Illinois
Illinois Land of Lincoln |
|||
| |||
Nchi | Marekani | ||
---|---|---|---|
Mji mkuu | Springfield | ||
Eneo | |||
- Jumla | 149,998 km² | ||
- Kavu | 143,961 km² | ||
- Maji | 6,037 km² | ||
Tovuti: http://www.illinois.gov/ |
Illinois ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Ilikuwa jimbo la Marekani tangu 1818. Iko katika magharibi ya kati ya nchi ikipakana na majimbo ya Wisconsin, Iowa Missouri, Kentucky na Indiana. Upande wa kaskazini - mashariki imepakana na Ziwa Michigan.
Eneo la jimbo ni 140,998 km² likiwa na wakazi 12,831,970 hivyo kuna msongamano wa watu 86.27/km². Idadi kubwa hukaa katika rundiko la jiji la Chicago penye wakazi milioni 9.
Mji mkuu ni Springfield lakini mji mkubwa ni Chicago. Kwa miji mingine angalia Orodha ya miji ya Illinois.
Watu kutoka Illinois
[hariri | hariri chanzo]- Rais wa 16 wa Marekani Abraham Lincoln
- Rais wa 18 wa Marekani Ulysses S. Grant
- Rais wa 40 wa Marekani Ronald Reagan
- Mchoraji na mkurugenzi wa filamu Walt Disney
- Hillary Clinton seneta wa New York na mke wa rais Bill Clinton
- Rais wa 44 wa Marekani Barack Obama alikuwa seneta wa Illinois kabla ya kuwa rais.
Majimbo ya Marekani |
---|
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Makala hii kuhusu maeneo ya Illinois bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Illinois kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |