Content-Length: 51987 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/TUKI

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka TUKI)

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) ni idara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Taasisi hii ni miongoni mwa taasisi kongwe za lugha nchini Tanzania. Madhumuni yake yakiwa ni kusimamia usanifishaji na maendeleo ya lugha ya Kiswahili. Hadi mnamo mwaka 2009 taasisi hii ilijulikana zaidi kwa jina la TUKI au "Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili".

Historia yake

Ilianzishwa mnamo mwaka 1930 kama Inter-territorial Language (Swahili) committee ya Nchi za Afrika ya Mashariki, baadaye ikaitwa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Mnamo mwaka 1964 kamati ilifanywa kuwa Sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaamu. Baadaye ikaitwa Chuo cha Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili. Tangu 1970 kimepewa jina la Taasisi ya Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili. Mwaka 2009, TUKI iliungana na iliyokuwa Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuunda Taasisi kubwa zaidi inayoitwa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili - TATAKI

Majukumu

Mwanzoni, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ni taasisi ya utafiti ilipewa jukumu la kutafiti nyanja zote za lugha ya Kiswahili, fasihi na utamaduni, na kuchapisha matokeo ya utafiti huo. Hivyo pamoja na BAKITA (Baraza la Kiswahili Tanzania) TUKI ndiye mlinzi wa usanifu wa lugha ya Kiswahili katika Tanzania. Baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili, sasa TATAKI inafundisha Isimu, Fasihi na Historia ya Lugha ya Kiswahili katika Shahada za Awali, Mahiri na Uzamivu.

Kazi yake

Kutafiti na kuchapisha matokeo ya utafiti katika nyanja mbalimbali za Lugha, Isimu na Fasihi ya Kiswahili, TATAKI inasimamia Tafsiri na Ukalimani. Inafundisha Kiswahili kama lugha ya pili hasa kwa wageni kutoka nje ya ulimwengu wa Waswahili na kuendeleza utungaji wa Kamusi mbalimbali zinazohusiana na Kiswahili. Kati ya kamusi hizi ni

TUKI imehariri toleo la Kiswahili la "Historia Kuu ya Afrika" iliyotungwa na kamati ya wataalamu ya UNESCO.

Viungo vya nje









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/TUKI

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy