Content-Length: 125363 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/Farasi_(kundinyota)

Farasi (kundinyota) - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Farasi (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa habari kuhusu mnyama angalia Farasi

Nyota za kundinyota Farasi (Pegasus) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Farasi (Pegasus), jinsi inavyoonekana kwenye nusutufe ya kaskazini
Pegasus kwenye mozaiki ya Kiroma huko Cordoba, Hispania


Farasi (Pegasus kwa Kilatini na Kiingereza) [1] ni jina la kundinyota kubwa kwenye nusutufe ya kaskazini ya Dunia.

Mahali pake

Farasi linapakana na makundinyota jirani ya Mara ( Andromeda), Mjusi ( Lacerta), Dajaja ( Cygnus), Mbweha (Vulpecula), Dalufnin (Delphinus), Kifarasi (Equuleus), Dalu (Aquarius), Hutu ( Pisces)

Jina

Jina la Farasi linatokana na Kiarabu الفرس al-faras ambalo ni umbo la jina asilia la Kigiriki Ίππος hippos yaani farasi. Baadaye ilikuwa Πήγασος au Pegasus kwa tahajia ya Kilatini. Wagiriki wa Kale walitumia jina hili kwa kutaja farasi mwenye mabawa katika mitholojia yao.

Pegasus - Farasi ni kati ya makundinyota yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK. Lipo pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia kwa jina la Pegasus. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni 'Peg'. [2]

Nyota

Nyota tatu za Alfa, Beta na Gamma Pegasi pamoja na Alpheratz (Alfa Andromedae) zinafanya pembenne.

Nyota angavu zaidi ni au Epsilon Pegasi au Enif (ar. أنف anif kwa maana « pua ») yenye mwangaza unaoonekana wa mag 2.38[3]. Ni nyotajitu yenye umbali wa miakanuru 670 kutoka Duniani. [4]

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miaka nuru)
Aina ya spektra
ε Epsilon 8 Anufu ya Farasi (Enif) mag 2,39 673 K2 Ib
β Beta 53 Scheat mag 2,4 - 3,0 199 M222 II-III
α Alfa 54 Marikabu (Markab) mag 2,49 140 B9.5 III
γ Gamma 88 Algenib mag 2,80 - 2,86 333 B2 IV
η Eta 44 Matar mag 2,93 215 G2 II-III
ζ Dzeta 42 Homam mag 3,41 209 B8.5 V
μ Mu 48 Sadalbari mag 3,51 117 M2 III
θ Theta 26 Biham mag 3,52 97 A2V
ι Iota 24 mag 3,77 38 F5 V
λ Lambda 47 mag 3,97 395 G8 II-III

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Pegasus" katika lugha ya Kilatini ni " Pegasi " na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Pegasi, nk.
  2. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Oktoba 2017
  3. Naming stars, tovuti ya UKIA, iliangaliwa Oktoba 2017
  4. ENIF (Epsilon Pegasi), tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje

Marejeo

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Pegasus” ukurasa 321 ff (online hapa kwenye archive.org)











ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/Farasi_(kundinyota)

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy