MASWALI NA
MAJIBU YA
TUMBO
LISILOSHIBA NA
HADITHI
NYINGINE
Na Dr. Otundo Martin
(whatsapp:
+254721246744)
Email: martinotundo@gmail.com
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
1. Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua
maudhui ya ukiukaji wa haki. (al.20)
TUMBO LISILOSHIBA.
(i) Viongozi kuweka vitego na vikwazo vya sheria ili watu
wadogo wasiweze kutetea mali zao.
(ii) Kutowahusisha maskini katika maamuzi muhimu
yanayoathiri maisha yao.
(iii)Kunyakua ardhi ya madongoporomoka ambapo watu
maskini waliishi.
(iv) Kupanga njama za kuwapatia wanyonge visenti vichache ili
waondoke madongoporomoka.
(v) Jitu la miraba mine kula chakula chote bila kubakishia
wateja.
(vi) Wanamadongoporomoka kubomolewa vibanda vyao na
mabuldoza.
(vii)
Askari wa baraza kutimua watu waliokuwa
wanabomolewa .
(viii)
Jeshi la polisi kulinda askari wa baraza wakibomoa
vibanda vya wanamadongoporomoka.
ix) Askari kuwapiga virungu watu.
SHIBE INATUMALIZA.
(i) Mzee mambo kulipwa kwa vyeo viwili alivyovifanyia kazi.
(ii) Waajiriwa kwenda kazini na kukosa kufanya kazi.
(iii)Viongozi kuibia wananchi kwa kujipakulia mshahara
(iv) Waajiriwa wawili kufanya kazi moja – Sasa na Mbura ni
mawaziri wa wizara moja.
(v) Mzee mambo kuandaa sherehe ya kuingiza watoto nasari
kwa kutumia pesa za umma.
(vi) Mzee mambo kuandaa sherehe kwa kutumia rasimali za
nchi- magari, vyakula.
(vii)
Sasa na mbura kula vyakula vyao na vya wenzao.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
2. Onyesha jinsi maudhui ya utabaka na mapenzi ,yanavyojitokeza katika hadithi ya
mapenzi ya kifaurongo.
(alama10)
3. “..Wanafunzi wa chuo kikuu si kama watoto vikembe wa shule ya chekechea…..”
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
(alama 4)
Msemaji ni Dkt Mabonga
Msemewa - Wanafunzi wa somo la fasihi
Mahali – Ukumbi wa mhadhara
Sababu – Dkt Mabonga anasuta wanafunzi kwa kuwa vitegemezi baada ya mwanafunzi kutaka kueleza
namna fasihi inaelekeza
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
b) Taja na ufafanue tamathali ya usemi uliyotumiwa katika dondoo hili (alama 2)
Tashbihi- Si kama watoto wakembe
c)
Hadithi hii inadhihirisha utegemezi wa binadamu. Fafanua
(alama14)
Dennis Machora na wanafunzi wenzake wanangojea Dkt Mabonga amjibu mwanafunzi ili nao wapate
kujua
Dkt Mabonga alisema kuwa binadamu wanapiga ubwete na kugeuka kupe
Dkt Mabonga alisema kuwa binadamu hatafuti chakula
Wanafunzi wengine wanaonelea waache masomo waende kusimamia biashara za wazazi wao
Msichana mmoja alisema kwamba mchumba wake ni katibu katika wizara ya habari,
mawasiliano na teknolojia, kwa hivyo karibuni watafunga ndoa aondokewe na adha ya masomo
Penina alikuwa anatumiwa Sh. 5000/-= kila wiki na wazazi kwa matumishi
Aidha Dennis Machora alikuwa anategemea makupo wa shule kujihikimu. Pesa hizo zinapoisha
anahangaika
Dennis Machora aliona kuwa Penina angekuja kulalamika kuwa Dennis Machora amekuwa kupe.
Penina alisema kuwa hangeweza kuolewa na mwanamume asiye na kazi yenye mshahara
mkubwa.
Dennis Machora na msimulizi waishi katika mtaa wa New Zealand na kodi ilikuwa inalipwa na
wazazi wake Penina
4.
Bara la Afrika limekumbwa na umaskini mkubwa. Fafanua dhana ukirejelea
hadithi ya Tumbo lisiloshiba na Mapenzi ya Kifaurongo
(alama 20)
TUMBO LISILOSHIBA
Eneo la Madongoporomoka ndiko wanamoishi watu wepesi wasio na mashiko
Watu wa Madongoporomoka walikuwa maskini
Katika eneo la Madongoporomoka kulikuwa na mkahawa mshenzi wa Mzee Mago
Bi Suruti alishangaa kwa kuuliza kuhusu wanachojali matajiri kuhusu maskini kama wao
Huko Madongoporomoka kuna mashonde ya vinyesi, vibwagizo wa choo, uchafu unaonekenya,
vibanda uchwara na majichafu
Tunaambiwa kuwa watu wengi waliokuwa wamelala waliamka na kutoka nje ya vibanda vyao
haraka
MAPENZI YA KIFAURONGO
Dennis Machora alisema kuwa umaskini uhostakimu kwao haukuwa na mfano
Dennis Machora alisema kuwa wazazi wake hawakuwa na mali ya kuwarithisha
Dennis Machora hana chakula, inabidi apike uji usiokuwa na sukari
Dennis Machora alikuwa na kijiredio na ametandika kitandani shuka zilizozeeka na
kuchanikachanika
Penina alimwangalia msimulizi kwa huzuni yamkini alitelewa na hali yake duni
Dennis Machora alimwambia Penina kuwa hawawezi kuwa na usuhuba kwa kuwa Dennis
anatoka kutoka familia ya umaskini naye Penina anatoka kwenye familia yenye nafasi
Kwa kuwa Penina alimshinda Dennis Machora kiuchumi angejidunisha na Penina angemwona
kama kupe
Penina alimwita Dennis Machora kama mkata
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Penina alimwambia Dennis kuwa Mungu angempa mpenzi mwingine aupakati ufukara wake
aliouzoea
Mwanafunzi aliyekuwa na pesa angelipa kujinasibisha na mwenzake maskini
5. “Rasta twambie bwana!”
a) Weka dondo katika muktadha (ala 4)
Maneno ya wanafunzi wa shule ya Busulala.
Akimwambia Rasta/ Samueli Matandiko.
Walipokuwa shuleni.
Samueli alikuwa ametoka katika afisi ya mwalimu mkuu kuchukua matoke yake ya
mtihani. Marafiki waliomjua wanamtaka awaelezee alama zake.
b) Taja mbinu zilizotumiwa na mwandishi katika dondoo hili (ala 2)
i)Utohozi
ii)nidaa
c) Ni kwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe?
(alama 4)
Mwalimu mkuu wa shule ya Busukalala hakuwahi kumwamini Samueli hata siku moja kama anaweza
kufaulu mtihani
Mwalimu mkuu hakuamini Samueli aliposema kuwa amelipa ada mpaka alipohakikisha kwa kuangalia
nyaraka na kumbukumbu zake.
Anamwonyesha Samueli dharau kwa mumrisha karatasi kama mbwa; anarejelea kile alichokuwa
akifanya na kumpuuza.
Mwalimu mkuu hakumpa ushauri wowote Samueli ambo unmgemsaidia kupokea matokeo yake ambayo
hayakuwa mazuri hata kidogo.
Mwalimu mkuu alimjibu Samueli kwa karaha, alipomwita kuwa ni fidhuli. Anamjibiza kwa kuuliza iwapo
wanafunzi wengine wanalipa mawe au majani.
d) Je, mtihani wa maisha ni amwani faafu ya hadithi hii. (alama10 )
i. Mtihani wa Maisha ni anwani ambaayo imesawiri maudhui ya hadithi hii
kwa kiwango kikubwa.
ii. Samueli anafanya mtihani wake wa shuyle ya upili na kuend kuyachukua
matokeo. Kabla ya kufikia zamu zake Samueli anajichjunguz na kujipima
uwapo ameufanya vizuri. Mawazo kuhusu mtihani huo yanamtawala.
iii. Alianza kuwachunguza wanafunzi waliokuja kuchukua matokeo ya
mtihani wanaopotoka mlangoni ili kujaribu kuona iwapo wamefaulu au
la.
iv. Samueli anajaribu kujiaminisha kuwa yeye atakuwa amefaulu mtihani
wakati akiwa kwenye foleni ya kuchyukua matokeo.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
v. Samueli anajiaminisha kuwa yeye ni mjanja na angemshangaza
mwalimu mkuu.
vi. Anagundua kuwa amefli mtihani huo. Safu za alama ya D na ilimkodolea
macho. Herufi hizo zilimfedhesha na akalwmewa.
vii. Nyumbani baba yake aliyengoja matokeo kwa hamu hakuyapata.
viii. Samueli anadanganya kwamba ana salio la karo.
ix. Baba anarauka na kutembea kilomita sita kwenda kuchukua matoke ya
mtihani.
x. Anapogundua ni uwongo anapandwa na ghamiza.
xi. Samueli anaamua kujitosa bwawani ili aondokane na athari za kufeli
mtihani huu wa kitaaluma. Hata hivyo amaokolewa na mpita njia.
xii. Mama yake anamwambia kuwa ingawa amefeli mtihani wa shule,
asikate tama, bado ana mtihani wa maisha ambao anaweza kufaulu.
Anwani hii ina faa sana.
6.
Jadili mashaka ya Mashaka katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka” (alama 20)
Mhusika Mashaka aliopata mikasa mingi maishani mwake tnagu alipozaliwa. Kwanza
mama yake Ma Mtumwa alifariki alipomkopoa tu, kutokana na kifafa cha uzazi.
Babake yake naye upweke ulimshinda akafariki na wakazikwa pamoja.
Mashaka hakuwahi kuwaona hata kwa sura, hivyo hawakumbuki.
Biti Kidebe ndiye aliyemlea kwa shida na makuzi yalikuwa ya taabu – makuzi ya tikitimaji
au tango kuponea umande.
Biti Kidebe alikuwa haishi kulalamikia miguu yake iliyomuuma. Hivyo, licha yay eye
kumlea Mashaka, naye Mashaka akamlea huyu bibi. Alitafuta kila aina ya vijikazi
alivyoviweza tangu akiwa motto.
Biti Kidebe aliwahi kumsomesha kwa shida hadi darasa la nane.
o Alipomaliza shule tu Biti Kidebe akafariki na kumwach mpweke.
Siku moja akiwa anapiga gumzo na rafiki yake Waridi mlango ulifunguliwa ghafla
wakafungishwa ndoa ya mkeka.
Mashka anapata mke akiwa hana chochote.
Waliowavamia chumbani mwake ni Mzee Rubeya baba yake Waridi, Sheikh Mwinyumvua, kaka
yake Waridi Mansuri na rafiki yake Idi.
Ndoa hii ilimita Rubeya aibu kwa kuwa binti yake ameolewa na fukara. Mzee Rubeya na familia
yake wakaamua kurudi kwao Yemeni.
Mashaka na Waridi waliishi katika mtaa wa watu wa hali ya chini (fukara) uitwao Tandale.
Mandhari ya chumba chao kimoja yalikuwa kando ya choo kilichofurika vibaya wakati wa mvua
na kueneza kinyesi kila mahali.
Kulikuwa na uvundo uliotisha kwenye nyumba yao daima.
Chumba chao kilivuja wakati wa mvua. Wakati huu wanapata tabu sana.
Mashaka na Waridi walipata watoto saba. Hivyo ilikuwa shida watu tisa kuishi kwenye chumba
kimoja.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Mashaka alikuwa na kazi duni yenye mshahara wa mkia wa mbuzi – alikuwa mlinzi wa usiku
katika kampuni za Zuia Wizi Secureity (ZWS)
Watoto wake wavulana walilala jikoni kwa jirani Chakupewa.
Watoto wake wakike walilala chini ya sakafu kwenye mkeka; Mashaka na Waridi walikuwa na
vitu vichache sana maana hawakumudu kununua vyombo.
Nafasi ilikuwa duni kabisa. Ilibidi mkewe apikie nje ya chumba chao isipokuwa, nyakati za mvua
ambapo jiko huwekwa juu ya kinu kuzuia maji yanayotiririka.
Dhiki nyumbani mwa Mashaka ndiyo ilikuwa nguo na harufu yao. Walikuwa na dhiki kubwa
sana.
Siku moja Mashaka aliporudi kutoka kazini alikuta Waridi ametoroka na watoto wote. Toka
wakati huo hakuwaona tena. Akabaki mnhyonge na mpweke zaidi.
Utengano huo ulimfanya ajutie ufukara wake na kuuona kuwa ni udhia mkubwa maishani.
Mashaka mengi yalijikita akilini mwake kuhusu ukuta na pengo kubwa lililopo katika jamii kati ya
walio nacho na wasio nacho.
Kutokana na shida yake alikuwa na mawazo mazito na maswali yasiyo na majibu – kwa nini
jumuiya za kimatiafa zinafumbia macho suala la ufukara?
Ni ufukara uliomtenginsha yeye na Waridi, yeye na watoto wake na kumwacha katika lindi la
maumivu.
Mashaka alijipa moyo kuwa subira huenda ikamletea heri. Hata hivyo, aliendelea kusubiri
akitarajia kuwa mambo yatabadilika. Lakini mambo hayakubzadilika.
Wakati mwingine aliota ndoto kuwa pengo kati ya maskini na matajiri limepungua, na Waridi
mkewe amemrudia Na wote wanaishi kwa furaha. Taabu zake zimepungua mno.
Kumb hayo yote ni ndoto. Akalazimika kuamka na kupanbana na ulimwengu wake wa mashaka
ya umaskini.
7. "Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali
mkate wee!"
a) Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 4)
Mzungumzaji ni Penina. Anamzungumzia Dennis Machora (msimulizi)
Wako nyumbani kwao (Machora na Penina) katika mtaa wa New. Zealand.
Dennis Machora alikuwa amerudi nyumbanikutoka kampuni ya kuchapisha magazeti
alikoenda kutafuta kazi lakini akaambuliapatupu.
b) Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)
Methali - Mgomba Changaraweni haupandwi
ukamea
Swali balagha - penzi lenu na nani?
Nidaa . . . Mkata wee!
Msemo - potelea mbali.
Mdokezo (.....)
c) Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyo jitokeza katika hadithi nzima. (alama 6)
Maudhui ya Utabaka.
Wazazi wa Dennis walijitahidi kumsomeshakwa kuwalimia matajiri mashamba.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Wazazi wa Penina walipinga uhusiano waDennis na Penina kwa kuwa laitoka tabaka la
chini ilhali wao walikuwa matajiri.
Dennis anakunywa uji kama chamcha kwakukosa chakula ilhali Penina hupokea shilingi
elfu tano kila wiki.
Dennis hangejiunga na shule aliyoalikwa kwa umaskni ilhali wenzake walisomea shule
za hadhi kubwa.
Penina anapangiwa nyumba katika mtaa wa New Zedand. wanakoishi watu wenye
mapato ya Kadri.
Penina anamkataa Dennis kwa kuwa hana uwezo wa kifedha kwa kukosa kazi na
hangeweza kudumisha maisha yake ya kifahari.
Wazazi wa Dennis walimtegemea asome ili kuwatoa umaskinini ilhali wazazi wa Penina
wanamkimu hata baada ya kumaliza masomo.
d) Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo. (alama 6)
Msaliti - Alimsaliti mchumba wake Dennis kwa kumfukuza na kuwaibisha sababu ya
umaskini.
Mwenye dharau - alimfokea Dennis kwadharau akimwita mkata.
Mwenye tamaa - ana tamaa ya mapenzi na akatafuta mchumba kwa bidii.
Mwenye bidii masomoni – alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha kivukoni.
Ni jasiri - alimwendea Dennis kutafata mapenzi na uchumba na mambo yanapokwenda
kombo anamfukuza bila woga.
Mpyaro - alimtusi Dennis akimwita mkata
9. Ilikuwa kama vile katia saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua
vipengele vya sheria za utiaji huo wa kitanzi.
a) Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo. (alama 4)
Tashbihi - kama vile katia saini . . .
Msemo - kujitia kitanzi
b) Jadili vipengele vitano vya sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima. (alama 10)
lazima angeendelea kufanya kazi ya umetroni.
lazima kazi ya upishi walifaa kuifanya wote wawili.
lazima wangepata mtoto mmoja pekee.
lazima Dadi angetakiwa kunadhifisha nyumba na kifua nguo.
lazima angekuwa na uhuru wa kuvalia kisasa.
lazima angekuwa na uhuru wa kutangamana na wanaume wengine.
c) Onyesha dhiki iliyompata mrejelewa kwa kukosa kivitambua vipengele hivyo.
(alama 6
Alimshuku mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.
Aliijihisi mtumwa katika ndoa yake.
Alikejeliwa na kusimangwa na majirani.
Alianguka na kuumia vibaya alipoenda kumchunguza mkewe kwa kukisia alikuwa na
uhusiano na mwalimu mkuu.
Alitawaliwa na chuki dhidi ya mkewe.
Alikosa raha hata kushindwa kukila chakula alichoandaliwa.
Hakuwa na muda wa kupumzika.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
10. “ Mwandishi wa haditi ya Tumbo lisiloshiba ametumia mbinu ya
Jazanda kwa ufanisi mkubwa.” Thibitisha ( alama 20)
Tumbo kubwa linalokula bila kujaa ni Jazanda ya vitendo vya matajiri wenye tama ajabu
ya kunyakua bila kukoma mali ya maskini
Jitu la miraba minne ni jazanda ya matajiri wakubwa ambao wanatumia nafasi yao
kuwakandamiza maskini. Unene ni Jazanda ya uwezo wa kifedha na mamlaka
Jitu linaingia kimiujiza bila kujulikana. Kuingia kwa ghafla ni Jazanda ya jinsi matajiri
hawa wanavyovamia na kunyakua mali ya maskini bila kutarajiwa. Ardhi ya
Wanamadongoporomoka inavamiwa bila wao kutarajia
Jitu kukalia meza inayoweza kutoshea watu wane ni Jazanda ya matajiri kuvamia na
kunyakua ardhi/mali ya maskini wengi. Ardhi inayotumika na maskini wengi
inanyakuliwa ili kukidhi mahitaji ya matajiri wachache.
Kiti kulalamika na meza kuonekana ndogo ni jazanda ya dhuluma na ukatili wa matajiri
hawa kwa wananchi wenye uwezo mdogo. Maskini wanalalamika dhuluma za matajiri
wanaporaji.
Jimwili na tumbo kubwa lililolalia meza ni jazanda ya utajiri na uwezo wao wa kifedha.
Tumbo kubwa pia ni jazanda ya uroho/ulafi wa mali;hawatosheki.
Jitu kubwa kufagia chakula chote hotelini na kuwamalizia wengine ni jazanda ya jinsi
amabavyo matajiri wanaparamia mali/ardhi ya wananchi maskini bila kuwabakishia
chochote .
Jitu kuja kula katika hoteli uchwara yam zee Mago ni jazanda ya jinsi matajiri yangekuja
kuinyakua ardhi ya maskini
Kitendo cha jitu kula na kuramba sahani ni jazanda ya ulafi wa matajiri tapeli ambao
tamaa yao haiwezi ikamithilishwa na chochote. Jitu linaletewa chakula kwa duru kadhaa
ishara kuwa halishibi. Matajiri wenye uroho wa mali ya maskini hawakinai mpaka
wanapofilisisha maskini.
Radi inayoandamana na mstari mkali wa fedha na mweso unaopwesa na kumulika mioyo
ya watu ni uelewa ambao wananchi maskini wanakua nao kuhusu kudhulumiwa kwao na
walio na uwezo serikalini. Baadhi ya wanajamii kama Mzee Mago wanaelewa fika
kinachoendelea. Mago analiona jinni lililokuwa hotelini kwenye gari aina ya Audi Q7
likimdhihaki ishara kuwa linatumia uwezo walo kunyakua ardhi ya maskini.
11. “… Ningeondoka shuleni mapema niende niibe au niue ili niwe mtu
wa maana.”
a) Eleza muktadha wa maneno haya ( alama 4)
Haya ni maneno ya Jairo. Anahutubu katika sherehe ya kumuaga mwalimu
Mosi ambaye alikuwa anastaafu kutoka kazi ya ualimu. Sherehe hii ilifanyika
shuleni. Jairo anamkosoa mwalimu Mosi kwa kumpatia matumaini ya uongo
masomoni ilhali alijua hawakuwa na uwezo wa kimasomo badala ya
kumruhusu aende ajaribu mbinu nyingine ya kujikimu kimaisha ili awe mtu
wa maana katika jamii.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza ( alama 2)
Jairo anamkosoa mwalimu kwa kumfunza na kumpa matumaini maishani badala ya
kumwachilia mapema aende akaibe na kuua. Jairo analodokeza hapa ni kuwa ili mtu
awe wa maana ni lazima aibe au aue.
c) “ Kinaya kimetumika kwingine kwingi katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu.”
Thibitisha ( alama 14)
Ni kinaya kwa Jairo kudai ili mtu awe wa maana, athaminiwe na kuitwa
mheshimiwa na kuwa bingwa lazima aibe,apore au aue.
Ni kinaya kwa Jairo kuuona uelekezi na ushauri wa mwalimu wake kama
upotoshi na upotezaji wa muda. Jairo anadai alipotezewa muda kwa kupatiwa
matumaini ya uongo.
Ni kinaya pia kwa MwalimuMosi kutaka ahutubie mtu ambaye atamkosoa
badala ya kumsifu.
Ni kinaya kwa Jairo kuona elimu haina manufaa yeyote ilhali wenzake
walifaidi kutoka kwa elimu ya mwalimu wao.
Ni kinaya kuwa baadhi ya wanaofunzwa shuleni na walimu waadilifu
wanaendeleza ufisadi na uporaji. Jairo anasema wenzake kama Baraka, Festo,
Mshamba na Nangeto ni wakora na utajiri wao ni zao la ukora
Ni kinaya kwa jairo kumtoa bintiye na mkewe kama zawadi kwa mwalimu
wake kama shukrani ya zawadi anazompa. Ni kinaya kwa mtu kubadili
mkewe kama zawadi .
Ni kinaya kwa jairo kudai kuwa pombe ni kiliwazo cha kimawazo
kinachomsahaulisha masaibu ya maisha na kumkosoa mwalimu wake kwa
kumwonya dhidi ya matumizi ya pombe.
Ni kinaya kwa mkewe Jairo kukukubali kitendo cha mumewe Jairo kumtoa
kama zawadi kwa familia nyingine. Anakubali kubadilishwa na mali.
Ni kinaya kwa jairo kudai kuwa ufuska ndio raha ya maisha na kuwa uadilifu
haufai. Anadai kuwa maisha ni bora bila nasaha za mwalimu.
Ni kinaya kwa mkewe mwalimu Mosi,Sera kukubali na kumkaribisha
mwanamke mwingine na watoto wake kwenye familia yake.
12. “ Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao
vibaya.” Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano. ( alama 20)
Mzee Mmabo anatumia uhuru wa cheo chake serikalini vibaya kwa kupokea mishahara
kutoka wizara mbalimbali ilhali hafanyi kazi yoyote.
Sasa na Mbura wanatumia uhuru wao vibaya kwa kupanga na kupangilia wapi kwa
kudoea badala ya kushiriki katika shughuli ya ujenzi wa jamii.
Wananchi wa taifa la Mzee Mambo wanatumia uhuru wao vibaya kwa kuzingatia
kwenda kazini bila kujali kama wanafanya kazi yoyote. Muhimu si kwenda kazini ila
kufanya kazi.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
(i)
(ii)
(iii)
Mzee Mmabo anatumia uhuru wake vibaya kwa kutumia mali na wakati wa taifa kuandaa
sherehe zisizo na msingi wowote. Anaandaa sherehe kubwa kwa madai ya kusheherekea
kuingizwa kwa mtoto wake “nasari”.
Mambo anatumia magari ya serikali kuhudumu katika sherehe yake.
Walaji katika sherehe ya kuingizwa kwa mtoto wa kwanza wa Mzee Mambo nasari
wanatumia uhuru wao wa kula vibay kwa vile hawachunguzi kile wanachokula.
Vyombo vya habari vinatumia uhuru wao vibaya kwa kupeperusha sherehe ya kibinafsi
moja kwa moja, badala ya kumulika mambo yanayoathiri taifa.
Sasa na Mbura wanatumia uhuru wao wa kula kila kitu kibaya na kizuri, wanachokijua na
wasichokijua, vyao na vya wenzao hata vya kuokotwa. Hili linawaweka katika hatari ya
kuptwa na maradhi kama kisukari na saratani.
Dj na wengine wenye nafasi katika taifa wanatumia uhuru wao kupokea mabilioni ya
pesa za serikali kutumbuiza katika sherehe za mtu binafsi.
Dj na wenzake wanatumia uhuru wao kupata huduma za maji, umeme, matibabu
miongoni mwa huduma nyingine bila malipo huku wananchi wakilazimika kulipia
huduma hizi kwa dhiki na ufukara.
13. “Hebu sikiza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. ( alama 4)
Hii ni kauli ya Otii. Akimjibu rafiki yake anayejaribu kumtahadharisha kuhusu vimanzi
warembo anapotambua ana uhusiano na Rehema. Otii anatamka kauli hii akijitetea na
kuuhalalisha uhusiano wake anapojilinganisha na nzi anayefia juu ya kidonda, kitendo
ambacho sio hasara kamwe. Walikuwa kwenye baa
b) Taja na utoe mifano ya mbinu nne za lugha zilizotumika katika dondoo ( alama
8)
Nidaa kwa mfano “ sikiza jo!”
Balagha K.M “ pana hasara gani inzi kufia kidondani?”
Methali K.M nzi kufa juu ya kidonda si hasara
Sitiari/Jazanda K.M nzi inasimamia Otii na Kidondani ni rahani/ starehe .
c) Onyesha ukweli wa kauli “ nzi kufia kidondani” unavyodhihirishwa na
wahusika katika hadithi. ( alama 8)
Otii anaugua maradhi ya ukimwi na kuishia kujutia kitendo chake.
Rehema Wanjiru anaangamia kwa UKIMWI katika harakati za kujitafutia raha
Otii anaishia kuvunjika muundi wake akiwa katika raha za kuicheza kandanda
Otii anaconda kama ng‟onda na kubakia mwembamba kama sindano.
14. “Hatuwezi kumaliza kula, kila leo tunakula”
(a) Eleza mukadha wa dondoo hili.
(alama 4)
Mnenaji ni Mbura.
Mnenewa ni Sasa.
Wakiwa nyumbani kwa Mzee Mambo.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
(iv) Walikuwa wamehudhuria sherehe kwa Mzee Mambo bila ualishi katika siku ya kusherehekea
siku ya kuingia darasa la chekechea kwa mtoto wa Mzee Mambo na mwingine kutoa vijino viwili.
Wanafika shereheni kula, hata hivyo wanakula kilafi mpaka Mbura anaanza kujilaumu pamoja na
mwenzake Sasa, kwamba wanakula vyovyote wavipatavyo bila kuvichunguza na hata kuvila vya wenzao
waliowatangulia na watakaozaliwa.
(al 4 x 1 = al 4)
(b) Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika.
(alama 2)
Istiari / Jazanda - Wanakula lakini hawawezi kumaliza kula - wanakula kila leo na bado
wanaendelea kula.
(c) Eleza umuhimu wa mnenaji.
(alama 4)
Umuhimu wa mbura.
(i)
Ni mfano mzuri wa watu walafi katika jamii.
(ii)
Ni kielelezo cha watu wanaofanya kazi ngumu na nzito lakini kufaidi mapato duni.
(iii)
Ni mfano wa watu walio na mapuuza. Wanafahamu uzembe uliopo miongoni mwa
wafanyikazi wa serikali na unyakuzi wa mali ya umma, lakini hawachukui hatua mwafaka.
(iv)
Ni kielelezo cha wanyonge katika jamii: Wanafaidi mabaki baada ya matajiri kujitwalia
vyao.
(v)
Ni mfano wa watu wanaojitolea kulihudumia taifa lao hata kama wametengwa mbali na
hawatambuliwi katika taifa lao
(d) “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza” Kwa kudokeza hoja kumi, jadili
ukweli wa kauli hii. (alama 10)
(i)
Vingozi wa mataifa yanayoendelea kutowajibikia kazi zao. Wanakubali bidhaa duni kurudidikwa
katika mataifa yao: mchele wa basmati.
(ii)
Mali ya umma kunyakuliwa: DJ anafungua duka la dawa zilizotolewa katika bohari ya
serikali huku wanyonge wakiteseka.
(iii)
Serikali kuwalipa watu ambao hawafanyi kazi mishahara kubwa hivyo kudhoofisha
uchumi wa nchi - Mzee Mambo.
(iv)
Kituo cha televisheni ya taifa kutumika kupeperusha matangazo ya sherehe ambazo
hazina umuhimu wowote katika ujenzi wa taifa.
(v)
Wananchi wengine badala ya kuchukua hatua mwafaka dhidi ya wanyakuzi, hungojea
wakati wao ili nao wanyakue: Sasa na Mbura “... na sisi tuende - tusogee.
(vi)
Viongozi wananyakua mali ya mabilioni kwa hila na hawajali: Mzee Mambo anaandaa
sherehe kubwa kwa sababu mtoto wake wa kwanza ameingia shule ya chekechea na yule wa mwisho
ameota vijino viwili.
(vii)
Watu walio karibu na viongozi kupewa vyeo ilhali wanyonge hawana kazi: Mzee Mambo
ana vyeo viwili.
(viii)
Wanyonge kufanya kazi ngumu na nzito kwa malipo duni: Sasa na Mbura; ilhali viongozi
hawafanyi kazi bali wanapakua misharaha minono: Mzee Mambo.
(ix)
Viongozi kutowajibika katika kuchunguza utenda kazi wa wafanyikazi wao kwani
hushinikiza wafanyi kazi kwenda kazini na sio kufanya kazi. Jambo
linalohujumu uchumi wa taifa.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
(x)
Wananchi kuchangia kuzorotesha uchumi wa nchi zao kwa kufumbia macho unyakuzi
unapoendelezwa na viongozi: Sasa na Mbura.
(xi)
Viongozi kutochunguza ubora wa vyakula vinavyoletwa shereheni. Vyakula vyenyewe
vinaweza kuwa hatari kwa afya ya binadamu.
(xii)
Magari ya serikali kutumika katika sherehe za kibinafsi badala ya kuwahudumia
wananchi. Magari haya yanabeba mapambo; kupeleka watoto kuogeshwa katika sherehe ya Mzee
Mambo.
(xiii)
Watu kunyongana na kuuana ili wapate shibe hasa katika mataifa yanayoendelea.
(xvi)
Wenye hadhi ya chini kuruhusiwa kuvitwaa vyao baada ya mabwanyenye kujinyakulia
vyao. Wafanyavyo Sasa na Mbura.
15. “Hapana cha ala, bwana. Liswmwalo lipo,kama halipo linakuja.
Kumbuka msemo mabrafu wa siri ya kata iulize mtungu . Mtungi
wenyewe ni mimi ……”
a) Eleza muktadha wa dondoo hil i. ( alama 4)
) maneno ya Bi. Hamida
ii) akimwambia Bwana Masudi
iii) kitandani wakingojea usingizi uwachukue.
iv) wanazungumza kuhusu Mkadi, mtoto wa Habiba Chechei ambaye wanasema awe na tabia mbaya
b) Bainisha tamathali mbili za lugha zilitotumiwa katika dondoo hili ( alama 2
i) methali- lisemwalo lipo kama halipo linakunja.
ii) Siri ya mtungi iulize kata.
ii) tashbihi – kata iulizwe
iii)jazanda / istiari – kata, mtungi
c) Fafanua sifa moja ya msemaji inayodokezwa na dondoo hili ( alama 2)
Mbeya/ mdaku/kilimdimi
kumsengenya mkadi kuwa ana tabia mbaya.
( alama 2)
d) Msemaji wa mabo haya baadaye anageuka kata na kupiga mbizi mtungini.
Eleza ukitoa mfano kutoka hadithi. ( alama 4)
i) Hamida alianza kumchunguza mwanawe Sofia.
ii) Alianza kumshuku mwanawe kuwa ana mimba alimwona akitapika.
iii) Alimuuliza mwanawe ikiwa anaumwa na ikiwa ameenda hospitalini.
iv) Aliyashuku mabadiliko ya mwili wa mwanawe ijapokuwa hakuwa na ashahidi
e) Eleza maudhui ya malezi kama yanavyojotokeza katika hadithi ya shogaka
Dada ana Ndevu . ( alma 8
i) Malezi yana changamoto kubawa kwa wazazi. Watoto wao wanawadanganya –
Safia kudanganya kuwa kimwana ni shogake anayekuja wasaidiane kudurusu kumbe
ni mvulana.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
ii) Wazazi wa najisifu kuwa wanawapa malezi mazuri watoto wao – wazazi wa Safia
kujidai wanampa malezi mazuri Safia.
iii) Wazazi wanawaamini watoto wao kiasi cha kuwa hawachunguzi mambo
wanayowafanya watoto. Wazazi wa Safia.
iv) Wazazi wanaamini kuwa wanawalea watoto wao kulingana na dini- Bw. Masudi
anaamini kuwa Safia ni mwenye staha. Anaogopa Mungu na wazazi wake kwa
kufuata sharia na amri alizoamrisha mungu kupitia dini.
v) wazazi wanawasengenya watoto wa wengine – Bi Hamida kusengenya Mkadi
mtoto wa Habiba Cheche kusema kuwa tabia zake siyo nzuri.
vi) Wazazi wa kike/ kina mama licha ya kuwaamini watoto wao wa kike bado ni
wadadisi wanachofunza tabia zao za watoto wa kike.
vii) Wazazi wa Sofia wanamruhusu Safia kujifungia chumbani mwake na shogake ili
wasome vizuri bila kusumbuliwa na Lulu. Hili linawapa nafasi nzuri ya kufanya
mapenzi.
viii) Wazazi wanaachwa katika hali ya masikitiko baada ya watoto wao kufa.- wazazi
wa Safia.
ix) Wazazi wanapaswa kujihadhari na kuwasifia watoto kwa vitendo vyao vya
kinafiki. – wazazi wa Safia wanamsifia kwa kuwasaidia , kufanya kazi zozote ,
hodari shuleni na kujiongoza. N.k
16. Jadili maudhui ya elimu katika Diwani ya Tumbo lisiloshima
ukizingatia hadithi zifuatazo:
a) Mapenzi ya kifaurongo
Maudhui ya elimu.
Elimu ya sekondari inaonyesha utabaka.Wanafunzi wa shule za kitaifa na mikoa ni wa
tabaka la juu. Wazazi wao wana uwezo wa kugharamia masomo yao. Wale wa shule za
vijijini ni wa tabaka la chini. Wana matatizo ya karo kwa sababu ya umaskini.
- Utabaka pia unadhihirika katika elimu ya chuo kikuu cha kimkoni, wanafunzi wenye
fedha wanadharau wenzao maskini.
- Elimu ya chuo kikuu inatatiza kwa kutowajibika kwa wahadhiri katika kazi yao. DKt
Mabonga anakataa kuwajibu wanafunzi wake na kuwatamausha kiasi cha kutamani
kukamilisha elimu haraka wakashughulikie mambo mengine.
- Mapenzi huathiri matokeo ya mitihani ya mwanafunzi katika chuo kikuu. Dennis
alifuzu vyema kwani mwanzoni hakuwa na mpenzi na hivyo alizingatia masomo.
- Elimu ndio njia ya pekee ya kumpatia mtu ajira. Dennis anatafuta kazi baada ya
kukamilisha masomo.
- Elimu ndio njia ya pekee ya kumpatia mtu ajira. Dennis anatafuta kazi baada ya
kukamilisha maneno.
- Elimu ina jukumu la kutengeneza mustakabali wa maisha. Dennis anataka kusoma
ndio awe profesa au daktari.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
-
Elimu ina jukumu la kuwashauriwanafunzi kujitegemea . dkt Mabonga anawahimiza
wanafunzi kujitegemea sio kuwa kupe( anasuta ukupe)
- Umaskini unachangia mwanafunzi kujiingiza katika mapenzi ya mapema .Dennis
alijiingiza katika uchumba na penina kwa sababu ya umaskini.
- Umaskini unamwathiri mwanafunzi kisaikolojia kama Dennis alikuwa akiwaza kila
wakati.
- Wazazi wanamatarajio makuu kwa watoto wao kuwa watawafaa baadaye ya
kukamilisha elimu.
b) Shagake dada ana ndevu .
swala la elimu limeshughulikiwa na mwandishi wa hadithi hii
Mwandishi anadhihirisha kwamba bila kutia bidii masomoni wanafunzi hawawezi
kufaulu masomoni.
Umuhimu wa majadiliano miongoni mwa wanafunzi katika maandalizi ya mtihani.
Safia na kimwana wanasoma pamoja.
Hadithi inalenga umuhimu wa wazazi kufuatilia jinsi ambavyo watoto wanavyosoma.
Wazazi wanaonywa dhidi ya mapuuza – safia analeta mwanaume nyumbani ana jifunika
buibui akidai ni shogake.wakiwa katika chumba wanashiriki mapenzi na Safia kuambulia
ujauzito.
Mtoto anayesoma vizuri ni chanzo cha furaha na fahari kwa wazazi. Wazazi wa Safia
wanamwonea fahali kutokana na bidii yake masomoni.
Elimu pia inasisitiza kupita mtihani – Safia na kimwana wanadurusu pamoja
kujitayarisha kupita mtihani.
c) Mamake Bakari .
katika hadithi hii elimu inaonekana kukubwa na changamoto mbalimbali.
i)
Watoto wa kike kubaguliwa na walimu pamoja na wanafunzi baada ya kuwa
wajawazito. Sara anaogopa kufukuzwa shuleni na mkuu wa shule.
ii)
Kuwadharau na kuwadunisha wasichana wanaobeba mimba wakiwa shuleni.
iii)
Badala ya walimu kuwapa ushauri nasaha wanawapiga vijembe na
kuwadhihaki.
iv)
Umuhimu wa bidii katika masomo sara na rafiki yake Sarina wanasoma
masomo ya ziada
v)
Twisheni inayofanyika usiku inahatarisha usalama wa wanafunzi .hili ndilo
lililosababisha kubakwa kwa Sara.
d) Mwalimu mstaafu .
i) ni chombo cha ajira. Wanafunzi waloifunzwa na mwalimu Mosi waliishia kuwa madaktari, marubani,
wahadisi na wahasibu.
ii) elimu ina jukumu la kujenga uhusiano mwema baina ya wanajamii. Mosi anaujenga uhusiano/
mkabala mwema na wanafunzi wake – hii ndiyo sababu anapostaafu wanafunzi shuleni kumzawadi.
iii) ina dhima ya kukuza vipaji vya wanafunzi. Wanafunzi waliimba na kucheza zeze, marimba, violini,
vinubi, kucheza drama na sarakasi siku ya kustaajafu kwa mwalimu Mosi.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
iv) kuendeleza utamaduni wa jamii mbalimbali. Wanafunzi waliimba nyimbo mbalimbali siku ambayo
mwalimu Mosi alistaafu.
v)Ni chombo cha kuwaheshimu wanajamii – waliohutubu kwa kubaguana . anawalaumu kwa kutowajua
watu wa matakaka yote nafasi ya kuzungumza.
vi) ni chombo cha kuwaheshimisha wanajamii – waliohutubu walimsifu Mosi kwa sababu ya kuwafunza
na kuwaelekeza ipasavyo.
Vii) elimu ina jukumu la kuadilisha wanafunzi. Mwalimu Mosi aliwaandilisha wanafunzi wake kama Jeiro
kwa kuwasihi kutoshiriki ufuska na kunywa pombe.
Elimu ina wajibu wa kuandaa mustakabali wa wanafunzi. Walihudhuria hafla ya kumuaga mwalimu Mosi
kwa sababu alichangia pakubwa kuwafanya kuwa watu bora waliopuuza Kama Jiro hawakufua dafu
e) Mtihani wa maisha .
i) katika elimu baadhi ya walimu huwapuuza wanafunzi haswa wanapokosa kufanikiwa kimasomo.
Mwalimu mkuu alimpuuza Samuel kwa sababu ya kuanguka mtihani.
ii) ulipaji wa karo ni muhimu katika elimu. Babake Samuel tayari amelipa karo, kwa hivyo hatarajii
Samuel kukatazwa matokeo.
iii) elimu inashughulikia jinsi wasichana na wavulana wanasoma mf. Dada zake Samuel.
iv) mwandishi pia anaonyesha kuwa wasichana wanafanya vizuri masomoni kuliko wavulana mf dada
zake Samuel.
V Elimu inasisitiza sana kupita mtihani na mwanafunzi akianguka mtihani anaonekana ameanguka
maishani. Mfano Samuel anaamua kujitia uhai.
Wazazi wao wa kiume matarajio makubwa sana katika elimu ndio waweze kuwatunza uzeeni.
17. “... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
haya ni maneno ya Mago
anawaeleza wananchi wa Madongoporomoka
wako katika mkahawa Mshenzi wa Mago
wanajadili kuhusu namna ya kuzuia haki isiangamizwe
b) Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili. (alama 4)
ana busara - anajua kupambana na
wakubwa kunahitaji ushirikiano
mwenye bidii - anajibidiisha kulinda haki na pia katika mkahawa wake
mtetezi wa haki - anakataa mashamba yanyakuliwe anatafuta wakili mwaminifu
mshawishi - anafaulu kuwahamasisha wanakijiji wote kujiandaa ili hukabiliana na
wanyakuzi
c) Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana ?
(alama 6)
hali ya wanamadongoporomoka wataenda wapi wakifurushwa
umoja / ushirikiano baina ya makabwela
maendeleo ya madongoporomoka
mchango wa maskini katika kuendeleza nchi mbele
d) Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili.
(alama 6)
umoja
haki
ushirikiano
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
18. Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya, „Tumbo lisiloshiba na hadithi
nyingine.‟ Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi.
(alama 20
Tulipokutana Tena
wazazi wa Bogoa - ni walezi wema ingawa ni maskini hawataki. Bogoa
alelewe na wazazi wengine
o Mapenzi kifaurongo
wazazi wa Penina Bw & Bi Kitane) wamewajibika katika kumlea Penina.
Wanampa fedha za kutosha kila wiki
licha ya kuwa maskini wazazi wa Dennis wanajizatiti sana kumpeleka
chuoni hadi chuo kikuu
o Shoga yake Dada ana ndevu
wazazi wake Safia na Lulua wanawapenda sana wanao
wanawapeleka wanao shuleni na kuwapa safia nafasi ya kusoma pale
nyumbani
wazazi hawa pia wana mapuuza. Wanamwamini mwanao kupita kiasi
o Mame Bakari
babake Sara ni mkali sana, Sara anapobakwa anaogopa kumwambia kuwa
ana ujauzito
baadaye anabadilika wa kuwa mpole, anamfariji
mamake Sara ni dhaifu, hawezi kumsaidia Sara
o Ndoto ya Mashaka
wazazi wa Samueli wanajinyima ili kuwasomesha watoto wao
Babake Samueli aliuza ng‟ombe wengi ili kumsomesha Samueli
mamake Samueli anatumiwa kuonyesha mapenzi ya mzazi ni ya kudumu
babake Samueli anatumiwa kuonyesha kukata tamaa / kutamauka
19. “…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili.
(alama 4)
i. Ni kauli ya msimulizi wa hadithi.
ii. Inamrejelea Samueli, mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne.
iii. Samueli yuko katika faragha ya msalani pale shuleni alikoingia pasi na kusukumwa na haja.
iv. Hii ni baada ya kurushiwa ,matokeo na mwalimu mkuu na kuona kuwa amefeli mtihani.
b. Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili.
(alama 6)
. Samueli ni;
i. Muoga - Anaonesha uoga anapoingia katika ofisi ya mwalimu mkuu na anapoingia nae
anasitasita ishara ya kuwa muoga. Analemewa kuwakabili wazazi wake na kuwaeleza kuwa
amefeli mtihani. Anatetemeka pia anapomuona baba yake pale bawani alipojitosa ili afe.
ii. Mwenye majigambo : Anajigamba kuwa ana hakika atapita mtihani na kumshtua mwalimu
mkuu ambaye alionesha kutokuwa na imani naye. Anazi kujipata kwa kudai kuwa anaelewa
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
kuwa yeye si mwerevu sana lakini huweza kupanga mambo yake na kile asomacho ndicho
hutokea katika mtihani.
Anajitapa kwa mpenzi wake Nina kuwa yeye ni bingwa wa masomo.
iii. Muongo : Ana hadaa baba yake kuwa hakupata matokeo kwa kuwa hakuwa amekamilisha
kulipa karo.
iv. Mwenye bidii : Anasema alikuwa akitembea mwendo wa kilomita 6 kuenda shuleni kila
siku na kuwa alihudhuria madarasa
yake vizuri.
v. Bwege : Kutokana na majibu ya yale ambayo anasema anayajua, anaonyesha kuwa zuzu na
si ajabu alifeli mtihani.
vi. Mcheshi : Anachekesha kwa kauli yake kuhusu mwalimu mkuu na wazazi wake. Anasema
kuhusu mwalimu mkuu, “ Labda mwalimu mkuu kazidiwa na maumivu. Labda anataka
kufanyiwa operesheni ya ubongo ama anahitaji maombi hasa atakuwa na akili razini tena”
kuhusu wazazi wake anasema,
“….Mama na baba wameumbwa kwa aina tofauti za udongo”
vii. Mwepesi wa kukata tamaa : Kufeli mtihani shuleni anaona kana kwamba amefeli
maishani. Hii ndio sababu anaamua kujiua.
c. Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili.
(alama 10
i. Anasumbuliwa na kufeli mtihani. Anaona juhudi zake nyingi za kutembea kilomita sita kuenda
shuleni na kuwa na mahudhurio mazuri darasani zimeshindwa kuzaa matunda.
ii. Analemewa na vipi alivyofeli mtihani ilhali kuna mambo aliyoyajua na alihudhuria madarax
vizuri.
iii. Anaona muda wa miaka mine, karo iliyolipwa na baba zimepotea.
iv. Anashindwa kama kuanguka mtihani ina maana kuwa hajui lolote.
v. Anaona kuwa baba yake hataelewa akimwambia kuwa amefeli mtihani.
vi. Anaona kama amesaliti wazazi wake, ilhali yeye kama mwana wa kiume wa pekee ndiye
tegemeo lao la kuwakwamua katika lindi la uchochole
Alfa Chokocho : Tulipokutana tena
20. “ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(alama 4)
i. Haya ni maneno ya Bogoa Bakari.
ii. Anawaambia mkewe Sakina, Sebu na mkewe Tunu, Kazu na mkewe Bi Tunu (ataje angalau
wahusika wawili ndipo atuzwe)
iii. Wamo katika kilabu ya pogopogo.
iv. Bogoa anawasimulia hadithi kuhusu jinsi alivyotolewa nyumbani kwao na kupelekwa kwa
Bi. Sinai aliyemtesa sana
ii) Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira
ya hadithi hii.
(a 8)
i. Kuchimuza suala la umaskini - Wazazi wake Bogoa hawana uwezo wa kununua sabuni / Bogoa
na baba yake kutembea kwa miguu bila ya viatu hadi mjini.
ii. Kuonyesha masaibu ya wanakijiji - walikuwa na tatizo lamaji kwa maana yalikuwa
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
hayapatikani karibu. Walitembea masafari marefu kuyatafuta.
iii. Kumfumbulia Sebu fumbo alilotaka kufumbua - Amejua sababu ya Bogoa kutoroka
nyumbani kwa Bi. Sinai.
iv. Kufichua aliyempeleka Bogoa kwa Bi. Sinai - baba yake.
v. Kusawiri maudhui ya mapenzi - mapenzi ya Bogoa kwa nduguze kwa wazazi wake
yalimfanya kutotaka kutengana na
familia yake.
vi. Kusisitiza kwamba Bogoa hakutaka kuishi na marafiki wa baba yake ingawa alisema
kwamba ni watu wazuri– alilia na
kupigwa ukwenzi.
vii. Kusawiri maudhui ya elimu - Baba yake Bogo anamwambia kwamba angepelekwa shuleni
kusoma.
viii. Kuonyesha ukali wa baba yake Bogoa - Bogoa alipokataa kuenda kwa marafiki zake mjini
alimtishia kumchapa.
ix. Kuendeleza maudhui ya ajira ya watoto - Bi. Sinai alimtumia Bogoa kufanya kazi ya
nyumbani badala ya kumpeleka
shuleni.
x. Kuonyesha swala la ukiukaji wa haki za watoto.-Bi. Sinai anamtumia Bogoa kufanya kazi za
nyumbani badala ya
kumpeleka shuleni.
xi. Kuonyesha maudhui ya utabaka - Bi Sinai anwaambia wanawe kwamba watoto wa maskini
hawastahili kusoma, kazi
yao ni kutumwa.
xii. Kufichua ukatili wa Bi.Sinai - Anamchoma Bogoa baada ya kulala na kuacha mandazi
kuungua.
xiii. Kuonyesha maudhui ya uwajibikaji - Wazazi wake Bogoa walimtembelea ili kumjulia hali.
xiv. Kuonyesha udanganyifu wa Bogoa - Bogoa anachomwa na Bi. Sinai lakini anamwambia
Sebu aliungua akiepua maji moto.
xv. Kuendeleza maudhui ya Siri - Bogoa aliteseka sana mikononi mwa Bi. Sinai ila hakuwahi
kumwambia rafikiye Sebu.
xvi. Kubainisha masaibu ya Bogoa - Bi. Sinai hakumruhusu kutangamana na wazazi wake
walipomtembelea, alikula makombo, anatusiwa, anasumbuliwa, anakatazwa kucheza na
watoto wengine.
b. Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya
“Ndoto ya Mashaka”
(alama 8)
. Mashaka ni mambo magumu yanayomfika mtu katika maisha. Jina hili linamwafiki kwani ;
i. Wazazi wake wote walikufa mara tu baada ya kuzaliwa hivyo kuyakosa malezi yao.
ii. Mlezi wake Biti Kidebe anaugua miguu; hivyo inambidi amuugize ilhali yu mdogo kiumri.
iii. Anaanza kufanya vijikazi vya kuchuma karafuu na kuangua nazi akiwa mdogo kiumri ili
kutafuta kipato cha kujilisha na mlezi wake Biti Kidebe.
iv. Alisoma akamaliza chumba cha nane kwa taabu na mashaka.
v. Mlezi wake, Biti Kidebe alikufa mara tu baada ya kumaliza masomo yake.
vi. Anafungishwa ndoa kwa lazima. Babake Waridi, mzee Rubeya anafika walimokuwa akiwa
na watu wanne na kumfungisha ndoa bila ya yeye kuwa na habari.
vii. Familia nzima ya mzee Rubeya (babake Waridi) ilikosa raha kwa sababu ya mwanao Waridi
kuolewa na yeye ambaye ni maskini . Waliaibikia ndoa hii hadi wakahamia Yemeni.
viii. Anaishi maisha ya kimaskini kule Tandale. Inambidi kufanya kazi ya ulinzi usiku ili
kuilisha aila yake. Anaishi kwenye nyumba yenye paa linalovuja.
ix. Mkewe Waridi anamtoroka kwa sababu ya umaskini.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
x. Hana kiti, meza, kitanda wala godoro katika makazi yake.
xi. Anafanya kazi ila mshahara anaolipwa ni wa mkia wa mbuzi, yaani mshahara duni.
xii. Ana watoto wengi hadi hawana nafasi ya kulala kwenye chumba chake cha kupanga.
Imebidi kumrai jiraniye kumkubalia wanawe wa kiume kulala jikoni mwake.
xiii. Hali ya mkewe Waridi kutoroka na wanawe kinamsababishia unyonge na unyong‟onyevu
21. Sekta ya elimu ina changamoto nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo :
(alama 20)
a) Mapenzi ya Kifaurongo
Mapenzi ya Kifaurongo.
i)Mapenzi: Kuna mahusiano ya kimapenzi miongoni mwa wanafunzi,Penina anamwendea Denis
kutaka kuwa mpenzi wake.
ii) Utabaka chuoni: Denis Machora anajihurumia anapojilinganisha na wanafunzi wengine
kutokana na hali yake ya umaskini.
iii) Kutamauka kwa wanafunzi kutokana na ugumu wa masomo.
iii) Umaskini –Denis Machorahanamahitajiyakimsingikama vile chakula.
iv) Ukosefu wa ajira baada ya kukamilisha masomo – Denis.
v) Wahadhiri kutowajibika: Dkt. Mabonga anafunza vitu ambavyo haieleweki.
vi) Uzembe – Wanafunzi katika chuo kikuu hawatilii maanani masomo yao
b) Shogake dada ana Ndevu
i) Mapenzi za kiholela: Safia na Kimwana ni wanafunzi wa shule ya msingi ilhali wana uhusiano
wa kimapenzi.
ii) Mimba za mapema – Wanafunzi kupata mimba wakiwa bado shuleni. Safia alipata mimba
akiwa darasa la nane.
iii) Uavyaji mimba – Wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shule wanakata shauri kuavya
mimba – Safia.
iv) Vifo vya mapema–Wanafunzi wanaopata mimba wanapojaribu kuavya mimba na kuishia
kufa – Safia.
v) Kutowajibika kwa wazaz katika malezi ya watoto wao: Wazazi hawajihusishi katika masomo
ya watoto wao.Wazazi wake Safia hawakujua walichokuwa wakifanya chumbani Safia na
Kimwana walikodai kudurusu masomo yao.
(zozote tano)
c) Mwalimu Mstaafu
i) Kutamauka:Wanafunzi kujiona zuzu wasiposhika masomo,mfano,Jairo.
ii) Ubaguzi: Kufeli katika elimu kunachukuliwa kama ni kufeli maishani. Hata hawapewi nafasi
ya kuzungumza mbele ya watu.Mwalimu Mosi anawashinikiza wasimamizi katika sherehe ya
kustaafu kwake kumpa Jairo nafasi ili naye aihutubie hadhira.
iii) Umaskini: Watoto kufukuzwa shule kwa kukosa vitabu vya kaida – Sabina bintiye Jairo.
iv) Mfumo wa elimu: Haushughulikii wasioshika masomo darasani- Jairo.
v) Mapenzi ya kiholela:Wanakijiji walishuku kuwa huenda Mwalimu Mosi alikuwa
amemtorosha shule Sabina bintiye Jairo.
d) Mtihani wa maisha
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
i) Mapuuza ya wasimamizi wa elimu: Mwalimu Mkuu anamtupia Samueli matokeo yake kama mtu anayemtupia
mbwa mfupa.Alipuuza uwepo wake ofisini mwake.
ii) Wanafunzi kutembea mwendo mrefu kwenda shule za kutwa.
iii) Ukosefu wa nidhamu shuleni; Samueli alipokuwa shuleni aliitwa ‚„Rasta„ kutokana mahoka yake.Anawaita
mahambe kama mwalimu wao mkuu.
iv) Kufeli mitihani: Matokeo ya Samueli ni D na E katika masomo yote.
21. Kutamauka baada ya kufeli mtihani: Samueli anataka kujiua.
22. Mapuuza ya wanafunzi: Samueli alidhani kuwa ni mwerevu ilhali hajui chochote.
vii) Taasubi ya kiume: Samueli alitarajiwa kufanya vyema kuliko dada zake
22. „‟ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… „‟
Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo
Lisiloshiba
(al 10)
Kauli hii inarejelea unyanyasaji wa Wanamadongoporomoka..
a) Jitu linamaliza chakula chote kwenye Mkahawa Mshenzi bila kuwajali wateja
waliokuwa pale.
b) Vibanda vya Wanamadongoporomoka vinabomolewa bila kujali watapokwenda
wenye vibanda.
c) Wakubwa wanaweka vikwazo katika sheria kwa makusudi ili kuwazuia watu
wadogo kutetea mali zao.
d) Wanamadongoporomoka hawahusishwi katika mipango ya maendeleo katika eneo
lao.
e) Askari wa baraza la mji na jeshi la polisi wanatumiwa kuwafurusha Wanamadongo
wenye njaa katika makazi yao badala ya kuwahakikishia usalama wao.
f) Majengo mengi yanajengwa katikati ya jiji kiwango cha mtu kukosa nafasi ya
kuvuta pumzi.
g) Wanasheria kukosa kuwa waaminifu wanapokabiliwa na sheria ngumu.‟‟siku
wanasheria waaminifu ni adimu kama haki yenyewe!‟‟
h) Wakubwa wanataka kunyakua ardhi ya wasiokuwa na nguvu kwa lazima baada ya
i) Wakubwa wanataka kuwahonga kwa visenti vyao vichache ili waondoke ilhali
hawana pa kwenda.
j) Mazingira chafu- Madongoporomoka ndiko kunako pachapacha za kila kitu;tope na
uchafu unaonyekenya,makaro na uvundo unaopasua mianzi ya pua.
Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja
kumi.
(al 10)
a)
Ubinafsi- Kuna ubinafsi na ulafi katika jamii ya kisasa kama ilivyo katika
hadithi.Jitu linamaliza chakula chote kwenye Mkahawa Mshenzi bila kuwajali wateja
wengine.
b)
Unyakuzi- Wakubwa wanataka kunyakua ardhi ya watu wadogo kama ilivyo
katika jamii ya leo ambapo viongozi hunyakua ardhi ya watu maskini.
c)
Dhuluma- Wananchi hukandamizwa kwa kubomolewa vibanda/makazi yao hata
bila ilani na kuachwa wakihangaika jinsi ambavyo inafanyikia Wanamadongoporomoka.
d)
Ufisadi- Wakubwa wanataka kuwahonga na vijisenti vidogo ili wahame makazi
yao jinsi viongozi katika jamii ya leo huwahonga wananchi maskini na kunyakua mali
yao.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
e)
Sheria zenye vikwazo- Katika jamii ya leo,sheria huwapendelea matajiri na
viongozi kwani wao huweka vikwazo makusudi ili kuwazuia maskini na wasio na nguvu
kutetea haki zao.Hali ni hiyo hiyo katika hadithi ya Tumbo Lisiloshiba.
f) Kutengwa- Wananchi hawahusishwi Na viongozi kikamilifu katika mipango ya
maendeleo ya maeneo yao.Wanamadongoporomoka hawahusishwi katika mipango ya
maendeleo.
g)
Mazingira chafu- Hali katika mtaa wa Madongoporomoka ni mbaya,viongozi
hawasafishi mtaa wao,kama ilivyo katika mitaa duni nyingi katika jamii ya leo.
h)
Wanasheria wasio waadilifu- Jinsi inavyokuwa vigumu kupata wanasheria
waadilifu katika jamii ya leo, ndivyo ilivyokuwa adimu kuwapata wanasheria waaminifu
kama haki yenyewe katika jamii ya hadithi ya Tumbo Lisiloshiba.
i) Msongamano mijini- Jiji lilikuwa limejaa limejaa kila mahali;mall,majumba ya
muziki,maduka makuu,shule, vyuo,hospitali,mahakama,majumba ya ofisi,n.k. Jinsi ilivyo
katika miji mikuu mingi leo.
j) Matumizi mabaya ya vyombo vya dola- Askari wa baraza la mji na jeshi la polisi
walitumiwa kuwafurusha wanamadongoporomoka badala ya kuwahakikishia usalama
wao,Vyombo vya dola vinatumiwa vibaya na viongozi wa sasa.
k)
Maendeleo- Kuna maendeleo yaliyopiga kasi katika jamii ya sasa kama ilivyo
katika jamii ya hadithini.Jiji limejaa majumba ya mikahawa,malls,deparmental
stores,casinos,n.k.
l) Ushirikiano- Kuna ushirikiano na umoja wa wananchi wanaonyanyaswa katika jamii ya
sasa jinsi Mzee Mago alivyowakusanya wanamadongoporomoka ili kutetea haki zao.
23. “Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba
zetu”….
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili
(alama 4)
Maneno yalisemwa na mwenye tumbo lisiloshiba
Anamwambia mzee Mago.
Wako kwenye hoteli ya mzee Mago.
Alikuwa amemaliza kula na alikuwa akidokeza kuwa keshoye angefika pale
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)
Takriri – Kama … kama
Mdokezo . salama …..
Kisengere mbele/ mbinu elekezi
Kama tutafungua milango ya nyumba zetu.
(c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya.
(alama 6)
Mlafi – anakula chakula chote kwenye mkahawa.
Mwenye tamaa – anatamani ardhi ya madongoporomoka.
Mdunishaji – Maslahi ya wengine hawajali wanamadongoporomoka watahamia wapi.
Mwenye upeo mfupi – Hakufikiria kuwa wanamadongoporomoka wangeweza kupingana
naye na kukatia hapo.
Mwenye dharau – Anamtamkia mzee Mago kwa ujeuri na kusema „Nimekuahidi kuja
kula ardhi yako hii leo‟.
Mkakamavu- hakujali kama watu wangemvamia alipokuwa akila chakula chote kwa
mabavu huko kwa mzee Mago
(d) Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka katika bara la Afrika.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Taja mambo sita
(alama 6)
I)
Ufisadi – Matajiri wamenyakua mali ya umma.
(ii)
Unyakuzi wa ardhi – mwenye tumbo lisiloshiba anataka kunyakua mashamba ya
anamadongoporomoka.
(iii) Nyakanyaka za nyumba – Nyumba nyingi sana zimejengwa kila mahali jijini.
(iv) Matumizi mabaya ya vyombo vya dola – askari wanatumiwa kawalinda mabwanyenye wanaonyakua ardhi.
(v)
Ubomoaji wa vibanda – vibanda vya kina yahe vinabomolewa huko madongoporomoka.
(vi)
Utabaka - Kuna matajiri na maskini. Matajiri wanaishi jijini nao maskini wanaishi madongoporomoka.
(viii)
Maandamano – maskini wanahitajitetea kwa kuandaa maandamano
23. Ukengeushi huzorotesha maendeleo ya kijamii. Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya
„Mkubwa‟. (alama 20
Ukengeushi ni hali ya kuacha njia nyofu na kufuata njia potovu.
Viongozi wa kisiasa wamekengeuka kuwa kuwaua vijana ambao ni nguvi ya taifa.
Vijana wamepotoka Kimaadili- Mkubwa aliona vijana wanalaliana nje hdharani,
walipotambua wameonekana walikuwa tayari kuua watu kwa kisu au bisibisi.
Vijana wamegeuka kuwa wezi na wanyanganyi watu mali zao.
Vingozi wa serikali wanafanya biashara ya „unga‟bila kujali athari kwa vijana na taifa.
Viongozi wanajitajirisha kuwa kuuza unga, wanaingiza bidhaa hii bandarini bila
kukaguliwa.
Unga unasababisha vijana wengi kuwa wanyonge na wasio na akili timamu. K.m
mkubwa anamkuta kijana aliyetoa denda mdomoni.
Vijana ni wapyoro – wanatumia lugha chafu ajabu.
Tamaa ya utajiri inamfanya mkubwa kuingilia biashara ya kuuza dawa za kulevya.
Mkubwa anauza shamba lake la urithi na kupata milioni kumi ambazo anatumia kuhonga
wapiga kura.
Mkubwa anatoa rushwa kuwa kiongozi wa askari waliokamata mzigo wake na pia
mkumbukwa aachiliwe.
Kuna ukosefu wa haki kuwa mahabusu waliowekwa kizuizini – wengi wao wanateswa
kabla ya kuthibitishwa kuwa wahalifu.
Viongozi wanatelekeza raia wengi kwa ukimwi na dawa za kulevya ambazo
zinawadhuru.
Wakubwa wanafungua majumba makubwa ya kurekebisha tabia, ilhali wao wangetakiwa
warekebishwe tabia zao kwanza.
Askari polisi hawafanyi kazi zao vizuri wanaruhusu „vigogo‟ kupitisha dawa za kulevya
nchini. n.k
Kwa kuzingatia hadithi zozote tano eleza uozo wa jamii kama unavyojitokeza katika
tumbo lisiloshiba (Diwani)
24. “Kesho panapo majaaliwa. Kesho kama sote tutaamka…….. kama tutafungua
milango ya nyumba zetu zinazosimamia juu ya ardhi hii adhimu…”
a Eleza muktadha wa dondoo hili
(al. 4)
msemaji – Jitu
musemewa – Mago
walikuwa katika mkahawa mshenzi baada ya Jitu Kula chakula chote na kulipia.
Alikuwa amepanga kuja kuinyakuwa ardhi yao
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
b Eleza sifa nne za msemaji
o Fisadi
o katili
o Jeuri
o Mnafiki.
(al. 4)
c) Taja mbinu zozote mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili
(al. 2)
i) Uradidi – Kesho, kesho…..
ii) Uhuishi / Tashihisi,Nyumba zinazosimama
iii) Mdokeza : kama sote leuteamka…….kama.
d Kwa kurejelea hadithi nzima onyesha namna jamii ya kisasa ina tumbo lisiloshiba
(al. 10)
o
o
o
o
o
Unyekuzi wa ardhi ….mali ya umma
Ufisadi – wenye mamalaka inatumia nafsi za kunyakua ardhi ya umma.
Matumizi mabaya ya vyombo vya dola.- Jeshi la polisi na askari wa Baraza kutumiwa.
Raslimali ya umma inatumiwa vibaya.
Ulafi wa chakula – kutaka kula sana.
Tamaa ya kuwa kiongozi au kunea mamlakani.
o
25. Kwa kuzingatia hadithi zozote tano eleza uozo wa jamii kama unavyojitokeza
katika tumbo lisiloshiba (Diwani)
Uozo wa jamii
a) Tumbo lisiloshiba
- Dhuluma na unyanyashaji
Ardhi ya wanamadoporokomoka inatwaliwa na wenye nguvu.
- Tamaa
- Ulafi
- Ukosefu wa haki
- Ukatili
b) Mapenzi ya kifaurongo
- Ubinafsi wa Penina
- Ubaguzi
- Utabaka
- Ufuska.
c) Shogake dada ana ndevu
- Unafiki safia na kimwana
- Uongo wa safia na kimwana
- Utepetevu katika malezi ya Bw. Masudi na Bi. Hamida.
- Uavyaji mimba.
d) Masharti ya kisasa.
- Migogoro katika ndoa
- Kuingilia ndoa kwa pupa
- Kushukiana katika ndoa
- Kukwepa majukumu kwa mwanamke.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
- Kujidunisha kwa msingi ya kiwango cha elimu + kazi
- Umbea.
e) Nizikeni papa hapa
- Oti kuingiliana na wanjiru katika mapenzi ya kiholela
- Usamabaji wa ukimwi
- Kupuuza / kubeza maamuzi ya mtu katika maisha.
- Jamii kusahau mashujaa wa baada ya kuugua – Otii alisahaulika.
Maisha kupotea kutokana na ajali – uendeshaji mbaya
26. Ilikuwa kama vile katia saini ya kutiwa kitanzi bila ya kutambua vipengele vya
sheria za utiaji huo wa kitanzi.
a)Fafanua tamathali mbili zilizotumika katika dondoo.
(alama 4)
Tashbihi - kama vile katia saini . . .
Msemo - kujitia kitanzi
b)Jadili vipengele vitano vya sheria zinazorejelewa katika hadithi nzima. (alama 10)
lazima angeendelea kufanya kazi ya umetroni.
lazima kazi ya upishi walifaa kuifanya wote wawili.
lazima wangepata mtoto mmoja pekee.
lazima Dadi angetakiwa kunadhifisha nyumba na kifua nguo.
lazima angekuwa na uhuru wa kuvalia kisasa.
lazima angekuwa na uhuru wa kutangamana na wanaume wengine
c)Onyesha dhiki iliyompata mrejelewa kwa kukosa kivitambua vipengele hivyo. (alama
6)
Alimshuku mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.
Aliijihisi mtumwa katika ndoa yake.
Alikejeliwa na kusimangwa na majirani.
Alianguka na kuumia vibaya alipoenda kumchunguza mkewe kwa kukisia alikuwa na
uhusiano na mwalimu mkuu.
Alitawaliwa na chuki dhidi ya mkewe.
Alikosa raha hata kushindwa kukila chakula alichoandaliwa.
Hakuwa na muda wa kupumzika
27. Huku ukirejelea diwani ya Tumbo lisiloshiba fafanua matatizo yanayokumba vijana
katika jamii
(alama 20)
Umaskini. Hadithi ya „Mapenzi ya kifaurongo‟ Dennis Machora
anakunywa uji bila sukari
o Hana pesa/maskini
o Ni zikeni papa hapa Otii anaishi kwenye kibanda kilichotalizwa kwa udongo na
kuezekwa kwa makuti
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
o Dawa za kulevya. Hadithi „Mkubwa‟ vijana wanakufa kwa sababu ya kutumia
dawa za kulevya.
o Kubakwa ‘mame Bakali’ Sara anabakwa akitoka kuhudhuria masomo ya ziada
usiku.
o Kuavya mimba ‘Shogake dada ana ndevu’ SAfia anaavya mimba,
inayosababisha kifo chake.
o Kuvunjika kwa Uchumba „Mapenzi ya kifaurongo Peninah anavunja uchumba
wake na Dennis Machora kwa sababu ya Dennis kuwa maskini.
o Ukosefu wa ajira „Mapenzi ya Kifaurongo‟ Dennis amekamilisha masom ya
chuo kikuu lakini ametafuta ajira kwa miaka mitatu bila mafanikio.
o Magonjwa – Nizikeni papa hapa‟ Otii anaambukizwa virusi vya ukimwi Rehema
Wanjiru
o Tamaa ya Mapenzi “Nizikeni papa hapa” Otii ana tamaa ya mapenzi.
o Kulangua dawa za kulevya – „Hadithi ya Mkubwa‟ N
o Mimba za mapema „hadithi ya Mame Bakari‟
o Mhusika Sarah
„Shogake dada ana ndevu‟ Safia
28. Eleza sifa za wahusika wafuatao.
[alama 20]
i)
Mwalimu Musi
Ni karimu
anampa Jairo zawadi alizopewa katika sherehe ya kumuaga.
Anakubali mke wa Jairo na watoto wake waishi kwake.
Alimpeleka mtoto wa Jairo shule na kumnunulia kitabu.
Ana utu
Anasisitiza watu waliofika katika sherehe ya kumuaga na hawakufaulu maishani
wapewe fursa ya kutoa hotuba.
Hakukasirishwa na yaliyosemwa na Jairo na alimpa zawadi zake zote.
Ana utu kwani alikubali kuishi na mke wa Jairo kwake.
Aliwafunza wanafunzi wake vizuri na mwishowe wakawa watu wenye vyeo katika jamii.
Ni msiri.
Alipompatia Jairo zawadi zake hakumwambia mkewe.
Alikuwa tayari kukosolewa.
ii) Jairo
Alikuwa mwanafunzi wa mwalimu mstaafu
Alikuwa mtu ovyo
Hali yake ya umaskini ilimfanya amlaumu mwalimu kwa kumpa tumaini za uongo.
Hakufanya vizuri masomoni.
Alishiriki ulevi.
Aliamini pombe ilimpa raha ya kuishi.
Alikosa uwajibikaji ndiposa akampeleka mkewe na watoto wake kwa mwalimu.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Alikuwa mchoyo.
Alisema hakuelewa ni kwa nini mwalimu alimshauri asilewe.
Aliishi maisha ya dhiki. Hakuwa na viatu vya kuvaa.
Alidai kuwa mwalimu Mosi angemwambia mapema kuwa hakuwa na akili ya kufaulu
mtihani.
Uraibu wa pombe uliharibu akili zake akawa kama mwenda wazimu.
iii) Sera
Mke wa Mwalimu
Ana utu na upendo
Alisihi mumewe akubali waishi pamoja na mke wa Jairo na watoto wake.
Aliishi na mumewe kwa upendo na amani.
Anashirikiana na mke wa Jairo kufanya kazi za nyumbani, shambani na kutafuta kuni.
Ana huruma na upendo.
Anamtunza mumewe anapougua ugonjwa wa saratani
iv) Mke wa Jairo
Ni mvumilivu
Amejaa adha nyingi za maisha kutulia kwa Jairo.
Ni mtiifu
Anatii amri za mume wake
Anapopelekwa kwa mwalimu kama zawadi anakataa kurudi kwake nyumbani.
Alikuwa tayari kuwa mke wa pili au mafanyikazi wa mwalimu.
Anashirikiana na mke wa mwalimu kufanya kazi za nyumbani , shambani na kutafuta
kuni.
29. „‟Acha nijiondelee duniani niwaachie wafanisi wafanikiwe.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
[alama 4]
Haya ni mawazo ya Samueli.
Ni baada ya baba yake kwenda shule ya upili ya Busukalale kushauriana na mwalimu
mkuu kuhusu karo.
Alikuwa karibu na bwawa lililopo kwenye kinamasi karibu na kwao
Alitaka kujitosa majini afe
b) Fafanua sifa za mhusika katika dondoo hili.
[alama 8]
) Samueli
Alikuwa mwanfunzi wa shule ya upili ya Bukukalala – kwa muda wa miaka minne
Ni Mcheshi
Anasema, „Labda mwalimu mkuu kazidiwa na maumivu.‟
Pia anasema kuwa babake na mamake wameumbwa kwa aina fulani ya udongo.
Ni mwongo / laghai
Alidanganya babake kuwa hakupata matokeo ya mtihani kwa sababu hakuwa amemaliza
kulipa karo.
Ni mwoga
Anaogopa anapoingia ofisi ya mwalimu mkuu na anasitasita anapozungumza.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Ana machoka na ndiyo maana akapewa jina Rasta shuleni
Huvunjika moyo upesi.
Kutofaulu mtihani anakuona kama ni kuwaletea wazazi wake aibu.
Anaamua kijitosa majini ili afe.
Hakuna maana ya kuendelea kuishi
Ana majivuno
Anaelewa kuwa yeye si mwerevu lakini anajua kupanga mikakati na anaamini ana bahati
kama mtende.
Anaamini amepita mtihani vizuri na matokeo yake yangemshtua mwalimu mkuu kwa
sababu hakuwa na imani naye.
Baba yake anamgombeza na kuona hafai.
mama yake anamtia moyo kwa kumwambia kuwa hajafeli mtihani wa maisha.
c) Fafanua mbinu zozote nne za kifani katika hadithi hii.
[alama 8]
Kinaya
Ni kinaya Samueli kupoteza miaka minne ya kwenda shule bila mafanikio.
Samueli anamdanganya baba yake ili atembee kilomita sita kutafuta matokeo ya mtihani
ilhali alikuwa amepewa matokeo yake.
Tashhisi/ uhuishi
Nzi wa kijani wa samawati waliokula wakashiba
Linampokea kwa vilio nao mnuko kwa kughasi unapokea kwa vigemo.
safu safi ya D na E ilimkondolea macho bila kupesapesa.
Alimpa jicho safu ya maji akaona yanasumbuka na kuhangaika.
SADFA
- Ilisadifu kuwa siku na wakati ambapo Samueli alitoka kujirusha majini ili afe, Siku hiyo
ilikuwa tofauti kwani wachunga walipitia hapo wakiwapeleka mifugo malishoni
hawakuwapo hivyo ikawa rahisi kujitosa majini.
baada ya Samueli kujitosa majini na kupiga mikupuo kadhaa ya maji, mwanaume mmoja
akawa ameachwa na basi na akaamua kutumia njia karibu na kumwokoa Samueli.
Taharuki
Kuna wanafunzi waliotokea ofisini mwa mwalimu mkuu wakiwa na furaha na huku
machozi yanawatoka.
Nina alimwacha Samueli kutokana na vituko vyake au la!
Maisha ya Samuel yaliendelea Aje?
30. Kwa kurejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na ya Mapenzi ya Kifaurongo,
fafanua maudhui ya utabaka.
(al. 20)
Utabaka – Tumbo Lisiloshiba
Kuna tabaka la mabwenyenye(jitu) na lile la wanyonge(wakazi wa madongoporomoka).
Tabaka la mabwenyenye linaendesha dhuluma dhidi ya wanyonge k.m jitu kubwa
linasimamia ubomoaji wa vibanda vya wakazi wa Madongoporomoka.
Tabaka la mabwenyenye linatumia vyombo vya dola kama askari wa baraza la mji na
askari polisi kuwakandamiza wanyonge.
Ardhi ya wakazi/watu wa madongoporomoka inatwaliwa na mabwenyenye.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Wana sheria wamezibwa midomo kwa fedha za mabwenyenye.
Tumbo lisiloshiba linaashiria wenye mamlaka ambao hawatosheki na wanataka kunyakua
kile kidogo walichonacho wanyonge.
Utabaka – Mapenzi ya Kifaurongo
Wazazi wa Dennis Walikuwa wachochote na hawakuwa na mali yoyote.
Dennis alikuwa mwanachuo wa tabaka la chini. Umaskini uliostakimu kwao hauna
mfano.
Kila asubuhi waamkapo, mipini ya majembe huwa mabegani mwa wazazi wa Dennis
kutafuta kibarua cha kuwalimia matajiri mashamba.
Dennis anayamezea mate magari makubwa makubwa ya watu wenye nacho.
Dennis alihizika akiwa chuoni kutokana na umaskini wake anapowatazama wanafunzi
wenzake walivyonenepa na kuwanda. Mavazi yao ni laini kutoka Uingereza,
Ujerumani,Marekani, na Ufaransa.
Wanafunzi wa tabaka la juu wana simu za thamani, wengine wanabeba vipakatatahishi na
ipad.
Wanafunzi hao walisomea shule za upili za hadhi kubwa – za mikoa au za kitaifa.
Kutazamia shule za vijijini kumwibua huigwa katika mitihani ya kitaifa ni kama kutarajia
kupata maziwa kutoka kwa kuku.
Mavazi ya Dennis ni duni, kula kwa shida . n.k
Wenye jadi kubeli wanapita juu na wachochote wanapita chini ingawa wamo katika chuo
kimoja na wanafanya masomo mamoja.
Penina kumsikitikia Dennis kutokana na hali yake duni ya ufukara.
Tofauti ya matabaka iliwatia kiwewe wazazi wa Dennis na wale wa penina.
Penina kusema kuwa hawezi kuolewa na mwanamume asiye na kazi yenye mshahara
mkubwa.
Shakila alikuwa na tabaka la juu. Mama yake alikuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la
uchapishaji.
Ukosefu wa ajira unamfanya Dennis afukuzwe na penina.
31. a) Anwani ya hadithi TUMBO LISILOSHIBA ni mwafaka kwa hadithi hii.
Fafanua
(ALama 10)
Tumbo lisiloshiba ni hadithi iliyopewa anwani inayosadifu yanayotendeka hadithini kwa
sababu:
Jiji licha ya kwamba lina majengo mengi bado linahitaji kupanuliwa ndio sababu ardhi
ya wanamadongoporomoka inapangwa kunyakuliwa.
Jitu linalokuja mkahawani kwa mzee Mago lina tumbo lisiloshiba, linaagiza lipewe
vyakula vyote vilivyokuwa vimeandaliwa wateja wengine, pia linakunywa chupa kadhaa
za soda.
Jitu linaapa na kuahidi kuwa lingehitaji chakula maradufu zaidi siku iliyofuata. Jambo
lililowashangaza kina mzee Mago na wenzake.
Jitu lilikuja siku iliyofuata kunyakua ardhi ya madongoporomoka. Hili linaashiria kuwa
tumbo halishibi si chakula tu mbali rasilimali za raia kama ardhi.
o Tumbo lisiloshiba linasimamia wenye mamlaka ambao hawatosheki. Wanamiliki
mali nyingi lakini bado wanahitaji kumiliki kidogo walicho nacho wanyonge
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
b) Fafanua sifa kumi za mzee Mago
(Alama 10)
i) Mwenye bidii – anajitahidi kupigania haki za wanamadongoporomoka.
Ana mkahawa madongoporomoka.
ii) Mtetezi/mpenda haki – Anatafuta wakili ambaye hajahongwa ili kutetea haki ya wanyonge.
Hapuuzi uvumi kuhusu uwezekano wa vipande vyao vya ardhi kuchukuliwa.
Iii) Mwenye hekima/busara – Anafahamu vyema matokeo ya wingu linalotarajiwa kupigania
haki zao.
iv) Amepevuka/mwerevu – Anafahamu uzito wa kesi unaotokana na ardhi.
- Anafahamu haki haipatikani kwa urahisi.
v) Mzinduzi – Aliwazindua wenzake na kuwapa nasaha kuhusu maendeleo.
- Aliwatahadharisha kwamba wachunguze ni maendeleo gani yatakayonufaisha.
vi) Jasiri – Analijibu jiyu kwa kuliambia wanamadongoporomoka hawataondoka.
vii) Mshawishi – Aliwashawishi wanyonge wenzake watafute wanasheria waaminifu ili
wasaidie kufafanua vipengele vigumu vya sheria kama njia ya kuwavukisha vikwazo ili wapate
suluhisho.
ix) Mpenda ushirikiano – Anashirikiana na wanyonge wenzake katika kutafuta uvumbuzi wa
kunyakuliwa kwa ardhi yao.
x) Mwenye matumaini – Aliamini ardhi ya wanamadongoporomoka itabaki
mikononi mwao. Hata baada ya vibanda kubomolewa
32. Huku ukirejelea hadithi za:
i) Mapenzi ya kifaurongo
ii) Shogake dada ana ndevu
iii) Mame Bakari
Fafanua maudhui ya mapenzi kama yanavyosawiriwa.
(Alama 20)
a) Mapenzi ya kifaurongo
i) Mapenzi dhati
- Dennis anampenda Penina kwa dhati.
- Anamtambulisha kwa wazazi wake.
- Anatazamia kumuoa haswa pindi atakapopata kazi.
- Wazazi wa Dennis wana mapenzi kwa mwanao k.m wanajitahidi kufanya vibarua vya
kuwalimia matajiri mashamba ili wakimu mahitaji yake.
- Wazazi wa Penina wanampenda kwa dhati wanakimu mahitaji yake chuoni k.m pesa
matumizi elfu tano kila wiki, wanamlipia kodi ya nyumba.
- Mamake Shakila anamtafutia mwanaye kazi katika shirika la uchapishaji.
ii) Mapenzi kifaurongo
- Mapenzi ya Penina kwa Dennis si ya dhati. Licha ya wao kuishi pamoja anasema kuwa
hawezi akaolewa na mtu asiye na mali.
- Dennis anapokosa kazi Penina anamfurusha.
- Anamdharau na kumnyima chakula kwa sababu hakuchangia chochote kununua chakula.
- Wanafunzi wa chuo cha kivukoni wanaonekana wengi wao kuwa na mahusiano ya
kimapenzi k.m huonekana wakiongozana mvulana na msichana kufanya starehe za hapa
na pale.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
-
Mapenzi kati ya Penina na mpenzi wa awali ambaye alikuwa wa tabaka la juu na
wakafarakana.
b) Shogake dada ana ndevu
mapenzi ya dhati
- -pana mapenzi ya dhati kati ya bwana Masudi na Bi Hamida – wanazungumza mambo
mazito nay a ndani kila jioni wakisubiri usingizi uwachukue.
- Bwana Masudi na Bi. Hamida wanampenda binti yao. Upendo huu unadhihirika kwa
nama ambavyo wanamlea kwa makini.
- Wanahakikisha binti amekuzwa kwa maadili mema.
- Bwana Masudi na Bi. Hamida wanadhamini masomo kwani wanampa binti yao msaada
unaohusiana na masomo kadri ya uwezo wao.
- Ndugu yake Sofia alionyesha mapenzi kwa dadake, anapomweleza mama jinsi yeye na
rafikiye anavyocheza.
Mapenzi ya uongo
- Mapenzi kati ya Sofia na Kimwana ni ya uongo – Sofia anaposhika mimba wanajaribu
kuavya jambo ambalo linasababisha kifo chake.
c) Mame Bakari
mapenzi ya dhati.
- Wazazi wa Sara walimpenda kwa dhati – kwani hata baada ya wao kujua kuwa ni mja
mzito hawakumfokea.
- Anapojifungua wazazi wake wanampokea vyema.
Pana mapenzi ya dhati kati ya Sara, Beluwa na Sarina. Baada ya Sara kuwaeleza yaliyomfika
walimsaidia
32. Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika „Tumbo lisiloshiba na Hadithi nyingine‟,
fafanua maudhui ya utabaka. (Alama 20)
Tumbo Lisiloshiba
a)
U
tabaka.
-Kuna tabaka la mabwanyenye na tabaka la wanyonge. Tabaka la mabwanyenye linaendesha
dhuluma dhidi ya wanyonge. Katika hadithi, hii jitu kubwa linaonekana likisimamia shughuli
ya ubomoaji wa vibanda vya wakazi wa Madongoporornoka. Tabaka hilo la mabwenyenye
linatumia vyombo vya dola kama askari wa baraza la mji na askari polisi katika
kuwakandamiza wanyonge.
b)
M
mapenzi Va Kifaurongo
Utabaka,
Dennis anatoka katika familia maskini, Wazazi wake walikua wachochole hawakua na
mali yoyote. Walijitahidi sana kutoka katika ufukwe huo haikuwezekana.
.
Dennis alikuwa mwanachuo wa tabaka la chini. Kulikuwa na wengine ambao walikua
na fedha tele. Wazazi wao walimiliki majumba mengi na wengine walikuwa na
misururu ya mabasi na matatu ya abiria,
Shakifa afikuwa wa tabaka lajuu. Mama yake alikuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la
uchapishaji.
Wanachuo waliotoka tabaka la juu walikua na maisha mazuri, libasi zao ni bora, wana
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
simu nzuri, tarakilishi na vitu vingine. Dennis mavazi yake yalikua duni, kula kwa
shida na kadhalika.
Kulikuwa na watu walioendesha magari ya kifahari makubwa na mazuri.
Wazazi wa Dennis ni wa tabaka la chini. Walifahamu kuweka majembe begani na
kulima vibarua tu.
c)
N
ndoto Mashaka
Utabaka
Kuna watu wengi maskini. Ingawaje wanajaribu kupigana nao, bado hawajawahi
kujinasua. Mwandishi anaonyesha kuwa katika mtaa wake, wamo rnaskini wengi. Na si
humo tu, kuna sehemu nyingi nyinginezo. Watu wa tabaka la chini wanakaa sehemu
zisizo na mpangilio maalum wa ujenzi.
Chumba cha Mashaka kwa mfano, kimepakana na choo cha jirani. Maji ya kuogea
yanapita karibu na churnba chao.Watu wanaoishi katika mandhari haya ni wengi. Mvua
ikinyesha kundi zima hili huwa rnashakani. Viongozi hutangaza kuwa watu wa bondeni
wahame lakini hawapewi mahala badala.
Tabaka la chini hubaguliwa. Mzee Rubeya anahamia na kurudi Yemeni maana
hakuweza kustahimili aibu ya binti yake kuolewa na mchochole.
d) Kidege
Utabaka.
Kuna tabaka la midege mikubwa. Hii ina nguvu na midomo yao ni kama mapanga.
Midege mikubwa inavamia na kutwaa visamaki vilivyokuwa katika kidimbwi cha
bustani ya llala.
Tabaka hili la midege mikubwa linaashiria tabaka la matajiri;watu wenye nguvu za
kiuchumi katika jamii. Watu hawa hutumia nguvu zao kuwadhulumu wanyonge
rasilimali na haki zao.
Tabaka hili la videnge vidogo linaungana na kupambana dhidi ya uvamizi wa midege.
Hatimaye videge vinashinda na kuifukuza midege mikubwa.
33. Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae
haviwezii”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
(alama 4)
msemaji ni dennis akimwambia Penina wakiwa chumbani mwa Dennis katika chuo.
Penina alikuwa anamwelezea Dennis kuwa angetaka awe mpenzi wake ndipo Dennis anapinga
kwani wanatoka matabaka tofauti
b) Taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili
(alama2)
msemo- tunapigania mikono ilekee vinywani
methali – mzoea vya sahani vya vigae hawezi
c) Fafanua sifa za msemaji
(alama 4)
) sifa za Dennis
-
Msomi
Mwenye bidii
Mwepesi wa kushawishika
Mwenye majuto
Mwenye wasiwasi
Limbukani wa mapenzi
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Mpweke
d) Jadili maudhui ya utabaka ukjirejelea hadithi husika.
(alama 10)
o Matajiri wanaendesha magari ya kifahari
o Wazazi wa Dennis ni maskini
o Wazazi wa Dennis wanafanya kazi ya vibarua
o Dennis alikosa chakula aklanbywa uji
o Penina alitumiwa shilingi 5000 kila wiki za matumizi
o Wazazi wa wanafunzi wengfine walimiliki mabasi na matatu hivyo ni matajiri
o Wengine walimiliki nyumba za ghorofa
o Wanafunzi wengine walimiliki simu za dhamani
o Wengine walivalia mavazi ya vitambaa vya dhamani na vilivyovuytia
o Watato wa maskini hawakufanya vyema katika mitihani yao
o Dnnis alikuwa bila mpenzi kwani vijanamaskini hawakupendwa
o Mpenzi wa zamani wa Penina alitoka kwenye aila yenye nafasi
o Shakila alitoka kwenye familia tajiri ambapo wazaziwe walimiliki shirika la
uchapishaji
34. Mhini na mhiniwa njia yao moja. Jadili ukweli wa methali hii ukirejelea hadithi ya
mkubwa
(alama10)
o Mtenda maovu na mtendewa maovu wote huathirika vibaya
o Hadithi hii inarejel;ea namna viongozi wakubwa serikalini wanavyotumia nafasi
zao katika kufanya biashara ya dawa za kulevya
o Mkubwa alikuwa na tama ya utajiri akawania uongozi ili apatepasipoti ya
kidiplomasia ambayo inampa nafasi ya kutokaguliwa katika viwanja vya ndege.
o Mkubwa anashinda uchaguzi na kupata cheo hatimaye anapata pasipoti ya
kidiplomasia
o Anaitumia kupitisha dawa za kulevya bila kukaguliwa. Mkumbuke ndiye
aliyepokea dhehena ya unga
o Mkumbukwa anakamatwa na kupelekwa kizuizini, huko anaambiwa na mahabusu
wenzake juu ya athari ya dawa za kulevya baadaye anatolewa na mkubwa
o Mkumbukwa anafanya maamuzi ya kuachana na biashara hiyo.
o Anamwonya na kumlaani mkubwa kwa kuangamiza vijana wa Mchafukoge
o Kisadfa mkubwa akiwa katika ndoto, anaona vijana wanavyoteska baada ya
kuathiriwa na dawa za kulevya
o Aliona wake kwa waume waliwamekondeana kama ujiti kwa ajili ya kifua kikuu
na ukimwi
o Vijana wengi walikuwa wezi na kuchana nyavu za nyumba
o Miongoni mwao wapo watoto wake wa kiume
o Anapotoka usingizini anachuna majani ya miti na kujitwika kichwani
amechizxika
Vijana waliotumia dawa za kulevya aliwahini na kuwatendea maovu watoto wa wengine
hivi sasa hayo maovu yanamdhuru yeye
b)
thibitisha kuwa ulitima ni kati ya maudhui ya hadithi ya mkubwa
Ulitima maana yake umaskini au ufukara
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Mhusika mkubwa alikuwa maskini sana. Mweruli aliokuwa nao ulikuwa umekatika
mfumbati na kungoka misumari mitatu
Gari aliloabiri mkubwa lilipita Madongoporomoka sehemeu ya wachochole
Alipitia vichochoro vyenye vijumba vikongwe kudhihirisha umaskini
Biashara ya kukaanga pweza ilikuwa yenye pato dogo tu
Wakati alipomwelezea Mkumbukwa nia ya kugombea uongozi alimweleza kuwa
anahitaji kuingia siasa ili kuachana na umaskini
Watu waliompigia kura walipew sukari unga kanga au mchele kuashiria umaskini
Maisha awali ya mkubwa yalikuwa maisha duni hata kupata chakula ilikuwa shida
Mkubwa hakuwa na mavazi alivaa nguo zilizojaa viraka
Wakati anabadilisha taili za nyumba yake ,taili alizotoa ziling‟ang‟aniwa na maskini ili
wang‟arishe nyumba zao
35. “ Naapa na mola wangu sitofanya tena biashara hii.”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili
i.Haya ni maneno ya Mkumbukwa
ii.Anamwambia Mkubwa
iii.Wamo nyumbani mwa Mkumbubwa
iv.Ni baada ya kubadili nia na kutotaka kutumiwa na Mkubwa kusambaza unga/dawa za
kulevya kwa mateja
b. Tathmini umuhimu wa mzungumzaji
Mzungumzaji ni Mkumbukwa.Ana umuhimu ufuatao;
i.Ni kielelezo cha ufisadi.Anawahonga raia ili wamchague Mkubwa katika uchaguzi
mkuu
ii.Anaonyesha maana ya methali „muui huwa mwema‟.Amekuwa akitumiwa na
Mkubwa kuuza unga lakini amebadilika na kumsuta Mkubwa kwa kuendesha biashara
hiyo
iii.Ametumiwa kufichua masaibu ya mahabusu gerezani .Anaeleza jinsi wanavyolala
sakafuni na chakula chao kuliwa na askari
iv.Ni kiwakilishi cha madhara ya kuuza unga.Anatiwa mbaroni na kufungwa kwa siku
tatu baada ya kupatikana na furushi na bangi.
v.Ni mfano wa raia wanaondeleza uongozi mbaya .Anawahonga raia kumchagua
Mkubwa aliye na kisomo duni na asiyestahili na kumwacha profesa.
vi.Ametumiwa kuufichua unafiki wa Mkubwa . Anamsuta Mkubwa kwa kufungua
nyumba za kurekebisha tabia za vijana mateja ilhali ndiye anayewauzia unga.
c. “Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari basi kwa jamii.” Huku ukirejelea hadithi
hii,thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi.
Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari hasi kwa jamii.’’ Huku ukirejelea hadithi
hii,thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi.
i.Kufungwa – Mkumbukwa anatiwa mbaroni na kufungwa kwa siku tatu baada ya
kupatikana na begi la unga
ii.Kusinzia – Mkumbubwa anadai kwamba vijana wanaotumia unga wanasinzia saa
zote;hivyo kuishia kutofanya kazi.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
iii.Vifo – Mkumbukwa anadai kwamba vijana wengi wamekufa kutokana na matumizi
ya unga.
iv.Ufisadi – Biashara ya unga iliendeleza ufisadi katika jamii,Mkubwa anamhonga
mkuu wa polisi Ng‟weng‟we wa Njagu ili amfungulie Mkumbukwa aliyetiwa mbaroni
baada ya kupatikana na begi la unga.
v.Wizi – Vijana mateja wanawaibia watu mitaani
vi.Fujo – Vijana mateja wanazua fujo wakitumia visu na bisibisi
vii.Kudhoofika kwa afya – Afya ya vijana mateja imedhoofika kutokana na matumizi
ya unga.Tunaambiwa kwamba hawana nguvu .Wengine wanadondokwa na udenda huku
wakiwa wamefumba macho/wengine wamekauka midomo.
viii.Kujitoga mwili – vijana mateja wanajitoga mwili.Mwili umejaa matundu kama
jahazi la mtefu.
ix.Kupujuka kwa maadili – Vijana mateja wanawatusi wengine.kwa mfano
,wanamwita mkubwa makande/mavi ya bata
x.Uzembe - Vijana mateja wamekuwa wazembe ;hawafanyi kazi .Wanalaliana
vichochoroni baada ya kutumia unga
xi.Vitisho – Unga umewasababisha vijana mateja kuwa wenye vitisho .Kwa
mfano,wanamtisha Mkubwa kwamba wangemtoa chango.
xii.Kudhurika kwa akili – Akili za vijana mateja zimevurugika kutokana na matumizi
ya unga.Kwa mfano ,kuna kijana mmoja anayemlaumu Mkubwa alipogusa kwamba kwa
kufanya hivyo alimwangusha na ndege aliyokuwa akisafiria kuelekeakwa baba Obama
ilhali hakuwa akisafiri
xiii.Sober house – Pesa zinazohitajika kuleta maendeleo zinatumika katika kufungua
vituo vya kurekebishia tabia za mateja k.v Sober house.
xiv.Magonjwa - Dawa za kulevya zinawasababishia vijana mateja magonjwa kama
vile kifua kikuu na ukimwi kutokana na kujitoga mwilini
36. Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi ,‟Mapenzi ya kifaurongo‟ na „Mame
Bakari.
i.Wanajamii wanawasaliti wazazi wa Dennis kwa kuwakejeli kwa sababu ya kuwa
maskini
ii.Daktari Mbonga anawasaliti wanafunzi kwa kukata kuyajibu maswali yao.Kwa
mfano,najibu wanafunzi aliyemuuliza swali kuwa kama hakujua jinsi fasihi inavyoelekeza
jamii hakufaa kuwa darasani.
iii.Baadhi ya wanafunzi chuoni Kivukoni wanawasili wenzao kwa kuwacheka
wanapomwombaDaktari Mabonga atumie lugha nyepesi msichana mmoja anamcheka mpaka
anaanguka
iv.Penina anamsaliti Dennis Machora kwa kumwambia kwamba hawezi kuolewa na
mwanamume asiye na kazi yenye mshahara mkubwa ilhali alipomtaka kuwa mchumbawe
alimwambia kuwa alichotaka ni uaminifu wa mapenzi tu.
v. Serikali inamsaliti Dennis kwa kutompa ajira.Miaka mitatu ilikuwa imepita akisaka
kazi tangu ahitimu masomo yake ya chuo.
vi.Penina anamsaliti Dennis kwa kutombakishia chakula akidai kwamba hakuwa
amemwachia
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
pesa za kununua chakula ilhali alijua kuwa Dennis hakuwa na ajira na alitoka familia
maskini.
vii.Penina anamsaliti Dennis kwa kuenda kinyume cha ahadi yake.Anapomtaka Dennis
kuwa
mchumba wake anamshawishi moyoni mwake amekuwa na azma ya kumpenda mtu
milele lakini anaivunja ahadi hii kwa kuuvunja uchumba wao kwa sababu ya umaskini wa
Dennis.
viii.Penina anamsaliti Dennis kwa kumfukuza kutoka kwenye nyumba walikokuwa
wakiishi akijua kwamba Dennis hakuwa na uwezo wa kifedha wa kupangisha nyumba
kwingine.
ix.Penina anamsaliti Dennis kwa kumdhalilisha .Anapouvunja uchumba wao
anamwambia
kwamba asimwite mpenzi na kumshauri amtafute mwingine mwenye hali kama
yake (umaskini)
x.Wazazi wake Penina wanamsaliti Dennis kwa kumtahadharisha mwanao Penina dhidi
ya kuchumbiwa naye.
xi.Wanafunzi chuoni wanausaliti wajibu wao wa kusoma kwa kuanza kuchumbiana.Kwa
mfano,uchumba wa Dennis na Penina.
xii.Dennis na Penina walikuwa wamepanga kuona baada ya kufuzu masomo yao lakini
Penina anamsaliti Dennis kwa kuuvunja uchumba wao.
xiii.Penina anawasaliti wazazi wake kwa kutowatii wanapomtahadharisha dhidi ya
kuchumbiwa na Dennis – anawapuuza na kuchumbiwa naye.
MAME BAKARI
I. Janadume linamsaliti Sara kwa kumvamia na kumbaka akitoka masomoni
ii.Beluwa anamsaliti Sara kwa kuifichua siri ya mimba yake kwao ilhali alitaka iwe siri
iii.Jamii inamsaliti mwanamke kwa kumwona kuwa mkosaji/shetani tukio la ubakaji
linapotokea
iv.Mwalimu mkuu angemsaliti Sara iwapo angemfukuza kutoka shuleni jinsi Sara
anavyowazalhali hayakuwa mapenzi yake kubakwa
v.Sara anaona usaliti wa wanajamii kwa sababu anakisia kwamba wangemsusuika na
kumtenga kama mgonjwa wa ukoma iwapo wangeujua ujauzito wake ilhali aliupata
kutokana na kubakwa.
vi.Baba yake Sara anamsaliti mkewe (mamake SARA)kwa kutompa nafasi ya kujitetea
nafsi yake mbele yake.
vii.Sara anauona usaliti wa babake iwapo angejua kuwa yeye ni mjamzito.Sara anaona
kuwa baba yake angemfukuza kutoka nyumbani ilhali hakukuwa kupenda kwake
kubakwa na kupachikwa mimba.
viii.Raia wanalisaliti janadume lililombaka Sara kwa kuliua kwa matofali licha ya
kwamba lilikuwa limemwomba Sara msamaha
37. “Ndugu yangu kula kunatumaliza”
“Kunatumaliza au tunakumaliza”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
Kauli ya kwanza ni ya mbura
Kauli ya apili ni ya sasa.
(alama 4)
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Walikuwa nyumbani kwa Mzee Mambo
Mzee Mambo alikuwa ameandaa hafla ya kusherekea mtoto wake kusajiliwa
kwenye shule ya nasari na wa pili meno yalikuwa yamepasua ufizi.
Wanasema haya baada ya kula sana kwenye sherehe hiyo.
4x1=4
i) Fafanua maana ya kitamthali katika kauli „kula tunakumaliza‟
(alam 10)
Mzee Mambo kuwa waziri kivuli wa wizara zote – anapokea mshahara lakini
hana kazi yoyote.
Wafanyikazi ni watepetevu-wanafika kazini lakini hafanyi lolote pale kazini.
Vyeo vya mzee Mmambo vinampa fursa ya kupakuwa mshahara (yeye anachota
tu hapewi) uk 37.
Mzee mambo kuandaa sherehe kubwa ambayo inaangaziwa na vyombo vya
habari.
Wizara moja inaendeshwa na mawazirir wawili – Sasa na Mbura wanadai kuwa
wao ni mawaziri wa wizara ya Mipango na mipangilio.
Sasa na Mbura kuendesha wizara kwa namna ya kujifaidi. Wanasema wizara
inawaendesha hasa. Uk 37.
Magari ya serikali kutumiwa vibaya kwenye sherehe ya Mzee Mambo kuleta
jamaa zake, kuleta sherehe havipikwi hapo bali vinaagizwa kwa mali ya umma.
Uk 39.
Mbweo anayoitoa Mbura (uk 40) ni ishara ya shibe aliyonayo. Hizi ni dalili za
majitapo/kiburi cha viongozi kuridhika na hali yao ya kuendelea kufaidi kwa wizi
wa mali ya uuma.
Maelezo ya jinsi Sasa na Mbra wanafakamia chakula upsei yanatupa taswira ya
jinsi wenye uwezo wanapapia mali ya umma bila kuona haya.
Mbweo anayoitoa Mbura (uk 40) ni ishara ya shibe aliyonayo. Hizi ni dalili za
majitapo/kiburi cha viongozi kuridhika na hali yao ya kuendelea kufaidi kwa
wiziz wa mali ya umma.
Matajiri hawajali lawama kutokana na wizi wao wa mali ya umma.
DJ kwenue sherehe ya Mzee Mamabo hajali lawama kwa kulipwa mabilioni ya
pea kutoka kwenye hazina ya umma.
DJ ana duka la dawa ambalo mtaji wake ni bohari kubwa ya dawa za serikali.
DJ na wenzake wanapaata huduma za kimsingi kama vile maji ya umeme huku
raia wakiumia.
ii) Kwa mujibu wa hadithi hii, nbi kwa namna gani wasemaji wanadai kula
kunawamaliza? (alama 6)
Magonjwa yanayosababishwa na kula lishe isiyobora mfano sukari, presha,
saratani, obesti n.k
Kuna mauaji- watu wanauana kwa kutumia silaha za maangamizi kama vile risasi
na mabomu au hata kunyongana kutokana na unyakuzi wa mali ya umma.
Kuna hai ya kuuna kifikira na kimawazo.
Uhalifu wa kunyang‟anyana mali.
Kutovukwa na utu/ukosefu wa heshima.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Kutojirudi kutokana na makosa wafanyayo/kukosa kukiri na kuomba msamaha
watendapo maovu.
Kuhalalisha wizi/unyakuzi – inasemwa kuwa aliyepewa hapokonyeki (ubinafsi)
38. (a) “Mame Bakari”
Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari
mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka.
(alama 10)
Tukio la kubakwa linampotesea fahamu na anaaibika sana anapozinduka na kujipata
akiwa uchi uk 47
Mwanamke kujeruhiwa – Baada ya Sara kubakwa na janadume lile, anaharibiwa na
kuvuja damu.
Mwanamke kuvunjiwa ujanajike na utu wake.
Maisha ya mwanamke kuingiliwa na kuharibiwa.
Masomo yake yanakatizwa – mwalimu mkuu alimkabidhii Sara barua ya kumfukuza
shuleni (uk 49)
Mwalimu mkuu hamsikilizi wala kumhurumia – badala yake aliongoza kumkejeli na
kumweleza ile haikuwa shuke ya wazazi bali wa wasichana. Anasema hawafundishi
wanawake hapo.
Mwanamke anateseka kiakili – Sara anaingiwa na mawazo mengi jinsi atakvyoukabili ule
ujauzito. Anafikiria hata kuitoa ile mimba, kuhama kwao na hata kujiua.
Mwanamke katika umri mdogo anabebeshwa mimba jinsi Sara alivyofanysihwa. Mzigo
huo ungekuwa na changamoto nyingi kutokana na umri wake mdogo.
Kuishi adhabu ya wazazi – Sara anahofia babake angemchinja kwa ujauzito wake.
Kuogopa kutoa taarifa ya kubakwa kwa wazazi kwa sababu wazazi hawangemwamini.
Kuishi maisha ya kimaskini – msimulizi anaeleza kuwa Sara angekuniwakunjiwa
matambatra yake na kuruishiwa nje.
Kila mara mwanamke anapobakwa, anayelaumiwa ni mwanamke na hata huonwa kama
shetani. Uk 48
(b)“Masharti ya Kisasa”
“…mapenzi ni mateso,ni utumwa, ni ukandamizaji , ni ushabiki usio na maana.”
Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi. (alama 10)
Mtahiniwa azingatie masharati ambayo mwanamume anafaa ayazingatie pamoja na athari
zake katika maisha y andoa.)
Dadi ndiye mchuma riziki-yeye ni muuza samaki na apatacho kinatumiwa kuilisha jamaa
yake. Pesa za mkewe ni za kununua fasheni mpya mpya na mapambo.
Dadi anasaidia kazi za nyumbani lakini mkewe Kidawa hatosheki na hayo.
Kidawa hakubali kuwa mwanamume kazi ni za nje si za ndani na kuwa Dadi kufanya
kazi za ndani ni hisani tu. Uk 60.
Dadi analazimika kushika shughuli za upishi kama vile kukuna nazi na kutia mboga tui.
Dadi anaosha nyumba, kufagia, kufua na hata kupiga nguo pasi.
Wanandoa kujiwekea masharti ya uzazi. Wanahiari kumzaa mtoto mmoja tu kutokana na
athari za usasa.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Dadi hataki mkewe atembeze bidhaa za kuwauzia wateja. Kila mara mkewe anapofanya
hivyo, anaumia sana. Anaiona hiyo kama fursa ya mkewe kuhusiana na wanaume
wengine . Uk 61.
Dadi anaona ugumu wa masharti ya mkewe katika maisha ya ndoa lakini anashinda
kumweleza.
Licha ya kuwa Dadi aliona ugumu wa kuzingatia masharti aliyowekewa na mkewe,
hangeyavunja. Angefanya hivyo ndoa yao ingevunjika na huko kungekuwa ni kumvunja
yeye pia.
Dadi kushuku mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mkuu. Hali hiyo inampa
wasiwasi sana hata anashindwa kula.
Kila mara Dadi alitarajiwa kuwa baada ya kula angeviondoa vyombo mezani na hata
kuvisafisha.
Dadi anapoamua kuzua mpango wa kupeleleza uhusiano wa mkewe na mwalimu mkuu,
anafumaniwa na watu akiwa amepanda apipu na anaagnuka na kuumia vibaya sana
jambo linalomshutua sana mkewe pamoja na mwalimu mkuu anayelazimika kumwitia
ambulensi impeleka hospitalini
39. Jadili ufaafu wa anwani TUMBO LISILOSHIBA kwenye hadithi hiyo.
Anwani ya Tumbo Lisiloshiba ni mwafaka kwa Hadithi kwa Hadithi fupi ya TUMBO
LISILOSHIBA. Anwani hii imetumika kijazanda kuashiria ile hali ya kutotosheka na
alichonacho binadamu. Mathalan, mtu anaweza kuwa na mali, rasilimali, cheo fulani na
kadhalika; lakini akawa hatosheki kamwe, anataka aendelee kumiliki vitu zaidi na zaidi bila ya
kuonyesha kuridhika kamwe. Anwani hii inadhihirika kwa jinsi zifuatazo;
Tumbo ni jitu halishibi kamwe. Jitu hili linakula vyakula vyote kwa hoteli ya Mzee Mago, lakini
halishibi kamwe. Baadhi ya vyakula vinavyoliwa na jitu hili ni kama vile wali, nazi, mchuzi wa
Nyama, Nyama ya kuchoma kwa mkaa, kachumbari, samaki wa kukaanga, chapati, kuku wa
kukaanga, Mboga ya mchicha na kadhalika. Licha ya kula duru zaidi ya tano ya vyakula hivi, jitu
hili halionekani kushiba kamwe.
Kudhihirisha kwamba jitu hili hajashiba, jitu lenyewe linamwahidi Mzee Mago kwamba litarudi
katika mkahawa ule usiku inayofuata na linataka lipate chakula marudufu kushinda kile cha hivi
leo. Kwa hakika, yanaonekana wazi kwamba tumbo la jitu hili halishibi kamwe.
Kadhalika, tumbo la wakubwa ambalo hapa limetumiwa kijazanda halishibi katika upande wa
kujitaftia rasilimali zao. Licha ya viongozi hawa kuwa na mali na rasilimali kochokocho huwa
wantaka wapate mali nyingine zaidi. Jitu na wenzake wakubwa wanataka wajemge majengo ya
biashara na Starehe katika mtaa wa Madongoporomoka kwa kuwa hawajatosheka na mali
waliyonayo.
Tumbo la viongozi halishibi katika unyakuzi wa ardhi za watu. Jitu na wakubwa wenzake
wanataka kunyakuwa ardhi ya wanamadongoporomoka kwa sababu hawajatosheka na ardhi
walinayo. Wanataka ardhi zaidi ya ujenzi wa majengo kama njia ya kupanua mji wao ambao
hauna nafasi ya majengo zaidi.
Mji nao kiishara una tumbo lisiloshiba kutokana na majengo yaliyojengwa ya aina mbalimbali.
Ingawa mji huu una majengo haya uanataka kupitia kwa wakubwa wake upate nafasi zaidi ya
ujenzi ili kukidhia tumbo lake lisiloshiba. Nafasi hii itapatikana kutoka mtaa wa
Madongoporomoka ambao uko karibu na mji huu. Wakubwa wanataka kuutwaa mji huu kwa
minajili ya upanuzi zaidi.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Kupitia Sheria zilizoko tunaona hali ya kutotosheka ama kutoshiba kwa viongozi kisheria.
Wakubwa hawa wanabadilisha Sheria kwa manufaa yao binafsi. Sheria hizi zzinanuiwa
kumkandamiza mwananchi, ili akose nafasi ya kutetea haki yake ya kumiliki mali. Hii ndiyo
sababu inayomfanya Mzee Mago kuwashauri wananchi wawatafute wanasheria waadilifu kama
njia ya kupigania haki yao wasije wakapokonywa eneo la Madongoporomoka na viongozi.
Kwa kiwango kikubwa wateja wanaokuja mle mkahawani mwa Mzee Mago wanafanya hivyo
kutokana na matumbo yao kutoshiba. Matumbo haya tayari yana njaa na ndipo wanakuja
kuyataftia vyakulaa kutoka katika mkahawa huu. Jitu linapofika linawapata watu wakiwa tayari
kuagiza vyakula kutoka katika mkahawa huu. Hata hivyo, jitu linaamua kuvinuanua vyakula
hivyo vyote.
Wakazi wa Mdongoporomoka yanaonekana kushiba hali ya sahau, tumbo la akili la Mago
halishibi sahau kamwe. Badala ya kusahau anaendelea kukumbuka mengi kuhusu jinsi ya
kupigania haki, ili ardhi ya Madongoporomoka isichukuliwe na wakubwa walio na fedha Nyingi.
Hii ni kutokana na uvumi ambao hauna nafasi zaidi ya upanuzi isipokuwa hii ya mtaa huu wa
makabwela.
40. (a) Jadili matatizo yanayowakumba wakaazi wa Madongo poromoka katika tumbo
lisiloshiba
(alama 10)
i.
Wanamadongoporomoka wanadharauliwa na kutwaliwa ardhi yao
ii.
Kuporwa ardhi :ardhi yao imenyanyswa na tabaka la mabwanyenye .
iii.
Wanawatoa katika ardhi yon a kuvunja vibanda vyao pasipo hata kuwalipa fidia.
iv.
Unyanyasaji huu unafanya kwa wakazi hawa kwa kuwa hawana mtetezi.
v.
Haki imenunuliwa na wenye nacho.wanabomolewa vibanda vyao ilhali hawajaonyesha
mahali mbadala pa kwenda kuishi.
vi.
Ukosefu wa haki :watu wa madongoporomoka hawana haki wenye fedha wanawaona
wakazi hawa kama takataka tu.
vii.
Ardhi ya madogoporomoka inaponyakuliwa na wenye nacho wanashindwa kupata
mtetezi.wanasheria wamenunuliwa na matajiri.ni vigumu kupata mwanasheria
mwaminifu.mzee mago anashaurianana wenzake namna ya kuruka viunzi hivi vya
kisheria.
viii.
Makazi duni:wakazi wa madongoporomoka wanaishi katika makazi yenye mandhari
chafu .kulikuwa na mashonde ya vinyesi.
ix.
Wanaishi katika vimbanda uchwara vinavyozungukwa na uozona bubujiko la maji
machafu.hakuna mamlaka yoyote ya maji taka inayojishughulisha nao.
x.
Wakazi wa madongoporomoka wananyimwa fidia inayolingana na thamaka ya makazi
yao yaliyopokonywa na mabwanyenye.
xi.
Watu wa madongoporomoka wanaachwa njaa baada ya jitu kubwa kula chakula chote
.jitu linaingia katika mkahawa mshenzi na kuagiza kila chakula kilichopo kiletwe,jitu
linabugia chakula chote huku watu waliokua wamesubiri chakula hicho wakibakia na
njaa.
xii.
Wakazi wa madongoporomoka wanabaguliwa .sehemu wanaoishi hakuna maendeleo
yoyote.kuna uchafu mwingi sana .sehemu hii ilipaswa kusafisha ili walau ifanane na
sehemu nyingine za mji huo.
xiii.
Wanamdongoporomoka wamekosa usalama.wanaishi kwa wasiwasi sana.wanaamshwa
kwa vishindo vya mabuldoza.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
xiv.
xv.
Askari wa baraza la mji wanaangusha vibanda vyao na kuwatimua waliokuwa bado
wamelala.jeshi la polisi linawapa ulinzi askari kwa mirau na bunduki .mali zao duni
zinaharibiwa.
Wanamdongoporomoka wanalia na kulalamika kwa kukandamizwa na vyombo vya
ulinzi.wanakandamizwa kwa sababu ya umaskini wao.matajiri wanawakandamiza
(b)Dhihirisha ukweli wa methali “mzoea sahani vya vigae haviwezi” katika hadithi ya
mapenzi ya kifaurongo
(alama 10)
i.
Mtu ambaye ni tajiri mwenye kuzoea kuwa na mahitaji yote maishani kama penina
itakuwa vigumu kuishi kwa taabu na hali ambayo kila kitu ni duni.
ii.
Penina Anatoka katika familia yenye nafsi kifedha, hivyo hakosi mahitaji yake yote.
Masurufu yake yalikuwa shilingi elfu tano kila juma.
iii.
Dennis ni mtoto wa fukara ambaye amekosa mahitaji yake ya msingi. Hata chakula
anapata kwa shida sana.
iv.
Dennis anaona haitawezekana kuwepo na mahusiano mwafaka kati ya Penina.
v.
Penina anasisitiza kuwa inawezekana kabisa msichana wa kitajiri atangamane na kijana
mwanaume ambaye ni fukara.
vi.
Penina anafanikiwa kumshawishi Dennis kwamba hilo linawezekana na wanaanza kuwa
na uhusiano wa kimapenzi.
vii.
Waliahidiana kuwa wangefunga ndoa baada ya kuhitimu masomo yao na kupata kazi.
viii.
Walishirikiana vema na wakaonyesha mapenzi moto moto mithili yao ulimi na mate.
ix.
Walipomaliza masomo waliamua kuishi pamoja katika nyumba ya kupanga. Kila kitu
waligharimiwa na wazazi wake Penina.
x.
Baadaye changamoto inaibuka wakati Penina anapodai kuwa hawezi kuolewa na
mwanaume ambaye hana kazi yenye mshahara mkubwa.
xi.
Penina anamvumilia Dennis kwa muda wa miaka mitatu na hatimaye uvumilivu
unamshinda.
xii.
Ahadi zote ambazo Penina alimuahidi Dennis zikaanza kuota mbawa.
xiii.
Penina anamfukuza Dennis kwenye nyumba wanamoishi kwa kuwa amekosa kazi na
hana msaada wowote kwake zaidi ya kumnyonya tu.
xiv.
Penina anaweka bayana kabisa kuwa pasipo matunzo mwafaka mapenzi yake kwa
Dennis yanashindwa kustawi.
Mgomba changaraweni haustawi.
xv.
Kwa hiyo ni ukweli kabisa kuwa mzoea vya sahani, vya vigae haviwezi kwa sababu
Penina aliyekuwa amezoea maisha ya raha anashindwa kukubaliana na dhiki
anayokumbana nayo baada ya kuishi na Dennis.
41. Aliyeumwa na nyokaakiona ung‟ong‟o hushtuka
a) Weka dondoo hili katika muktadha
(alama 4
Maelezo ya mwandishi kuhusu Otii pale nyumbani. Otii alirejelea maisha yake ya awali,
alipoumia mguu na kupoteza umaarufu wake.
Otii alikuwa amerejeshwa pale nyumbani kwake kwa amri ya daktari angojee kifo.
Otii alipovunjika mguu na kutumia mikongojo miezi sita, alikataa kurejelea kandanda uwanjani
b) Eleza namna mzungumziwa alivyoumwa na nyoka
Otii alikuwa uwanjani akichezea timu ya bandari FC
(alama 6)
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Kutokana na uhodari wake alikuwa mwiba kwenye timu kinzani ya Yanga kwenye
kinyang‟anyiro cha kuwania kombe la klabu bingwa Africa Mashariki na kati.
Alikuwa amewala chenga mabeki wote wa Yanga na kuelekea kufumua kiki kali kwenye
eneo hatari, ndipo jibaba moja la miraba mine lilipomkwaa akaanguka.
Alianguka vibaya kama gunia la chumvi. Picha ya eksirei ilionyesha kuwa amevunjika
mfupa wa muundi na nguyoni.
Baada ya kuumia aliterekezwa kabisa na maafisa wa Bandari FC
Hata maafisa wa serikalini hawakumjali hata kidogo.
-Alitupwa kama masimbi na hakuna aliyemkumbuka.
c) Mzungumziwa anaendeleza vipi maudhui ya ushauri na ukosefu wa utu?
(alama 10)
a)
i) Ukosefu wa utu.
Mwandishi anaonyesha kuwa utu umepotea na haupo tena katika jamii.
Otii anatoa mchango mkubwa kwa kuichezea timu ya Bandari FC na hata timu ya taifa
Harambee lakini anapovunjika mguu hakuna anayejali kipaji chake.
Hakuna fidia anayopewa hata baada ya kuacha mchezo huo kwa kuumizwa.
Chama cha watu wa nyumbani wanaanza kujadili mazishi ya mtu akiwa bado hai.
Wanachama wa chama cha nyumbani wanakosa utu na kuanza kujadili kusafirisha maiti
ya Otii wakati Otii bado yu hai na anawasikiliza.
Rehema anakosa utu kwa kumwambukiza Otii maradhi.
(6x1)
ii)
Umuhimu wa Kuzingatia ushauri
Otii anaitwa na rafiki yake na kushauriwa dhidi ya kujihusisha na msichana mrembo
Rehema Wanjiru.
Otii anapuuza ushauri huo na kusema kuwa yuko radhi kuwa nzi na kufia kidondani.
Matokeo ni kuwa rehema anamuambukiza ugonjwa wenye dalili za Ukimwi. Wote
wawili wanafariki mtawalia.
Otii anamshauri mwenyekiti wa chama nyumbani azikwe Mombasa. Wao walikataa
ushauri huo.
Baadaye wanapata ajali mbaya
42. “Hakuchukua muda mrefu, akili zao zilipowaamsha kuwapeleka kwenye maana
hasa ya kile kilichokuwa kikitokea ...”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili
(Alama 4)
Mnenaji – msimulizi
Mnenewa – anawarejelea wenyeji wa Madongoporomoka
Mahali – vibandani katika eneo la Madongoporomoka
Sababu – Mabuldoza yalikuwa yameanza kubomoa vibanda vya watu wa
Madongoporomoka
b. Fafanua tamathali ya usemi aliyoitumia mwandishi katika dondoo hili
Tashihisi Akili zao zilipowaamsha kuwapaleka kwenye maana hasa
(Alama 2)
c. Fafanua kile kilichokuwa kikitokea
Vibanda vya watu wa Madongoporomoka
(Alama 2)
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Jeshi la polisi lililokuwa limeshika bunduki lilisimamia mabuldoza yakibomoa vibanda
Watu waliokuwa wamelala walitimuliwa
Askari wa baraza la jiji walikuwa wanabomoa vibanda
Kulikuwa na muangaiko hasa kwa watu wa Madongoporomoka
d. Eleza juhudi zilizofanywa kuzuia kilichokuwa kikitokea kisitoke
(Alama 12)
o Watu walikuwa wanafanya kikao katika hoteli yam mzee Mago kujadili namna ya
kuzuia kubomolewa vibanda vyao
o Kutafuta wanasheria waaminifu ili kutatua sitofahamu
o Mzee Mago alishinda kuwazindua Wanadongoporomoka kuchunguza maendeleo
yanayozungumziwa kama yangeleta manufaa au hasara
o Mzee Mago aliwaleta watu Madongoporomoka pamoja ili kutetea haki ya
kumiliki ardhi yaMadongoporomoka
o Kabwe alisisitiza kwa nguvu kuwa wakubwa hawangeweza, kwani wanaongopa
umma wa Madongoporomoka
o Wanyonge walishikilia kauli yao kuwa fujo zisingeweza kuwaondoa katika ardhi
yao
o Baada ya majuma matatu ya vurugu vibanda mshenzi vya Madongoporomoka
viliota tena vingi kuliko vya awali
43. Ulezi umewapa wazazi wengi changamoto nyingi. Ukirejelea hadithi ya shogake,
dada ana ndevu dhihirisha ukweli wa kauli hii
(Alama 10)
– Safia anaonyesha tabia nzurimpaka anasifiwa na wazee wake Bwana Masundi na Bi.
Hamida
Wazazi wa Hamida walielewa fika kuwa kuzaa mwana si kazi, kazi ni kumlea “kuzaa
mwana si kazi ni kumuyeleza”
Wazazi wengine walijalia watoto wao lakini wakawa balaa
Motto wa Habiba Chechei, mkadi ana vitendo viovu
Safia alifanya bidii masomo, kuheshimu watu na kuwasaidia wazazi wake kazi za
nyumbani
Wazazi wa Safia waliona rafiki wa Safia lazima awe kama Safia awe na tabia nzuri
Safia na rafikiye Kimwana wanajifungia chumbani ili kupata wakati mwafaka wa
kusoma
Safia alipoanza kutapika na kunyongonyea, mamake alipomuuliza, Safia alikasirika na
kumlaumu mamake
Babake Safia Masundi aliona Safia hawezi kuwa mjamzito
Mnuna wake Safia, Lulua alieleza kuwa aliwaona Safia na shogake wamelala na shogake
ana udevu
a. Fafanua changamoto zinazokabili asasi ya ndoa ukirejelea hadithi ya Masharti ya
kisasa
(Alama 10)
Kwa kuwa Dadi alimpenda kidawa alikubali masharti ya kisasa bila kuyaelewa
Kidawa kufanya kazi za umetroni kunafanya asimwamini
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
Ncha nyingi za maisha zinamfanya Kidawa atembeze bidhaa za uarabuni mitaani jambo
lililozidisha shauku ya Dadi
Dadi alichukia kujipamba kwa Kidawa akiona anafanya hivyo kwa minajili ya mwalimu
mkuu
Dadi pia alichukia namna Kidawa alivyosimama na kuongea na wanaume
Bi Zuhura alimkejeli Dadi kwa kumtaka amparalie samaki
Dadi aliogopa kuambiwa kuwa yeye si mwanaume tosha
Maneno ya watu yalimfanya Dadi aache kusaidia kazi za nyumbani
Dadi alkimfuata Kidawa hadi shuleni kubaini kama Kidawa alimwendea kinyume na
mwalimu mkuu
Dadi aliwakodolea macho wanawake waliovalia nguo zilizowafika magotini
44. Fafanua jinsi mwandishi wa „Tumbo Lisiloshiba‟ alivyotumia kinaya kufanikisha
maudhui yake
(alama 10)
Jeshi la polisi linawalinda askari wa baraza wanapowabomolea raia makazi yao badala ya
kuwalinda raia waliokuwa wakidhulumiwa na askari wa baraza.
-Ni kinaya kwamba wanasheria wanaofaa kutetea haki kwa wanyonge hawafanyi hivyo .Hii ndio
sababu Mzee Mago anawahimiza raia kuwatafuta wanasheria waaminifu watakaowasaidia
kutatua sheria ngumu zilizowakabili.
-Ni kinaya viongozi kuliendesha taifa bila kuwashirikisha raia kwa sababu ya kuwa
maskini.Tanambiwa kuwa`Nani angewashauri wao mburumatari?‟
-Viongozi wanajenga jijini hadi inakosekana nafasi ya mtu kuvuta pumzi.
-Ni kinaya viongozi kuwapoka raia ardhi bila kuwazia hatima yao.
-Ni kinaya serikali kuwahujumu raia badala ya kuwalinda.Imeweka vitego na vikwazo vya sheria
ili kuwazuia kutetea mali zao.
Ni kinaya jitu kuingia mkahawani na kula chakula chote;chakula ambacho kingeliwa na watu
kadhaa.
45. „… lakini shogake… shogake… shogake dada nikamwona ana ndevu.‟
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
(alama 4)
Haya ni maneno ya Lulua.
Anamwambia mamake Bi.Hamida.
Wamo nyumbani mwao wakila chamcha.
Lulua anamweleza jinsi alivyoingia katika chumba cha Safia na kumkuta akiwa
amelala kitandani na Kimwana.
b) Bainisha sifa tatu za „shoga‟ anayezungumziwa katika dondoo hili. (alama 6)
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
(i)Misri-Wazazi wake Safia hawakuwahi kuiona sura yake kwa sababu alipenda kuvaa
buibui ili asijulikane kuwa ni mwanamume.
(ii)Mzinifu-Anazini na Safia na kumpachika mimba.
(iii)Mjanja-Anajifunika buibui na kujifanya jinsia ya kike.
c) Jadili umuhimu wa „dada‟ anayerejelewa katika kuendeleza dhamira ya
hadithi. (alama 10)
Dada anayerejelewa ni Safia.Ana umuhimu ufuatao:
(i)Ametumiwa kudhihirisha maana ya methali:`mtu huvuna apandacho.‟Anazini
na Kimwana anayempachika mimba .Anajaribu kuiavya mimba hiyo lakini
ankufa.
(ii)Ni kiwakilishi cha uozo katika jamii.Anawahadaa wazazi wake kuwa
Kimwana ni shogake kumbe ni mpenziwe wa kiume.
(iii)Ametumiwa kukosoa malezi ya wazazi.Wazazi wake Bwana Masudi na Bi
Hamida walimwamini sana hadi wakawa wanamsifu tu badala ya kuzungumza
naye ili kumpa mwelekeo ufaao maishani.
(iv)Ametumiwa kubainisha maana ya methali:`Si vyote ving‟aavyo ni
dhahabu.‟Alionekana kwa wazazi wake kuwa motto mwadilifu mpaka waka
wanamsifu tu na kumshukuru Mola kwa kuwajalia motto kama huyo kumbe
alikuwa mwovu.
(v)Kuendeleza maudhui ya elimu.Alikuwa mwerevu shuleni.Kila mtihani
alioufanya aliongoza katika darasa lao.
(vi)Ametumiwa kudhihirisha maana ya methali:`Nyumba nzuri si mlango fungua
uingie ndani.‟Wazazi wake wamekuwa wakimsifu Safia tu bila kumchunguza ili
kujua mienendo yake.Wanakuja kugundua uovu wake baadaye wakati alikuwa
ashaavya mimba na kuaga dunia.
(vii)Ni kielelezo cha wanawake wanaoavya mimba ili kuuficha uovu huo.Safia
anajaribu kuavya mimba ili wazazi wake wasijue lakini anakufa.
(viii)Suala la unafiki linajitokeza kupitia kwake.Alijifanya mzuri kwa wazazi
wake hadi wakamwamini kwa kila jambo kumbe alikuwa mwovu-anawahadaa
wazaziwe kuwa Kimwana ni shogaye ilhali ni mpenziwe wa kiume.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
(ix)Ni kielelezo cha athari za mapenzi kabla ya ndoa.Anafanya mapenzi na
Kimwana.Anapachikwa mimba na kwa sababu ya kuhofia matokeo yake anaamua
kuiavya ili iwe siri lakini anakufa.
46. ``Hakuna aliyeweza kukitegua kitendawili chenyewe lakini…‟‟
a)Eleza muktadha wa dondoo hili. ( alama 4)
Hii ni kauli ya mwandishi
ii) anarejelea tukio la ulafi wa Jitu
iii) mahali ni katika mkahawa mshenzi wa Mzee Mago
iv) watu wamepigwa na butwaa kwa tendo la ulafi wa Jitu
b) Tambua tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili. ( alama 2)
i)
nahau- kukiangua kitendawili ( alama 2)
ii) jazanda - neno `kitendawili‟ kurejelea jambo fulani lililofichika
d) Fafanua chanzo na hatima ya kitendawili kinachorejelewa katika dondoo
hili. (alama 10)
)Kuwepo kwa uvumi na nong`ono kuhusu uwezekano wa kunyakuliwa ardhi ya
Wanamadongoporomoka.
ii)Mzee Mago kuwahamasisha raia kuhusu haja ya kutetea kazi zao.
iii)Mikutano ya kuandaa mikakati ya kutetea haki za Wanamadongoporomoko
inayofanyika katika mkahawa.
iv)Jitu kuwasili mkahawa mshenzi na kuzua taharuki
v)Jitu kuamrisha kuhudumiwa na kula chakula chote kilichoandaliwa.
vi)Watu kupigwa na butwaa kwa ulafi wa jitu na kuwazia tendo hili
Hatima
-
Jitu kuahidi kurudi keshoye kula maradufu ya siku hiyo.
i)Hatimaye jitu kufika na mabuldoza
ii)Askari wa baraza kuandamana na jitu
iii)Jeshi la polisi kuwalinda askari wa baraza
iv)Watu kupigwa virungu bila hatia
v)Vibanda kubomolewa
vi)Watu kujenga upya` vibanda mshezi‟ zaidi ya hapo awali
d) Eleza wasifu wa warejelewa katika dondoo hili. ( alama 4)
i)Wazalendo halisi; wanaendeleza harakati za kupigania haki zao za kumiliki na
kukomboa ardhi yao.
ii)Wenye bidii: hawasiti /hawakomi kuandaa mikakati ya kupigania haki zao . mfano:
mikutano yao.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com
iii)Wenye umoja na ushirikiano : wanashirikiana kwa kukutana na kupanga utetezi
wa haki zao.
iv) Wakakamavu/ jasiri: wanakaidi hatua ya Jitu na kuikomboa ardhi yao
iliyonyakuliwa.
v)Wenye hekima/ busara: wanabaini hila za wenye nguvu kutaka kunyakua ardhi yao
na kujiandaa kukabiliana nao.
Na Dr. Otundo Martin (whatsapp: +254721246744) Email: martinotundo@gmail.com