Dini ya miungu mingi
Dini ya miungu mingi (pia: upolitheisti, kutoka ing. polytheism) ni aina ya dini inayotambua zaidi ya mungu mmoja na kuabudu mingi.
Katika dunia
[hariri | hariri chanzo]Mifano mashuhuri ni dini za kale kama zile za Misri ya Kale, Ugiriki ya Kale na Roma ya Kale.
Leo hii dini zinazoamini umoja wa Mungu, kama vile Ukristo na Uislamu, huwa na wafuasi wengi duniani.
Lakini kuna pia wafuasi wengi wa dini zinazosadiki miungu mingi kama vile Uhindu (India) na Shinto (Japani).
Katika Afrika
[hariri | hariri chanzo]Katika Afrika dini asilia mara nyingi zilimjua Mungu mmoja pamoja na mapepo mbalimbali. Hivyo Waafrika hawakuona shida sana kusadiki dini za kimataifa zilizotangaza kuwa Mungu amejifunua kwa binadamu.
Hata Afrika ya Magharibi, ambayo ina dini za kienyeji yenye miungu mingi, wakazi wanazidi kujiunga na dini za Mungu Pekee.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |