Nenda kwa yaliyomo

Joseph John Thomson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sir J.J. Thomson

Joseph John Thomson (18 Desemba 185630 Agosti 1940) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa anajulikana kwa kugundua elektroni. Mwaka wa 1906 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Mwaka wa 1908 alipewa cheo cha Sir cha Uingereza.

Pamoja na gunduzi zake muhimu alikuwa pia mwalimu bora akachangia hivyo kwenye maendeleo ya sayansi. Mmoja wa wanafunzi wake alikuwa Ernest Rutherford aliyemfuata baadaye kuwa pfofesa wa fizikia kwenye Chuo Kikuu cha Cambridge. Nane kati ya wasaidizi wake waliendelea kupata baadaye pia tuzo za Nobel katika fani za fizikia au kemia (Francis William Aston, Charles Glover Barkla, Niels Bohr, Max Born, William Henry Bragg, Owen Willans Richardson, Ernest Rutherford, Charles Wilson). Mwanawe George Thomson alshinda mwaka 1937 tuzo ya Nobel kwa kuthebitisha tabia ya elektroni kuwa kama wimbi.

Hadi kifo alikuwa Mkristo wa Kanisa la Kianglikana.[1]

  1. Seeger, Raymond. "The American Science Affiliation". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-12-01. Iliwekwa mnamo 2017-03-09.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joseph John Thomson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy