Nenda kwa yaliyomo

Asmara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muonekano wa Mji wa Asmara


Jiji la Asmara
Nchi Eritrea
Eneo Maekel

Asmara (pia Asmera) ni mji mkuu na makazi makubwa nchini Eritrea, watu 579,000 wakiwa wanaishi mjini humu.

Nguo, nyama, pombe, viatu na seramiki ni mojawapo ya vifaa vinavyotoka mji wa Asmara.

Asmara yenyewe kijiografia iko 15°20' kaskazini, 38°55' mashariki (15.333, 38.91667).

Mji umo katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Asmara ilianza kutoka vijiji vinne karne ya 12 kama eneo la biashara na baadaye kama mji wa Ras Alula.

Ilitawaliwa na Waitalia tangu mwaka 1889 na kuwa Mji Mkuu 1897 wa koloni la Eritrea.

Miaka ya 1930 Waitalia waligeuza mji kwa majengo mapya; Asmara iliitwa na Waitalia "Piccola Roma" (Roma mdogo). Siku hizi majengo makubwa zaidi ya Asmara ni ya Kiitalia, na maduka bado yana majina ya Kiitalia, mfano - "Bar Vittoria", "Pasticceria moderna", "Casa del formaggio", "Ferramenta".

Faili:Asmara-architecture.jpg
Sanaa ya mwaka 1930, ambayo yanaonyesha mtindo wa deco ya onekana kwa benki ya dunia.

Siku za vita vya uhuru wa Eritrea kutoka Ethiopia, Uwanja wa ndege wa Asmara ulikuwa mhimu sana, Waethiopia walitumia uwanja huo kupata silaha kutoka ng'ambo. Mji wa mwisho kuanguka kwa Jeshi ya ukombozi wa Eritrea ulitekwa mwaka 1990 na kusalimishwa na Jeshi ya Ethiopian bila vita mnamo 24 Mei 1991.

Mji wenyewe una makumbusho na unajulikana kwa majengo ya karne ya 20, sanaa ya Deco, sinema Impero, Kubisti, Pensheni Afrika, Kanisa kuu la Tewahedo, Nyumba ya Opera, ujenzi wa umbele, jengo la Fiat Tagliero, jengo la neo-Romanesque, kanisa kuu la Kanisa Katoliki na ujenzi wa kupendeza.

Asmara pia ni nyumbani kwa Chuo kikuu cha Asmara na gome ya karne ya 19. Kituo cha ndege, Uwanja wa Kimataifa wa Asmara, kimeungana pia na bandari ya Massawa kwa Reli ya Eritrea.

Asmara ni makao makuu ya Patriarki wa Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea, lililokubaliwa na Patriarki wa Aleksandria (Misri) kuwa linajitegemea tangu mwaka 1993 na kuongozwa na Patriarki wake tangu mwaka 1998, sawa na Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia ambalo pia linakiri umoja wa nafsi wa Yesu Kristo (Tewahedo).

Uchambuzi

[hariri | hariri chanzo]
  • Edward Denison, Guang Yu Ren, Naigzy Gebremedhin and Guang Yu Ren - Asmara: Africa's Secret Modernist City (2003) ISBN 1-85894-209-8 (Siri ya Afrika Mji wa kisasa)

Viungo via nnje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Asmara kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy