Content-Length: 76704 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/Wandamba

Wandamba - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Wandamba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wandamba ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi kiasili katika mkoa wa Morogoro (Wilaya ya Malinyi na Wilaya ya Mlimba), hasa katika mji wa Ifakara pamoja na vijiji vya Mofu, Ruipa, Mbingu, Mngeta, Merera, Chita, Ngombo, Mlimba na Biro. Wa wanapatikana pia katika wilaya ya Ulanga katika kijiji cha Malinyi.

Lugha yao ni Kindamba (wenyewe wanatamka Chindamba), ambacho kinafanana sana na Kimbunga (69%) na Kipogoro (56%), lugha ya Wapogoro wanaoishi katika wilaya ya Ulanga. Hiyo inathibitisha kwamba asili yao ni moja.

Mwaka 1987 walikadiriwa kuwa 79,000, mbali ya Wambunga waliokuwa 29,000.

Asili ya Wandamba wengi ni kuwa wapole, wakarimu, si wachoyo wala bahiri. Pia Wandamba huwa na mapenzi ya ukweli, akipenda amependa haswahaswa.

Upande wa dini wengi wao ni wafuasi wa Yesu Kristo katika Kanisa Katoliki.

Wandamba ni maarufu kwa kupenda kula wali na samaki hata mwaka mzima kutokana na kilimo cha mpunga na uvuvi wa samaki. Samaki wanaopendwa sana na Wandamba ni Kitoga. Mapishi ya wali kwa samaki hupikwa bila kutumia mafuta wala nazi.

Ngoma ya asili ya Wandamba inaitwa Lindenda. Ngoma hiyo huchezwa wakati wa furaha katika mfumo wa duara.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wandamba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/Wandamba

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy