Content-Length: 112568 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/Ubao

Ubao - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Ubao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ubao ulioandaliwa kuwa kuni
Mti huu unaonyesha miviringo 27 ya miaka yake ya kukua pamoja na safu ya nje ya ubao laini pamoja na kiini cha katikati

Ubao ni dutu inayofanya gogo na matawi ya mti. Ina matumizi muhimu kwa ujenzi na vifaa pia kama kuni kwa moto.

Ubao hutengenezwa na mti wakati wa kukua. Ubao laini katika ganda la nje la gogo hupitisha maji na lishe kutoka mizizi kwenda kwenye matawi na majani. Kila mwaka ganda jipya linaongezeka nje na ganda la ndani huwa imara na kupoteza uwezo wa kupitisha maji. Mabadiliko haya ya kila mwaka huonekana katika miviringo ya ubao ndani ya mti.

Ubao umetumiwa na wanadamu tangu miaka maelfu. Mwanzoni ilitumiwa kama kuni na fimbo ya silaha. Baadaye watu walijifunza kuchonga ubao kwa matumizi mbalimbali kama vile ujenzi, vifaa, sanaa kama uchongaji, karatasi na mengi mengine.

Ubao huwa na faida ni imara lakini si vigumu ya kukata na kuchonga, tena ni nyepesi. Pia unapatikana kwa wingi angalau katika maeneo ambako miti inakua.

Tazama pia

Wikimedia Commons ina media kuhusu:








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/Ubao

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy