Content-Length: 114912 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/Algorithm

Algorithm - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Algorithm

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uhaishaji wa algoriti ya QuickSort ikipanga safu zilizowekwa kiholela.

Algorithm au (algorithimu au algoriti kwa Kiswahili kutoka Kiingereza: Algorithm) ni utaratibu wa hatua-kwa-hatua wa kutatua tatizo haswa tatizo la kihesabu [1], yaani ni kanuni au maelekezo ya hesabu ambayo kama yakifuatwa na kompyuta yanaweza yakapata jibu la tatizo [2], hivyo ni njia ya kutatua kwa hatua chache magumu katika hisabati. Njia hiyo inaweza kufanya hesabu na usindikaji wa data.

Algoriti inaweza kutumika kwenye kazi rahisi kama kupanga orodha ya namba au kwenye majukumu tata kama kutoa mapendekezo ya mahudhui kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Algoriti hufanya kazi kwa kufata maelekezo au kanuni za kutekeleza jukumu au kutatua tatizo, zinawezwa andikwa kwa kutumia lugha ya asili, lugha ya programu, msimbo bandia, na chati mtiririiko.

Lugha ya asili huwa haitumiki sana kuandika algoriti kwasababu ya utata wake, lugha ya programu hutumika zaidi kuandika algoriti ambayo huchakatwa na kompyuta [3].

Jina linatokana na mwanahisabati wa Uajemi al-Khwarizmi aliyetoa maelekezo ya kwanza ya namna hiyo katika karne ya 9 BK.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Algorithm kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Definition of ALGORITHM". www.merriam-webster.com (kwa Kiingereza). 2023-12-21. Iliwekwa mnamo 2024-01-04.
  2. https://dictionary.cambridge.org/dictionary/english/algorithm
  3. "What is an algorithm? | TechTarget". WhatIs (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-04.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/Algorithm

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy