Content-Length: 89343 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/Kitabu_cha_Yoshua_bin_Sira

Kitabu cha Yoshua bin Sira - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Kitabu cha Yoshua bin Sira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kitabu cha Yoshua bin Sira ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Mwandishi alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyetunga kitabu chake kwa Kiebrania mnamo miaka 196 KK - 175 KK huko Aleksandria (Misri).

Halafu mjukuu wake alikitafsiri kwa Kigiriki akitanguliza dibaji. Wakatoliki na Waorthodoksi wanakubali kama Neno la Mungu tafsiri hiyo, si maandiko asili.

Ingawa kitabu hakionyeshi mara moja mpangilio mzuri, kwa kugusagusa mambo mbalimbali, mafundisho yake makuu ni kwamba Hekima, ambayo ni mamoja na Torati, ni sifa maalumu ya Wayahudi; hao tu wanaweza kumfikia Mungu.

Kitabu kinatoa hasa maadili yanayofanana na yale ya Kitabu cha Mithali.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.


Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Yoshua bin Sira kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/Kitabu_cha_Yoshua_bin_Sira

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy