Nenda kwa yaliyomo

John Henry Newman

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
John Henry Newman alivyochorwa na John Everett Millais, 1881.
J. H. Newman alipokuwa na miaka 23 wakati alipohubiri mara ya kwanza.
John Henry Newman
Deski ya Newman katika nyumba ya Oratori mjini Birmingham
Chumba cha Newman katika Oratori hiyo.
Kikanisa chake ndani ya chumba hicho

John Henry Newman, C.O. (London, Uingereza, 21 Februari 1801 - Edgbaston, Birmingham, 11 Agosti 1890) alikuwa padri na kardinali wa Kanisa Katoliki baada ya kuacha ukasisi wa madhehebu ya Anglikana akiwa tayari maarufu nchini kote kutokana na mahubiri na maandishi yake[1].

Alitangazwa na Papa Benedikto XVI kuwa mwenye heri tarehe 19 Septemba 2010[2] halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 13 Oktoba 2019.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Oktoba[3].

John Henry alikuwa wa kwanza kati ya watoto 6 wa mwenye benki John Newman na Jemina Foundrinier, mwenye asili ya Ufaransa.

Alipata elimu bora karibu na London akaathiriwa na mchungaji wa Kikalvini hata akashikilia msimamo wa Kiprotestanti kwa uamuzi ambao baadaye aliuita wongofu wake wa kwanza 1816.

Mwaka 1817 alijiunga na Trinity College huko Oxford akawa shemasi wa Kianglikana mwaka 1824.

Mwaka 1828 alifanywa paroko wa kanisa la chuo kikuu kwa jukumu la kuwachunga wanachuo; wakati huohuo alijitosa katika masomo ya falsafa na teolojia.

Baada ya kuwa profesa wa Oxford na kasisi wa Anglikana (Church of England) mwenye mwelekeo wa Kiinjili, Newman alipata kuwa kiongozi wa Oxford Movement. Kundi hilo la Waanglikana lilikusudia kurudisha Kanisa la Uingereza kwenye imani na ibada za Kikatoliki.

Miaka 2 baada ya kuacha ukasisi na hatimaye Anglikana yenyewe, alijiunga na Kanisa Katoliki moja kwa moja (9 Oktoba 1845).

Mwaka 1847 alipata upadirisho akaanzisha shirika la Waoratori mjini Birmingham.

Alichangia kwa kiasi kikubwa (1851 - 1858) uundaji wa Catholic University of Ireland, ambayo leo inaitwa University College, Dublin na ni chuo kikuu kinachoshinda kwa ukubwa vingine vyote vya Ireland.

Baada ya kufanya uchungaji tena, mwaka 1879 aliteuliwa na Papa Leo XIII kuwa kardinali.

Kama mwandishi wa teolojia na fasihi ya Kiingereza, Newman ni maarufu hasa kwa simulizi la maisha yake Apologia Pro Vita Sua (18651866), kwa Grammar of Assent (1870), kwa shairi The Dream of Gerontius (1865), ambalo lilitiwa muziki na Edward Elgar mwaka 1900 kama oratorio.

Kati ya tenzi zake, maarufu zaidi ni Lead, Kindly Light na Praise to the Holiest in the Height (kutoka Gerontius).

Juu ya kaburi lake yameandikwa maneno ya Kilatini aliyoyachagua mwenyewe kama muhtasari wa maisha yake aliyoyaona kama safari kuelekea ukweli: Ex umbris et imaginibus in veritatem (Kutoka vivuli na mifano hadi ukweli).

Sala yake

[hariri | hariri chanzo]

Mungu wangu uliyetuumba, ulijua kwamba wewe tu unaweza kutushibisha; basi umeamua kujifanya chakula na kinywaji chetu.

Fumbo abudiwa kuliko yote! Huruma ya ajabu kuliko zote!

Wewe mwenye utukufu, uzuri, nguvu na utamu kuliko wote ulijua fika kwamba chochote kingine kisingeweza kutegemeza umbile letu lisilokoma, mioyo yetu dhaifu; kwa hiyo ulitwaa mwili na damu ya kibinadamu, hivi kwamba, vikiwa mwili na damu ya Mungu, viweze kuwa uhai wetu...

Naja kwako, Bwana, sio tu kwa sababu pasipo wewe sina raha, si tu kwa sababu najitambua ninakuhitaji, bali kwa sababu neema yako inanivuta nikutafute kwa ajili yako mwenyewe, kwa jinsi ulivyo mtukufu na mzuri.

Naja kwa uchaji mkubwa, lakini kwa upendo mkubwa zaidi.

Maandishi

[hariri | hariri chanzo]
Akiwa Mwanglikana
  • The Arians of the Fourth Century (1833)
  • Tracts for the Times (1833–1841)
  • British Critic (1836–1842)
  • On the Prophetical Office of the Church (1837)
  • Lectures on Justification (1838)
  • Parochial and Plain Sermons (1834–1843)
  • Select Treatises of St. Athanasius (1842, 1844)
  • Lives of the English Saints (1843–44)
  • Essays on Miracles (1826, 1843)
  • Oxford University Sermons (1843)
  • Sermons on Subjects of the Day (1843)
Akiwa Mkatoliki
  • Essay on the Development of Christian Doctrine (1845)
  • Retractation of Anti-Catholic Statements (1845)
  • Loss and Gain (novel – 1848)
  • Faith and Prejudice and Other Unpublished Sermons (1848–1873; collected 1956)
  • Discourses to Mixed Congregations (1849)
  • Difficulties of Anglicans (1850)
  • The Present Position of Catholics in England (1851)
  • The Idea of a University (1852 and 1858)
  • Cathedra Sempiterna (1852)
  • Callista (novel – 1855)
  • The Rambler (Catholic periodical)]] (editor) (1859–1860)
  • Apologia Pro Vita Sua (religious autobiography – 1864; revised edition, 1865)
  • Letter to Dr. Pusey (1865)
  • The Dream of Gerontius (poem) (1865)
  • An Essay in Aid of a Grammar of Assent (1870)
  • Sermons Preached on Various Occasions (various/1874)
  • Letter to the Duke of Norfolk (1875)
  • Five Letters (1875)
  • Sermon Notes (1849–1878)
  • Select Treatises of St. Athanasius (1881)
  • On the Inspiration of Scripture (1884)
  • Development of Religious Error (1885)
Mengineyo
  • Historical Tracts of St. Athanasius (1843)
  • Essays Critical and Historical (various/1871)
  • Tracts Theological and Ecclesiastical (various/1871)
  • Discussions and Arguments (various/1872)
  • Historical Sketches (various/1872)
  • Addresses to Cardinal Newman and His Replies, with Biglietto Speech (1879)
Madondoo

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/92649
  2. "Pope to Meet Queen on Visit to Scotland". 2 Februari 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-10. Iliwekwa mnamo 2011-05-15.
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kesi ya kumtangaza mtakatifu

[hariri | hariri chanzo]

Vyama vya Newman

[hariri | hariri chanzo]

Maisha na maandishi

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy