Content-Length: 53512 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/Kingwana

Kingwana - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Kingwana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kingwana ni lahaja ya Kiswahili inayozungumzwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hasa upande wa mashariki.

Chanzo cha Kingwana ni Kiswahili cha wafanyabiashara na askari kutoka pwani ya Bahari Hindi (leo nchini Tanzania) walioingia katika Katanga kwa biashara ya watumwa na pembe za ndovu wakati ya karne ya 19 kabla ya ukoloni.

Lugha ikaendelea ilipokuwa chombo cha mawasiliano katika mchanganyiko wa watu wa makabila mbalimbali walioelekea kutafuta kazi katika migodi ya Katanga na Kongo ya Mashariki.

Mfano wa Kingwana (Mwanzo wa Injili ya Yohane katika Agano Jipya)

[hariri | hariri chanzo]

HABARI NJEMA KAMA YOHANA ALIANDIKA - SURA YA KWANZA

1 Ku mwanzo Neno alikuwa, na Neno alikuwa pamuya na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. 2 Ye njo alikuwa ku mwanzo pamoya na Mungu. 3 Vitu yote zilifanywa na ye; na haiko na ye, kitu haikufanywa ile ilifanywa. 4 Ndani yake ilikuwa uzima; na uzima ilikuwa nuru ya watu. 5 Na nuru inangala ku iza; na iza haikusinda ye. 6 Mutu moya alitokea, alitumwa kutoka ku Mungu, jina yake Yohana. 7 Ye njo alikuya sahidi, asuhudie nuru, watu yote waamini kwa sababu yake. 8 Hakukuwa nuru ile, lakini alikuya asuhudie nuru. 9 Nuru ile ilikuwa nuru ya kweli, ile inapatisa nuru kila mutu ile anakuya ku ulimwengu. 10 Alikuwa ku ulimwengu, na ulimwengu ilifanywa na ye, na ulimwengu haikuyua ye.









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/Kingwana

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy