Allen Johnson
Rekodi za medali | ||
---|---|---|
Johnson katika mbio ya 2007 ISTAF Berlin | ||
Riadha ya Wanaume | ||
Anawakilisha nchi Marekani | ||
Michezo ya Olimpiki | ||
Dhahabu | 1996 Atlanta | 110 m urukaji viunzi |
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF | ||
Dhahabu | 1995 Gothenburg | 110 m urukaji viunzi |
Dhahabu | 1997 Athens | 110 m urukaji viunzi |
Dhahabu | 2001 Edmonton | 110 m urukaji viunzi |
Dhahabu | 2003 Paris | 110 m urukaji viunzi |
Medali ya Shaba | 2005 Helsinki | 110 m urukaji viunzi |
Mashindano ya Mabingwa ya Ndani ya Ukumbi | ||
Dhahabu | 1995 Barcelona | 60 m urukaji viunzi |
Dhahabu | 2003 Birmingham | 60 m urukaji viunzi |
Dhahabu | 2004 Budapest | 60 m urukaji viunzi |
Fedha | 2008 Valencia | 60 m urukaji viunzi |
Allen Kenneth Johnson (alizaliwa 1 Machi 1971) ni mwanariadha wa mbio za kuruka viunzi aliyeshinda medali ya dhahabu katika mbio ya 110m na urukaji viunzi katika michezo ya Olimpiki ya 1996,Atlanta,Georgia.
Aliyezaliwa mjini Washington D.C.,ni mwanamichezo bora na alisoma katika Chuo Kikuu cha Carolina Kaskazini alipofuzu katika michezo mbalimbali.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Johnson alipata majeraha katika mwaka wa 2000 lakini bado katika juhudi zake alifika fainali ya mbio yake katika Olimpiki ya 2000 huko Sydney,Australia.Alichukua nafasi ya nne katika fainali akishindwa na kidogo tu.
Mwaka wa 2003 katika Stade de France,Johnson alishinda medali yake ya nne ya dhahabu katika mbio za IAAF za Mabingwa wa Dunia katika 110m ya urukaji viunzi akishinda Terrence Trammell.Hii ilishinda medali tatu alizoshinda Greg Foster katika mashindano ya IAAF.
Katika Olimpiki ya 2004,alijikwaa na kiunzi katika awamu ya pili ya kuhitimu na hivyo basi akashindwa kumaliza mbio hiyo na hakufika fainali. Hata hivyo,aliorodheshwa kama nambari ya kwanza duniani katika msimu wa 2004.
Johnson hufanya mazoezi chini ya Kocha Curtis Frye katika Chuo Kikuu cha Carolina Kusini ambapo anafanya kazi kama kocha msaidizi wa kujitolea. Yeye anaishi Irmo,katika eneo la South Carolina.
Muda wake bora wa kibinafsi ni sekunde 12.92,imekosa kufikia rekodi ya Colin Jackson kwa sekunde 0.01 na sekunde 0.05 nyuma ya rekodi ya Dayron Robles. Johnson amemaliza mbio 11 halali kwa muda ulio chini ya sekunde 13,nyingi kuliko mtu mwingine hivi sasa.
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo](Mbio ya mita 110 ya urukaji viunzi)
- 1994
- 1995
- Mashindano ya Mabingwa wa Dunia katika Riadha ya 1995 - Gothenburg, Uswidi
- 1995 IAAF Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Ndani ya Ukumbi - Barcelona, Uhispania
- 1996
- 1998
- Michezo ya Goodwill ya 1998 - Uniondale, New York
- 2000
- 2001
- Mashindano ya Mabingwa wa Dunia katika Riadha ya 2001 - Edmonton, Alberta, Kanada
- Michezo ya Goodwill - Brisbane, Australia
- 2002
- Mashindano ya Kombe la Dunia ya 2002 - Madrid, Uhispania
- 2003
- Mashindano ya Mabingwa wa Dunia katika Riadha ya 2003 - Paris, Ufaransa
- Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF ya Ndani ya Ukumbi ya 2003 - Birmingham, Uingereza
- 2004
- 2005
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Biography at USA Track & Field Ilihifadhiwa 25 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Allen Johnson's U.S. Olympic Team bio Archived 2004-08-25 at Archive.today
- IAAF wasifu wa Allen Johnson
Alitanguliwa na Colin Jackson |
Wanaume Bora katika mbio ya 110m ya urukaji viunzi wa Mwaka 1995 — 1998 |
Akafuatiwa na Mark Crear |
Alitanguliwa na Mark Crear |
Wanaume Bora katika mbio ya 110m ya urukaji viunzi wa Mwaka 2000 — 2001 |
Akafuatiwa na Anier García |
Alitanguliwa na Anier García |
Wanaume Bora katika mbio ya 110m ya urukaji viunzi wa Mwaka 2003 |
Akafuatiwa na Liu Xiang |