Nenda kwa yaliyomo

Kidudu-deraya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kidudu-deraya

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
(bila tabaka): Bilateria
(bila tabaka): Prostomia
Faila ya juu: Ecdysozoa
Faila: Loricifera
Kristensen, 1983
Oda: Nanaloricida
Kristensen, 1983
Ngazi za chini

Familia 3:

Vidudu-deraya ni wanyama wadogo sana wa bahari wa oda Nanaloricida, oda pekee ya faila Loricifera wanaofunikwa na mabamba kama deraya. Wana urefu wa mm 0.1-1. Huishi katika masimbi ya sakafu ya bahari kwa vina vyote, aina zote za masimbi na latitudo zote[1].

Wanyama hao wamefunua hivi karibuni kiasi. Faila yao imeelezewa mwaka 1983 na Kristensen. Mnamo 2021 spishi 43 zilikuwa zimeelezewa[2], lakini spishi nyingine 100 zinasalia kuelezewa[3].

Wana kiwiliwili kikubwa kilichozungukwa na mabamba sita ya deraya. Kichwa, ambacho hubeba miiba mingi iliyopinidika nyuma, huunganishwa na kiwiliwili kupitia shingo yenye pingili ambayo inaweza kurudishwa ndani ya deraya. Mdomo unaoweza kubenuliwa uko ncha ya mbele na umezungukwa na sindano nane. Ubongo umesitawi vizuri na umeunganishwa moja kwa moja na kila mwiba. Kamba ya neva hupita upande wa chini kuelekea ncha ya nyuma. Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula huanza na mfereji wa mdomo ambao unaweza kutolewa. Kisha hufuata koromeo ya umbo la tufe iliyo na misuli yenye nguvu na hatimaye utumbo ulionyooka ambao hufunguka katika mkundu mwishoni kabisa [4].

  1. Ruppert, Edward E.; Fox, Richard S.; Barnes, Robert D., whr. (2004). Invertebrate Zoology (tol. la 7th). uk. 776. ISBN 978-0-03-025982-1.
  2. Cardoso Neves, Ricardo; Kristensen, Reinhardt Møbjerg; Møbjerg, Nadja (5 Mei 2021). "New records on the rich loriciferan fauna of Trezen ar Skoden (Roscoff, France): Description of two new species of Nanaloricus and the new genus Scutiloricus". PLOS ONE. doi:10.1371/journal.pone.0250403. id 10.1371.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Gad, Gunnar (17 Juni 2005). "Successive reduction of the last instar larva of Loricifera, as evidenced by two new species of Pliciloricus from the Great Meteor Seamount (Atlantic Ocean)". Zoologischer Anzeiger. 243 (4): 239–271. doi:10.1016/j.jcz.2004.09.001.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. {https://www.notesonzoology.com/phylum-loricifera/phylum-loricifera-features-and-classification-marine-animals/1732}
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy