Abia (jimbo)
Mandhari
Abia ni jimbo la kujitawala la Nigeria lenye wakazi milioni 4.2 (2005) na eneo la km² 5,834. Mji mkuu ni Umuahia na mji mkubwa Aba wenye wakazi 900,000.
Eneo
[hariri | hariri chanzo]Abia imepakana na majimbo ya Enugu, Ebonyi, Cross River, Akwa Ibom, Rivers, Imo na Anambra. Haina pwani.
Mito muhimu ni mto Imo na mto Aba inayoelekea kwenye delta ya mto Niger.
Kusini mwa jimbo ni tambarare ya chini yenye mvua nyingi. Maeneo ya kaskazini ni ya juu kidogo.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Uchumi umetegemea hasa kilimo. Nafaka, minazi, mahindi, mpunga, muhogo, matunda na mboga hulimwa.
Kuna pia madini yanayochimbwa: ni hasa zinki, mchanga, chokaa pia kiasi cha mafuta ya petroli. Abia hukorogwa bia na kuna viwanda vya nguo na kioo.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Watu wa Abia ni hasa wa kabila la Igbo.
Abia | Abuja Federal Capital Territory | Adamawa | Akwa Ibom | Anambra | Bauchi | Bayelsa | Benue | Borno | Cross River | Delta | Ebonyi | Edo | Ekiti | Enugu | Gombe | Imo | Jigawa | Kaduna | Kano | Katsina | Kebbi | Kogi | Kwara | Lagos | Nasarawa | Niger | Ogun | Ondo | Osun | Oyo | Plateau | Rivers | Sokoto | Taraba | Yobe | Zamfara |
Makala hii kuhusu maeneo ya Nigeria bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Abia (jimbo) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |