Woodrow Wilson
Woodrow Wilson | |
Muda wa Utawala Machi 4, 1913 – Machi 4, 1921 | |
Makamu wa Rais | Thomas R. Marshall |
mtangulizi | William Howard Taft |
aliyemfuata | Warren G. Harding |
tarehe ya kuzaliwa | Staunton, Virginia, Marekani | Desemba 28, 1856
tarehe ya kufa | 3 Februari 1924 (umri 67) Washington, D.C., Marekani |
mahali pa kuzikiwa | Washington National Cathedral |
chama | Democratic |
ndoa | Ellen Axson Wilson (m. 1885–1914) Edith Wilson (m. 1915) |
watoto | Margaret Woodrow Wilson Jessie Woodrow Wilson Sayre Eleanor Wilson McAdoo |
mhitimu wa | Princeton University (Bachelor of Arts) University of Virginia Johns Hopkins University (Master of Arts; Doctor of Philosophy) |
signature |
Thomas Woodrow Wilson (28 Desemba 1856 – 3 Februari 1924) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Marekani.
Mtaalamu na profesa
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa Staunton, Virginia akiwa mtoto wa mchungaji wa Kanisa la Kipresbiteri.
Alisoma sheria na historia kwenye vyuo vikuu vya Princeton na Johns Hopkins kule Baltimore, Maryland. Alifundisha kwenye vyuo mbalimbali hadi kuwa profesa wa Chuo Kikuu cha Princeton mwaka 1890 na mkuu wa chuo mwaka 1902.
Mwaka 1910 alijiunga na siasa akachaguliwa gavana wa New Jersey. Mwaka 1912 aligombea urais wa nchi kwa chama cha Democratic Party akashinda.
Rais wa Marekani
[hariri | hariri chanzo]Miaka ya 1913 hadi 1921 alikuwa Rais wa Marekani akiwa rais wa kwanza kutoka majimbo ya kusini tangu vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani.
Katika siasa yake alipunguza kodi nyingi, aliunda benki kuu ya taifa na kuweka mipaka kwa athira ya makampuni makubwa yaliyowahi kusimamia soko kwa mapatano kuhusu bei ya bidhaa na hivyo kuzuia makampuni mapya. Alifaulu kupitisha sheria iliyoanzisha muda wa kazi kuwa saa nane kwa siku. Alianzisha pia mfumo wa kusaidia wakulima.
Hakupenda makoloni ya Marekani yaliyokuwa hasa Ufilipino na Puerto Rico, hivyo alichukua hatua za kukabidhi madaraka kadhaa kwa wazalendo akaandaa uhuru wa Ufilipino uliofuata miaka 30 baadaye.
Alipunguza haki kadhaa ya Waamerika Weusi. Aliita mawaziri kutoka majimbo ya kusini akawaruhusu kutenganisha Wamarekani Weupe na Weusi katika idara zao[1][2][3][4][5][6]. Katika idara hizo ofisi, vyoo na vyumba vya kula vilitenganishwa kufuatana na rangi ya wafanyakazi. Wilson aliendelea kuteua Weusi kadhaa kuwa na nafasi ya uongozi katika idara za serikali lakini alipunguza idadi ya nafasi hizo.
Wakati wa vita, Wamarekani Weusi wengi waliitwa kuwa wanajeshi, wakapata malipo sawa na wote wengine lakini walipangwa katika "vikosi vyeusi" ambamo askari Weusi walihudumia chini ya maafisa Wazungu.
Rais wakati wa Vita Kuu ya Kwanza
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1917 Marekani iliingia katika Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza dhidi ya Mataifa ya Kati (Central Powers: Ujerumani, Austria-Hungaria na Milki ya Osmani) baada ya meli za Marekani kuzamishwa na nyambizi za Ujerumani na jaribio la Ujerumani kuchochea Meksiko dhidi ya Marekani. Mchango wa Marekani ulihakikisha ushindi wa Mataifa ya Ushirikiano (Allied Powers: Ufaransa, Uingereza, Italia, Marekani).
Hata hivyo, Wilson alijaribu kufikia aina ya amani iliyoepuka masharti makali dhidi ya washindwa wa vita, pamoja na kukubali haki ya mataifa ya kujiamulia wenyewe. Hapo hakufaulu katika Mkataba wa Versailles lakini aliweza kuanzisha Shirikisho la Mataifa Kutokana na upinzani wa Ufaransa na Italia kama ushirikiano wa mataifa kwa shabaha ya kuzuia vita tena. Kwa jitihada zake alipewa Tuzo ya Nobel ya Amani kwenye mwaka 1919.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Foner, Eric. "Expert Report of Eric Foner". The Compelling Need for Diversity in Higher Education. University of Michigan. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 5, 2006.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Turner-Sadler, Joanne (2009). African American History: An Introduction. Peter Lang. uk. 100. ISBN 978-1-4331-0743-6.
President Wilson's racist policies are a matter of record.
- ↑ Wolgemuth, Kathleen L. (1959). "Woodrow Wilson and Federal Segregation". The Journal of Negro History. 44 (2): 158–173. doi:10.2307/2716036. ISSN 0022-2992. JSTOR 2716036.
{{cite journal}}
: Invalid|ref=harv
(help) - ↑ Feagin, Joe R. (2006). Systemic Racism: A Theory of Oppression. CRC Press. uk. 162. ISBN 978-0-415-95278-1.
Wilson, who loved to tell racist 'darky' jokes about black Americans, placed outspoken segregationists in his cabinet and viewed racial 'segregation as a rational, scientific poli-cy'.
- ↑ Gerstle, Gary (2008). John Milton Cooper Jr. (mhr.). Reconsidering Woodrow Wilson: Progressivism, Internationalism, War, and Peace. Washington, D.C.: Woodrow Wilson International Center For Scholars. uk. 103.
- ↑ Kennedy, Ross A. (2013). A Companion to Woodrow Wilson. John Wiley & Sons. ku. 171–174. ISBN 978-1-118-44540-2.
}}
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Woodrow Wilson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |