Aruj Barbarossa
Mandhari
Aruj Barbarossa (alijulikana kama Oruç Reis kwa Waturuki, 1474 - 1518) alikuwa mharamia wa Milki ya Osmani ambaye baadaye alikuwa Sultani wa Algiers. Alikuwa ndugu mkubwa wa Hayreddin Barbarossa, ambaye alikuwa jemadari maarufu wa Ottoman.
Aruj alizaliwa kisiwani Midilli (Lesbo ya leo nchini Ugiriki) chini ya Dola la Osmani na alikufa vitani dhidi ya Wahispania huko Tlemcen.
Alikuwa anajulikana kama Baba Aruj baada ya kuwasafirisha idadi kubwa ya wakimbizi Wamorisco, Waislamu, na Wayahudi kutoka Hispania hadi Afrika Kaskazini. Jina hili lilibadilika kwa muda mrefu katika etimolojia ya watu barani Ulaya, na kuwa Barbarossa, ambalo linamaanisha "Ndewe Mwekundu" kwa Kiitaliano.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "World Monument Photography". worldmonumentphotos.com. Iliwekwa mnamo 2017-12-08.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Aruj Barbarossa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |