Nenda kwa yaliyomo

Nikeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Nikeli
Jina la Elementi Nikeli
Alama Ni
Namba atomia 1
Uzani atomia 58,6934 u
Valensi 1
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 1728 K (1455 °C)
Kiwango cha kuchemka 3186 K (2913 °C)
Asilimia za ganda la dunia 0,01

Nikeli ni dutu sahili ya metali na elementi. Namba atomia yake ni 28 katika mfumo radidia, uzani atomia ni 58.6934. Katika mazingira ya kawaida ni metali ngumu yenye rangi nyeupe. Alama yake ni Ni.

Nikeli huyeyuka kwa 1728 K (1455 °C) na kuchemka kwa 3186 K (2913 °C).

Inaonyesha uchumasumaku kama chuma. Haijibutiki rahisi na oksijeni, hivyo inatumiwa sana pamoja na chuma au metali kwa mchanganyiko au kama ganda la nje kwa kusidi la kuzuia kutu.

Ina hatari kwa afya ya binadamu. Watu wasio wachache hupata mziro wakigusa nikeli mara kwa mara. Kwa sababu hiyo vifaa vya kiganga vilivyokuwa vya nikeli siku hizi vinatengenezwa ama na nikeli kidogo au bila.

Kiasi cha miligramu 50 kinatosha kumdhuru au hata kumwua mtu.

Nikeli iligunduliwa mwaka wa 1751, lakini, muda mrefu kabla ya hapo, wachimbaji wa Saxon walijua vizuri madini hayo, ambayo yalionekana kama shaba na ilitumika katika utengenezaji wa glasi kwa uchoraji glasi kijani.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nikeli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy