Nenda kwa yaliyomo

Mwandiko wa kikabari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kutoka picha ya kichwa (1-3) kwa alama ya kikabari (4) iliyorahisishwa zaidi katika mwendo wa karne kumaanisha tu sauti ya "sag"
Maendeleo ya mwandiko wa kikabari
safu 1: picha asilia;
safu 2: mwandiko uliorahisishwa wakati wa Hammurabi;
safu 3: wakati wa Ashuri;
safu 4: wakati wa Babeli Mpya mnamo 600 KK;
safu 5: maelezo ya picha asilia na maana ya silabi iliyopatikana baadaye

Mwandiko wa kikabari ni kati ya aina za mwandiko wa kale sana duniani: ilikuwa kawaida katika Mesopotamia ya kale ukitumiwa na Wasumeri, Wababeli, Waashuri na wengine hata katika nchi jirani.

Ilianzishwa na Wasumeri mnamo mwaka 3,000 KK ikaishia baada ya mwaka 400 KK: mfano wa mwisho unaojulikana uliandikwa mwaka 75 BK.

Mwandiko picha mwanzoni

[hariri | hariri chanzo]

Chanzo chake ilikuwa mwandiko wa picha zilizotumiwa kuandika habari. Mwandiko picha huu ulirahisishwa na kuonyeshwa baadaye kwa kuchora mistari kadhaa ya kikabari badala ya picha kamili.

Vigae vya mwandiko wa kikabari

[hariri | hariri chanzo]

Mistari hii ilipatikana kutokana na njia ya kawaida ya kuandika: hapakuwa na karatasi lakini waandishi walitumia vipande vya udongo wa mfinyanzi kama ubao mdogo wa umbo la mchemraba bapa. Humo waliandika kwa kijiti na kwa njia walichora alama zinazofanana na mistari yenye vichwa au "kabari".

Vipande vya udongo wa mfinyanzi vilikaushwa na vingine kuchomwa kama tofali au vigae. Kwa njia hii viliweza kudumu katika mazingira makavu kwa miaka elfu kadhaa hadi leo. Mikusanyiko ya vigae vya mwandiko wa kikabari ilikuwa kama maktaba au hifadhi za nyaraka na ile iliyodumu hadi leo ni chanzo cha habari nyingi kuhusu utamaduni wa Mesopotamia ya Kale.

Kwa matumizi ya haraka udongo haukukaushwa. Iliwezekana pia kufuta mwandishi yote kwa kunyosha tena kipande cha udongo na kuandika upya, kwa mfano kwa matumizi ya dukani na kadhalika. Vigae vya mwandiko viliyokaushwa tu havikudumu kama vinngine vilivyochomwa lakini kuna hifadhi za nyaraka ambako vigae vilichomwa kwa bahati tu kama majengo yaliungua moto kutokana na ajali au wakati wa vita.

Maandishi maalumu, kama sheria za mfalme Hammurabi wa Babeli, yaliandikwa pia cha kuchonga alama katika jiwe au mwamba lakini hii haikuwa njia ya kawaida.

Mabadiliko ya mwandiko

[hariri | hariri chanzo]

Katika muda wa miaka 2000 ya matumizi yake mwandiko huo uliendelezwa jinsi inavyoonekana katika picha kwenye makala hii. Baada ya kuacha picha yenyewe, alama zilitumiwa kama silabi, hivyo mwandiko wa silabi ulijitokeza. Maana watu hawakuangalia tena maana asilia ya picha, bali sauti yake tu, jinsi ilivyo na herufi za alfabeti yetu.

Mwanzoni walitumia tu picha za nyumba, watu, mifugo au mazao pamoja na mistari kwa kutaja idadi. Baadaye waliendelea kuunganisha alama. Kwa mfano walitumia mistari minne |||| kwa namba 4 kama alama ya „kubwa“ au „sana“. Picha ya kisu pamoja na „4“ ilimaanisha hivyo upanga (kisu kikubwa). Picha ya samaki ilimaanisha pia rutuba, pamoja na „4“ ilipata maana ya „kuzaa kwa wingi, kuenea“.

Mfano mwingine ni kuunganisha picha za mdomo na maji kwa maana ya „kunywa“, au jicho na maji kwa „kulia machozi“. Hadi nagi hii bado walishindwa kushika lugha yenyewe, hasa vitenzi na nyakati zao.

Hapo walipata maendeleo kwa kutumia sauti ya majina tu, bila kujali maana.

Jina la maji katika lugha yao ilikuwa sauti ya „a“ – basi walianza kutumia picha ya maji kwa fonimu „a“. Vivyo hivyo neno lao kwa samaki ilikuwa "cha" - basi walianza kutumia alama ya samaki kwa sauti „cha“. Kwa njia hii walichagua picha za vitu vyenye majina fupi yaliyowakilisha silabi na sauti zilizotosha kutamka maneno yote ya lugha yao jinsi walivyosema. Kwa mfano, kwa kuandika neno "acha" wangeunganisha picha za maji yenye sauti ya "a" na samaki yenye sauti ya "cha", kumbe pamoja ni "acha".

Babu wa alfabeti yetu

[hariri | hariri chanzo]

Baadaye mwandiko huu uliendelezwa kuwa mwandiko wa Wafinisia uliokuwa asili ya alfabeti ya Wagiriki iliyo mama ya alfabeti yetu ya Kilatini. Katika alfabeti ya Kilatini herufi ya "A" yaonekana hadi leo ya kwamba asili yake ilikuwa picha cha kichwa cha ng'ombe iliyogeuzwa.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwandiko wa kikabari kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy