba nayaleta mbele zako
Tre: Hakuna mwingine tena x2
All: Hakuna mwingine tena x2
Wakuniokoa dhambi zangu zote niokoke x2

2) Tre: Yesu alipopelekwa juu


All: Msalabani
Tre: Akatolewa kaafara Goligotha
Ten: Akasema
All: Yamekwisha x2

32
PONGEZI KWA BWANA NA BI ARUSI

1) Treble: (jina) Pongezi x2 kwa kumpata (jina)


All: Mume (jina) pongezi x2 kwa kumpata (jina) x2

Treble: Mmepatana
All: Mmepatana
Treble: Na kupendana
All: Nakupendana (kuanzia leo mjue mwili ni mmoja x2)

2) Treble: (jina) pongezi x2 kwa kumpata (jina)


All: (jina) pongezi x2 kwa kumpata (jina) x2

3) Treble: (jina) amini (jina) amini le oleo leoooooo


All: (jina) amini (jina) amini leo leo leo x2

4) Treble/ Alto: Nawe (jina) usiseme!


All: La! Huyu si mume (kuanzia leo mjue mwili ni mmoja x2)

5) Treble/Alto: Na wazazi musiseme!


All: La! Hawa si watoto

6) Treble/Alto: Na watoto musiseme!


All: La! Hawa si wazazi (kuanzia leo mjue mwili ni mmoja x2)
Kuanzia leo mjue-e-e mwili-ii ni-ii mmoja-aa

TUKUTENDEREZA YESU
1) Yesu mulokozi wange,
Leero nze wuwo wekke,
Omusaayi gwo gunnaazizza,
Yesu mwana gwendiga.

Tukutendereza Yesu,
Yesu mwana gwendiga,
Omusaayi gwo gunnazizza,
Nkwebaza mulokozi.

2) Edda nafuba bufubi,


Okufuna emirembe,
Leero mmaliridde ddala,
Okweyabiza Yesu.

3) Nnaababuliranga abantu,
Obulokozi bwanna,
Obutali bwa kitundu,
Obulamba bwe buwo.
33
4) Nnaatengeezanga eby Yesu,
N’ obuvumu ne sitya,
Eyanzigya mu busibe,
N’ okuwonya eyamponya.

5) Neebaza eyannunula nze,


Eyamponya wa kisa,
Yesu ankuma asanyusa era,
Bulijjo yeebazibwe.

BULIJJO TUTENDEREZA EKIBUGA KYAFFE

1) Bulijjo tutendereza,
Ekibuga kyaffe,
Ekyakubibwa muggulu,
Yesu kye yazimba.

Singa mbadd nebiwaawa,


Nga bamalayika,
Nandibuuse, nandituuse,
Eri mu saayuuni.

2) Era ennyumba zaakyo zonna,


Ziringa nga zaabu,
Ze zisinga zonna ddala,
Ezizimbibwa abantu.

3) Yesu mwali ye mukama,


Abafuga bonna,
Bamalayika beeyanza,
Nga bamuweereza.

4) Muntebe ye mufuluma,
Mazzi g’obulamu,
Agamasamasa ddala,
Nga effeeza ennungi.

5) Era gyali gye gumere,


Muti gwo’obulamu,
Amalagala kwe gali,
Agawonya abantu.

34
6) Ffe tusiime ekibuga,
Yesu kristo waffe,
Kye yatulongoosereza,
Ekiri mu ggulu.

7) Otuzibule amaaso,
Yesu tukulabe,
Tubiwulire ebigambo,
Bya mukama waffe.

MY SINS
1) My sins were flowing like a river,
When the Lord sacrifice me x2

Singing glory halleluyah


When the fire came down x2
When the Lord sacrifice me x2

2) My sins were higher than the mountain,


When the Lord sacrifice me x2

3) My sins were deep as a valley,


When the Lord sacrifice me x2

KATIKA MJI MWEMA

1) Katika Mji mwema mbinguni kwa Mungu x2


Ndipo ahadi zetu ziendapo x2

Mji wangu wee, uko mbinguni juu,


Nikiuona nina utamani,
Raha ya dhambi yanitia giza,
Nitauona lini Mji mwema x2

2) Mwokozi wetu Yesu, naye asikia x2


Yale maombi yetu tuombayo x2

3) Msikose kuomba, Yesu asikia x2


Naye atatufikisha mbinguni x2

35
FURAHA KWA ULIMWENGU

1) Furaha kwa ulimwengu, Bwana amekuja,


Nyote mkaribisheni, mioyo yenu na mpeni,
Wote wamshangilia, wote wamshangilie,
Na wote wamshangilie.

2) Furaha kwake dunia, mwokozi ni mfalme,


Bonde na milima na mwamba,Maji mitoni na shangwe,
Rudisheni sauti, rudisheni sauti,
Rudisheni na rudisheni sauti.

3) Atawala na neema, kwao mataifa,


Yuaja kutubariki, atuletea ushindi,
Kuharibu dhambi, kuharibu dhambi,
Kuharibu na kuharibu dhambi.

KUTAKUWA MWANGA

1) Kutakuwa mwanga, nyumbani mwa Bwana,


Nifikapo mwisho wa mwendo,
Nitapata raha mkononi mwa bwana,
Nifikapo mwisho wa mwendo.

Safari ikomapo siku ya mwisho


Nitakaribishwa na pendo
Kwa kuwa mwokozi ananingojea
Nifikapo mwisho wa mwendo.

2) Sitazikumbuka taabu za njia,


Nifikapo mwisho wa mwendo,
Sitawakumbuka walionipinga,
Nifikapo mwisho wa mwendo.

3) Nimuone rafiki aliye mwokozi,


Nifikapo mwisho wa mwendo,
Hiyo natamani katika mbinguni,
Nifikapo mwisho wa mwendo.

36
SAUTI YA BWANA
1) Sauti ya Bwana yaita kila siku,
Tubuni dhambi siku zinapita,
Usijelewe siku ya hukumu,
Bwana Yesu ndiye ataamua vita x2

Sop: Siku hiyo kubwa itakapofika


Hakuna kabisa mwenye kuijua
All: Wengine hulewa na kupenda anasa
Bwana Yesu ndiye ataamua vita x2

2) Wateule wa Bwana watafurahi sana,


Nyimbo za ushindi zikimsifu Bwana,
Mbinguni nyumbani mbinguni kwenye raha,
Ndugu yangu njoo twende na Bwana Yesu x2

3) Yesu atawaita watakatifu wake,


Atawapeleka kwenye kiti cha enzi,
Ndipo siku hiyo maombolezi mengi,
Kama utavuna kwenye ziwa la moto x2

NI SIKU TUKUFU
1) Ni siku tukufu, halleluyah, amina,
Ya kupumzika, halleluyah, amina,
Tuache shughuli, tumwabudu Mungu,
Bwana wa mbinguni, halleluyah, amina.

2) Ni siku tukufu, halleluyah, amina,


Tukufu kabisa, halleluyah, amina,
Njooni ndugu znagu, tumwabudu Mungu,
Kw roho na kweli, halleluyah, amina.

3) Ni siku tukufu, halleluyah, amina,


Ya furaha mno, halleluyah, amina,
Yesu kufufuka, na sasa yu hai,
Anatuombea, halleluyah, amina.

4) Ni siku tukufu, halleluyah, amina,


Ndiyo maarufu, halleluyah, amina,
Tunaye mwokozi, atuokoaye,
Sasa na milele, halleluyah, amina.

37
HARUSI YA MUNGU
(Sop) Harusi ya Mungu
(All) Harusi ni sisi kubwa kwa wale walioitimiza x2
(Sop) Mnapoahidi
(All) Wakristo wote wanashuhudia yale mnayosema
(Bass) (Ni dhahabu yenu) muitunze kila siku isijechafuka
(All) (Naye Mungu) wa uwezo (maishani) mwenu awasaidie

(Sop)(Mliooana) kumbukeni siri hii ni siri ya ndoa ya rohoni,


(All) (Kujipamba kwenu) kusiwe kwa nje tu bali mjipambe rohoni.

(Sop) (Mtakatifu Paulo) katika waraka kwa waefeso sura ya tano,


(All) (Aliwaambia) waume wapendeni wake zenu kama miili yenu.

(Sop)(Nanyi wanawake) mtii waume zenu kama vile apendavyo Bwana.

PRINTED BY
FILARETOS
DOMNIC

38

You might also like

pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy