Content-Length: 114330 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/Chuo_Kikuu_cha_Dar_es_Salaam

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Logo for University of Dar es Salaam
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mlimani
Wito kwa KiswahiliHekima ni Uhuru
Kimeanzishwa1961
AinaChuo cha Umma
WakfuChuo cha kwanza Tanzania
ChanselaDkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Makamu wa chanselaProf. William A.L. Anangisye
DeanMs. Paulina Mabuga
MahaliDar es Salaam, Tanzania
KampasiMain Kampasi, CoICT Kampasi, DUCE Kampasi, MUCE Kampasi, Zanzibar Kampasi, SJMC Kampasi na Mbeya Kampasi
RangiBluu, Nyeupe
MsimboMlimani, UDSM
Tovutihttps://www.udsm.ac.tz/
Hekima ni Uhuru
Ukumbi wa Nkrumah.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CKD) (kiingereza: University of Dar es Salaam) ni chuo kikuu cha kwanza nchini Tanzania[1] chenye kauli mbinu inayosema Hekima ni Uhuru. CKD kina kampasi mbalimbali kama vile Main Kampasi, CoICT Kampasi, DUCE Kampasi, MUCE Kampasi, Zanzibar Kampasi, SJMC Kampasi na Mbeya Kampasi. Hizi Kampasi zipo mahali mbalimbali. Main Kampasi, CoICT Kampasi, DUCE Kampasi na SJMC Kampasi zinapatikana jijini Dar es Salaam. MUCE Kampasi inapatikana mkoa wa Iringa. Zanzibar Kampasi inapatikana Zanzibar. Mbeya Kampasi inapatikana jijini Mbeya.

Historia yake

[hariri | hariri chanzo]
  • Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilianzishwa mnamo mwaka 1961 kama Ndaki cha Chuo Kikuu cha London (kiingereza: College of the University of London) kikiwa na Kitivo cha Sheria.[2]
  • Mnamo mwaka 1963 kilibadilisha jina na kuitwa Ndaki cha Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki (kiingereza: Constituent College of the University of East Africa) kikiwa na Shule ya Udaktari. Mnamo mwaka 1968 hii shule ilibadilishwa kuwa Kitivo cha Udaktari cha Ndaki ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kiingereza: Faculty of Medicine of the University College of Dar es Salaam).[2]
  • Mnamo Agosti 1970 chuo hiki kilitangazwa kama chuo kikuu cha kitaifa kupitia kifungu cha sheria namba 12 cha mwaka 1970 cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kikiwa na kitivo kiitwacho Kitivo cha Udaktari cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(kiingereza: Faculty of Medicine of the University of Dar es Salaam).[2]
  • Mnamo Julai 1991 Kitivo cha Udaktari cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilitangazwa kama Ndaki ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiitwacho Ndaki ya Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya Muhimbili (Kiingereza: Muhimbili University College of Health Sciences). Kulingana na kifungu cha sheria namba 7 cha mwaka 2005 cha vyuo vikuu, mnamo mwaka 2007 ndaki hii ya masuala ya Afya ilifanywa kuwa Chuo Kikuu kinachojitengemea kilichoitwa Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) kwa lugha ya kiingereza.[2]
  • Mnamo mwaka 1996, Taasisi ya Ardhi ilibadilishwa kwa Ndaki ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam itwayo University College of Lands and Architectural Studies (UCLAS) kwa lugha ya kiingereza. Kulingana na kifungu cha sheria namba 7 cha mwaka 2005 cha vyuo vikuu, mnamo mwaka 2007 ndaki hii ya masuala ya Ardhi ilifanywa kuwa Chuo Kikuu kinachojitengemea kilichoitwa Chuo Kikuu cha Ardhi (kiingereza: University of Ardhi, ARU) badala ya UCLAS.[2]
  • Baada ya miaka kadhaa kupita, chuo hiki kilifanikiwa kuanzisha vitivo, ndaki na taasisi mbalimbali. Baadhi za ndaki hizo zinajitegemea kama vyuo vikuu (MUHAS na ARU).[2]

Kiwango cha Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 2019, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilitambuliwa kama chuo kikuu bora zaidi nchini Tanzania, hapo juu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo mjini Morogoro.[3] UDSM kilitambuliwa kama chuo cha sitini na tisa kwa ubora zaidi wa elimu kwa Afrika.[4] Kinatambulika kama chuo cha 1885 kwa ubora wa kitaaluma duniani.[5]

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinatoa programu kadhaa za shahada ya kwanza, kama vile: akiolojia, usanifu majengo, biolojia, biashara, kemia, elimu ya mawasiliano, elimu ya komputa, masomo ya maendeleo, uchumi, elimu, uhandisi na elimu ya hali ya mazingira.[6] Chuo kinatoa programu kadhaa za shahada za Uzamili na Uzamivu, kama vile: elimu ya usimamizi wa fedha, sanaa, jiografia, sheria, isimu ya lugha, fasihi, uongozi, hisabati, utabibu, muziki, lishe, fizikia, sayansi ya mimea, elimu ya siasa, saikolojia, na sanaa za maonyesho.[7]

Maisha ya Chuo Kikuu

[hariri | hariri chanzo]

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kina maeneo matano mjini na karibu na mji wa Dar es Salaam. Mlimani iko kilomita kumi na tatu magharibi mwa jijini.[8] Chuo Kikuu ni nyumbani kwa wanafunzi 17,098 wa shahada ya kwanza, na wanafunzi 2,552 wa shahada za uzamili na uzamivu.[9]

Watu maarufu waliohitimu Chuoni

[hariri | hariri chanzo]

Wahadhiri wanaofahamika

[hariri | hariri chanzo]
  • Molly Mahood, Profesa wa Kiingereza, 1954-1963
  • Walter Rodney, Mwanahistoria maarufu wa Guyanese, mwanaharakati wa kisiasa na msomi
  • Yashpal Tandon, Mtunga sera wa Uganda, mwanaharakati wa kisiasa, profesa, mwandishi na wasomi wa umma
  1. "Register of Universities" (PDF). Tanzania Commission for Universities. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-09-24. Iliwekwa mnamo 15 Julai 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 "Background". Iliwekwa mnamo 2020-07-25.
  3. "URAP - University Ranking by Academic Performance". www.urapcenter.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-25. Iliwekwa mnamo 2019-07-28.
  4. "URAP - University Ranking by Academic Performance". www.urapcenter.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-25. Iliwekwa mnamo 2019-07-28.
  5. "URAP - University Ranking by Academic Performance". www.urapcenter.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-25. Iliwekwa mnamo 2019-07-28.
  6. "University of Dar es Salaam-Programme". www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2019-07-28.
  7. "University of Dar es Salaam-Programme". www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2019-07-28.
  8. "University of Dar es Salaam", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-07-20, iliwekwa mnamo 2019-07-28
  9. "University of Dar es Salaam", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-07-20, iliwekwa mnamo 2019-07-28

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/Chuo_Kikuu_cha_Dar_es_Salaam

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy