Nenda kwa yaliyomo

Jinaha la Ghurabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jinaha la Ghurabu (Gamma Corvi, Gienah)
Jinaha la Ghurabu inaonekana kama nyota pacha katika picha hii iliyopigiwa na darubini ya angani Hubble.Jinaha la Ghurabu A ni nyota kubwa, Jinaha la Ghurabu B iko chini yake upande wa kushoto.
Kundinyota Ghurabu (Corvus)
Mwangaza unaonekana 2.58 [1]
Kundi la spektra B8 III
Paralaksi (mas) 21.23
Umbali (miakanuru) 154
Mwangaza halisi -0.79
Masi M☉ A: 4.2 B: 0.8
Mng’aro L☉ 331
Majina mbadala Gienah Corvi, 4 Corvi, BD–16 3424, FK5 457, HD 106625, HIP 59803, HR 4662, SAO 157176


Ghurabu na Batiya kwenye ramani ya nyota "Urania's Mirror" ya Mwingereza Sidney Hall mnamo mwaka 1824. γCor ni nyota kwenye ubawa wa kushoto, hata kama jina lake la Kiarabu linasema "kulia"; tofauti inatokana na kawaida kuchora nyota kama "kwa macho ya Mungu".

Jinaha la Ghurabu (kwa Kiingereza na Kilatini Gienah, pia γ Gamma Corvi, kifupi: Gamma Cor, γ Cor) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Ghurabu (Corvus). Iko karibu kiasi na nyota angavu ya Sumbula (Spica) katika Mashuke Mashuke (pia Nadhifa, lat. Virgo).

Jina

Jinaha la Ghurabu ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema اليمن الغراب الجناح janaha-l-ghurab-al-yaman ambayo inamaanisha “ubawa wa kunguru wa kulia”[3]. Hapa Waarabu wanatumia jina la utamaduni wao ingawa walitafsiri pia jina la Kigiriki Κύων Ki-on yaani mbwa waliokuta kwa Ptolemaio katika kitabu chake cha Almagesti. Hivyo kulikuwa zamani pia kwa Kiarabu jina la "nyota" ya mbwa" kwa ajili ya Jinaha la Ghurabu. Asili ya jina la Kiarabu الشعرى ash-shi'ra inaweza kutoka kwa Kigiriki Σείριος sei-ri-os inayomaanisha "ya kuchoma, moto sana". Wagiriki walitumia jina hili pamoja na "Nyota ya Mbwa" kwa sababu wakati ule nyota hii ilianza kuonekana vema kwenye anga ya asubuhi katika siku za joto kuu. Hapo kulitokea pia jina la "siku za mbwa" (ing. dog days) kwa ajili ya kipindi cha siku za joto katika lugha mbalimbali.[4]

Katika matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulichagua "Gienah"[5].

Gamma Corvi ni jina la Bayer. Ilhali hii ni nyota angavu zaidi katika Ghurabu ingestahili "alfa", lakini kupewa jina "gamma" ambayo ni herufi ya tatu katika Alfabeti ya Kigiriki ni mfano kwamba Bayer hakutoa herufi zake kikamilifu kufuatana na mwangaza halisi.

Tabia

Jinaha la Ghurabu - Gienah ina mwangaza unaoonekana wa mag 2.58 na mwangaza halisi ni -0.79. Umbali wake na Dunia ni miakanuru 154.[6].

Jinaha la Ghurabu si nyota moja tu bali nyota maradufu. Kuwepo kwa nyota ya pili isiyoonekana kwenye darubini kulithibitishwa kwa njia ya utafiti wa spektra yake.

Nyota kuu ni jitu buluu yenye jotoridi kubwa, takriban nyuzi 12,000 usoni wake.

Tanbihi

  1. Data kufuatana na Janson & alii (2011)
  2. ling. Knappert 1993
  3. Allen uk. 119 anataja jina asilia kuwa « Al Shi ra al Abur al Yamaniyyah, the Brightly Shining Star of Passage of Yemen, in the direction of which province it set.« 
  4. Leo hii kuonekana vile kwa Jinaha la Ghurabu kumeshahamia kipindi cha siku 30 hivi tangu nyakati za kale kwa sababu mbili: a) mwendo wa nyota yenyewe katika anga-nje, b) Mzunguko wa kuinama wa mhimili wa Dunia inayobadilisha polepole pembe jinsi tunavyoona nyota.
  5. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
  6. GIENAH (Gamma Corvi), tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje

pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy