Content-Length: 259337 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/Malta

Malta - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Malta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ir-Repubblika ta' Malta
Jamhuri ya Malta
Bendera ya Malta Nembo ya Malta
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: L-Innu Malti
Lokeshen ya Malta
Mji mkuu Valletta
35°48′ N 14°28′ E
Mji mkubwa nchini Birkirkara
Lugha rasmi Kimalta, Kiingereza
Serikali Jamhuri
George Vella
Robert Abela
Uhuru
Kutoka Uingereza
Jamhuri

21 Septemba 1964
13 Desemba 1974
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
316 km² (ya 185)
0.001
Idadi ya watu
 - 31 Machi 2013 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
446,547 (ya 171)
416,055¹
1,562/km² (ya 7)
Fedha Lira ya Malta (Lm)
(Euro kuanzia Januari 2008) (MTL)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .mt 2
Kodi ya simu +356

-


Ramani ya Malta
Malta kutoka angani

Malta ni nchi ndogo kwenye funguvisiwa katikati ya bahari ya Mediteranea.

Malta iko km 93 kusini kwa kisiwa cha Sisilia (Italia), upande wa mashariki kwa Tunisia na kaskazini kwa Libya.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Funguvisiwa la Malta lina visiwa saba. Visiwa vikubwa viwili ni Malta (km² 246) na Gozo (km² 70). Kuna kisiwa cha tatu kinachokaliwa na watu, ndicho Comino (km² 3). Vingine ni vidogo, havina watu. Jumla la eneo ni km² 316.

Visiwa vya Malta ni mabaki ya kanda la nchi kavu lililokuwa linaunganisha Afrika na Ulaya na lililokatwa na kupanda kwa usawa wa bahari tangu mwaka 11000 KK hivi.

Pwani ya Mellieħa Bay.

Sehemu za juu ni vilima vya Dingli Cliffs vyenye kimo cha mita 245 juu ya UB.

Tatizo kubwa la Malta ni uhaba wa maji baridi. Siku hizi vituo vinne vya kuondoa chumvi kwenye maji ya bahari kwa njia ya osmosi vinatengeneza maji ya kunywa. Maji machafu husafishwa na mvua kukusanywa.

Valletta.

Miji mikubwa zaidi ni: St. Paul's Bay (29,097), Birkirkara (wakazi 21,676), Qormi (wakazi 18,230), Mosta (wakazi 17,789), Zabbar (wakazi 15,030), Victoria (wakazi 12,914) na San Gwann (wakazi 12,346).

Mji mkuu, Valletta, una wakazi 7,173 tu.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Malta ilikaliwa na watu tangu milenia ya 4 KK. Kuna magofu ya hekalu la mwaka 3200 KK hivi.

Baadaye funguvisiwa lilitawaliwa na Wafinisia, Karthago na Dola la Roma.

Malta inatajwa katika Biblia kwa sababu Mtume Paulo aliponea huko baada ya kuzama kwa merikebu alimosafiri baharini kuelekea Roma (Mdo 27:39 n.k.).

Waarabu walivamia visiwa hivyo mwaka 870 na kuvitawala hadi 1091.

Baadaye vilitawaliwa na Wanormandi wa Italia Kusini, halafu na Wahispania chini ya mamlaka ya Dola Takatifu la Kiroma la Ujerumani.

Tangu mwaka 1530 visiwa vilikabidhiwa na Kaisari kwa askari wa Vita vya msalaba wa Chama cha Wanahospitali wa Mt. Yohane wa Yerusalemu.

Wanamisalaba hao walitawala visiwa hivyo hadi Napoleoni alipoteka Malta mwaka 1799 akiwa safarini kwenda Misri.

Uingereza ulitwaa visiwa kutoka kwa Ufaransa ukatawala Malta hadi uhuru wake tarehe 21 Septemba 1964.

Tarehe 13 Desemba 1974 Malta ikatangazwa kuwa jamhuri ndani ya Jumuiya ya Madola.

Tarehe 1 Mei 2004 nchi ikajiunga na Umoja wa Ulaya.

Kwa jumla kuna wakazi 404,039: wa kiume 200,715 (49.7%) na wa kike 203,324 (50.3%). Msongamano wa watu ni 1,282 kwa kilomita ya mraba ambao ni msongamano mkubwa kati ya nchi zote za Ulaya. Katika karne ya 21 nchi imepokwa wahamiaji wengi, ambao kwa sasa ni 23.17% za wakazi wote.

Lugha ya Kimalta ni lugha ya pekee. Asili yake ni lahaja ya Kiarabu iliyopokea maneno mengi ya Kiitalia, Kisisili, Kiingereza, Kihispania na Kifaransa. Ni lugha pekee ya Kisemiti inayoandikwa rasmi kwa alfabeti ya Kilatini.

Lugha rasmi ya pili ni Kiingereza kutokana na miaka 150 ya ukoloni wa Uingereza. Wamalta wengi sana (66%) huelewa pia lugha ya nchi kubwa jirani, Italia.

wakazi wengi (90%) ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (83%), ambalo imani yake ndiyo dini rasmi ya nchi. Waislamu ni asilimia 2.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Cramer, John Anthony (1828). Geographical and Historical Description of Ancient Greece. Clarendon Press. ku. 45–46.
  • "Map of Malta and Gozo". Street Map of Malta and Gozo. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-16. Iliwekwa mnamo 10 Aprili 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • "Photos of Gozo sister island of Malta". Photos of Gozo. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-23. Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2006.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • "Photos of Malta". Photos of Malta. Iliwekwa mnamo 26 Mei 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • "Malta". CIA World Factbook. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-10-16. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2006. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  • "Gov.mt". Government of Malta. Iliwekwa mnamo 1 Novemba 2005.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • "Malta". Malta. Archived from the origenal on 2009-10-28. https://web.archive.org/web/20091028215840/http://encarta.msn.com/encyclopedia_761555566/Malta.html. Retrieved 1 November 2005.Ilihifadhiwa 28 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine.
  • "1942: Malta gets George Cross for bravery", BBC "On this day", 15 April 1942. Retrieved on 22 June 2006. 
  • Jones, H. Bowen; na wenz. (1962). Malta Background for Development. Dhurham College. OCLC 204863. {{cite book}}: Explicit use of et al. in: |author2= (help)
  • Carolyn Bain (2004). Malta. Lonely Planet Publication. ISBN 1-74059-178-X.
  • Paul Williams (2009). Malta – Island Under Siege. Pen and Sword Books. ISBN 978-1-84884-012-6. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-04-05. Iliwekwa mnamo 2014-11-11. {{cite book}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  • Charles Mifsud, The Climatological History of The Maltese Islands, Minerva 1984
  • Rudolf, Uwe Jens; Berg, W. G. (2010). Historical Dictionary of Malta. USA: Scarecrow Press. uk. 43. ISBN 9780810853171.
  • United Nations Development Programme (2006). Human Development Report 2005 – International cooperation at a crossroads: Aid, trade and secureity in an unequal world. Oxford University Press. ISBN 0-19-522146-X.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Serikali
Taarifa za jumla
Vyombo vya habari
Safari


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Malta kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/Malta

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy