Nenda kwa yaliyomo

Halijoto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kipimajoto (thermomita) inaonyesha kiwango cha halijoto ama joto au baridi

Halijoto (pia: Jotoridi) ni neno la kutaja hali ya kitu kama ni baridi au moto. Wanadamu wana mishipa inayoonyesha tofauti kati ya baridi na joto. Kwa kuwa na uhakika tunatumia thermomita inayoonyesha halijoto kwa kipimo kama selsiasi, kelvini au fahrenheit.

Kisayansi halijoto ni kiasi cha mwendo wa molekuli ndani ya gimba, kiowevu au mjao wa gesi. Ndani ya gimba mango na pia ndani ya kiowevu na gesi molekuli huchezacheza kiasi; mkasi wa kucheza unaonekana kama halijoto yaani kiwango kidogo cha kucheza ni "baridi" na kiwango kikibwa cha kucheza ni "joto". Mkasi wa mwendo wa molekuli (au atomi) ndani ya gimba hutegemea na nishati mwendo ya molekuli zake. Nishati mwendo inaweza kuongezeka au kupunguza kiasi jinsi molekuli zinapokea nishati kutoka nje au kupitisha nishati yao kwa kitu kingine.

Kupasha moto chini ya sufuria ya maji huongeza nishati mwendo ndani ya sufuria na ndani ya maji kwa sababu nishati ya joto inapokelewa na molekuli na kuwa nishati mwendo. Hivyo halijoto ya sufuria na ya maji hupanda juu. Kinyume chake ni kupoa maana molekuli za maji na sufuria hupitisha nishati mwendo kwa molekuli za hewa na kwa njia hii halijoto ya sufuria inashuka.

Pasipo na mwendo kabisa ndani ya mada huitwa kiwango cha joto cha sifuri halisi ambacho ni sawa na vizio −273.15° kwenye skeli ya selsiasi au vizio 0° kwenye skeli ya kelvini. Hiki ni kiwango cha duni kabisa hakuna baridi zaidi. Kiwango cha juu hakijulikani inawezekana hakuna.

Viwango muhimu vya halijoto duniani

[hariri | hariri chanzo]

Katika mazingira ya dunia kuna viwango fulani vya joto ambavyo ni muhimu hasa:

  • Maji huganda mnamo halijoto ya 0 °C, 32 °F, au 273.15 K.
  • Maji huchemka mnamo halijoto ya 100 °C, 212 °F, au 373.15 K. (habari za maji zinalingana na kimo sawa na uwiano wa bahari)
  • Mwili wa kibinadamu hwa na halijoto ya 37 °C kama mtu ni mzima.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy