Quintana Roo
Mandhari
Quintana Roo ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko upande wa kusini - mashariki ya nchi na mashariki ya rasi ya Yucatán. Ina pwani ndefu na Bahari ya Karibi.
Mji mkuu ni Chetumal na mji mkubwa ni Cancún.
Imepakana na Yucatán, Campeche na nchi ya Belize. Kunako mwaka wa 2005, idadi ya wakazi ilikuwa 1,135,309. Eneo la jimbo ni 20,212 km².
Jina la jimbo lilitolewa kwa heshima ya mzalendo ya nchi Andrés Quintana Roo.
Siku hizi imekuwa nchi tajiri kutokana na utalii.
Gavana na jimbo ni Félix González Canto.
Lugha ni Kihispania na Kimaya.
Miji Mikubwa
[hariri | hariri chanzo]- Cancún (572,973)
- Chetumal (136,825)
- Playa del Carmen (100.383)
- Cozumel (73,193)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kihispania) Estado de Quintana Roo Sitio oficial Archived 10 Julai 2009 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mexiko bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Quintana Roo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |