Dknob
Dknob | |
---|---|
Dknob wakati wa mahojiano na Mkasi TV, East Africa TV.
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Innocent Cornel Sahani |
Pia anajulikana kama | Mfalme wa mitaani Kitaani Most Wanted Ghuughaa! |
Amezaliwa | 12 Februari 1980 |
Asili yake | Dar es Salaam, Tanzania |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Mwimbaji Rapa |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 1998-hadi leo |
Studio | Mwamba Productions Bongo Records Mj Records Mid Man Records Mitaani Most Wanted Mwanalizombe Studios |
Ame/Wameshirikiana na | Benjamin Mez B K Bazili Ray C Squeezer Q Jay Mwasiti Hemed |
Tovuti | Tovuti rasmi |
Innocent Cornel Sahani (amezaliwa tar. 12 Februari 1980) ni msanii wa hip hop na Bongo Flava kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jia lake la kisanii kama "Dknob". Dknob ametoa nyimbo nyingi tu zenye kuwika sana katika Afrika ya Mashariki. Nyimbo hizo ni kama vile, Elimu Mitaani.com, Sauti ya Gharama, Ingewezekana, Kitu Gani, Mr. Sahani, Bora Tumeachana, na Nishike Mkono ambayo kaimba na Mwasiti.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Dknob alizaliwa mnamo tarehe 12 Februari ya mwaka 1980, katika mkoa wa Tabora, Tanzania. Amenza kupata elimu yake ya msingi katika shule ya Mazoezi Ligula Mtwara na kuja kumalizia katika shule ya msingi ya Kipawa iliyopo Dar es Salaam. Baada ya kumaliza elimu ya msingi, baadaye akawa anaendelea na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari ya Pugu kwa kidato cha kwanza mpaka cha nne na baadaye kidato cha tano na sita akamalizia katika shule ya sekondari ya Jitegemee ya jiji Dare es Salaam.[1]
Shughuri za muziki
[hariri | hariri chanzo]Dknob alianza rasmi shughuli za muziki kunako mwaka wa 1998, ni baada ya kuvutiwa sana na albamu ya marehemu Tupac na Big Small au Notorious Big. Ilipofika mwaka wa 2000, Dknob alirekodi nyimbo ya Kibongo Stance ambayo pia ilishirikisha baadhi ya wasanii mbalimbali akiwemo G-Pozz, Pig Black, Dknob mwenywe na wengine kibao.
Mnamo mwaka wa 2001, Dknob akabahatika kurekodi nyimbo yake ya kwanza akiwa kama msanii binafsi na nyimbo ilikwenda kwa jina la "usiniache" ambayo pia alimshirikisha Mez B na ilitayarishwa na matayarishaji mashuhuri Bw. Miikka Mwamba. Kurekodiwa kwa nyimbo ya usiniache, ikawa kama ndiyo mwanzo wa Dknob kupata mafanikio na akabahatika kukutana na Ruge Mutahaba, ambaye pia ni mkurugenzi wa Smooth Vibe Project, ambayo iliweka nyimbo ya Dknob katika compilesheni za Bongo Hottest (mkusanyiko wa nyimbo kali za Bongo Flava).
Mwaka 2003, Dknob akatoa single ya elimumitaani.com ambayo ilifanya vizuri zaidi na kuweza hata kumleta umaarufu katika medani ya muziki wa kizazi kipya. Na kibao hiko cha elimumitaani, nacho kilitayarishwa na mtayarishaji mashuhuri wa muziki Bw. Miikka Mwamba na ndiyo ikawa mara yake ya mwisho kwa Miikka kumtengenezea Dknob nyimbo kwa mwaka wa 2003 na 2004 Miikka akarudi kwao nchini Finland.
Baada ya hapo, Dknob akakutana Dj Steve B wa kituo cha radio cha Clouds FM na akawa kama kiongozi wake na hata kumdhamini katika kukamilisha albamu ya Dknob na kumfanyia promosheni za nguvu. Akiwa na meneja Stveve B, Dknob akafanikiwa kurekodi nyimbo ya Sauti ya Gharama akiwa amemshirikisha tena mwanamuziki Mez B na nyimbo ilitengenezwa na mtayarishaji maarufu Bw. P Funk Majani .
Mwaka wa 2005, Dknob akafanikiwa kutoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Elimumitaani.com ikiwa chini yake mwenyewe Dknob akiwa pamoja na Steve B na albamu ikasambazwa na FKW Promoters. Mnamo tarehe 4 Septemba ya mwaka wa 2006, Dknob akataoa single yake ya "ingewezeakana" akiwa amemshirikisha Ray C na Squeezer na single ikaingia katika albamu ya nyimbo mchanganyiko ya Pamoja Ndani ya Game (mchanganyiko wa nyimbo kali za Bongo Flava).
Katika mwaka huo huo wa 2006, Miikka akawa amerudi Bongo na akaanza mpango wa kutengeneza albamu ya Dknob ya "Bomoa Mipango". Mnamo tarehe 20 Aprili ya mwaka wa 2007, Dknob akaachia single yake ya "Kitu Gani" ambayo ilimshirikisha msanii machachali wa Bongo Flava Bw. Q Jay na ilivyofika tarehe 20 Agosti ya mwaka wa 2007, akatoa video ya nyimbo hiyo na kazi hiyo ilifanywa na kampuni ya kupigia video ya Visual Lab ya Dar es Salaam, Tanzania. Ifikapo tarehe 1 Julai ya mwaka wa 2008, Dknob atatoa albamu yake ya pili itakayo kwenda kwa jina la “Bomoa Mipango” na single ya kutambulisha albamu hiyo itakwenda kwa jina la “Dear Mtoto”, ambayo pia inategemewa kutoka mnamo tar. 25 Julai ya mwaka wa 2008. Katika albamu hiyo, pia kuna nyimbo ya ziada ambayo inaitwa Badamn akiwa amemshirikisha msanii Cannibal wa kutoka nchini Kenya.
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tar. 29 Septemba ya mwaka wa 2008, Dknob amemuoa Bi. Anitha Ramadhani (amezaliwa 9 Septemba 1983). Kwa pamoja wana mtoto mmoja ambaye alizaliwa kabla ya ndoa aitwaye Vivican, aliyezaliwa mnamo tar. 18 Agosti ya mwaka wa 2006. Vilevile Dknob ni mtu wa mitungi tangu yungali bwana mdogo, lakini mtitungi yake imefikia kikomo ilivyofika tar. 8 Januari ya mwaka wa 2009, pale alipowekewa sumu kwenye pombe akiwa klabu, hapo ndipo ikawa mwanzo na mwisho wa yeye kunywa pombe. Kwa sasa anaishi yeye na familia yake iliyopo huko Kiwalani, jijini Dar es Salaam.
Muziki
[hariri | hariri chanzo]Albamu zake
[hariri | hariri chanzo]- Elimu Mitaani.com (2005)
- Bomoa Mipango (2008)
Single zake
[hariri | hariri chanzo]- Kitu Gani (2007)
- Sauti ya Gharama (2004)
- Elimu Mitaani.com (2003)
- Ingewezekana (2006)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuri rasmi ya Dknob Ilihifadhiwa 18 Desemba 2014 kwenye Wayback Machine. (Kiingereza)
- Maelezo kuhusu Dknob Ilihifadhiwa 14 Julai 2007 kwenye Wayback Machine. katika Mwamba Records
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dknob kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |