Nenda kwa yaliyomo

Viola Davis

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Viola Davis
Amezaliwa11 Agosti mwaka wa 1965
UtaifaMmarekani
Mhitimuchuo cha Rhode Island (1988) shule ya Juilliard (1994)
Kazi yakeMwigizaji
Urefu5'5
MwenzaJulius Tennon (2003)
Watoto1
TuzoTony (1996, 2001, 2010)

Viola Davis (alizaliwa 11 Agosti 1965) ni mwigizaji wa Marekani aliyecheza katika filamu nyingi. Alianza katika Broadway na sasa anafanya kazi katika Hollywood kama mwigizaji maarufu sana. [1]

Malezi yake

[hariri | hariri chanzo]

Viola Davis alizaliwa katika jimbo la Carolina Kusini, mji wa Saint Matthews. Baba yake (Dan Davis) alikuwa mpandafarasi stadi, wakati mama yake (Mary Alice Davis) alipokuwa mke wa nyumbani na alifanya kazi katika kiwanda.[2] Viola aliolewa mume wake (Julius Tennon) katika mwaka wa 2003 na yeye ana mtoto (Genesis Tennon) moja na Viola ni muumini wa Ukristo.[3][4] Wakati yeye alipokuwa mtoto, yeye aliishi katika jimbo la Rhode Island, mji wa Central Falls. Yeye na familia yake waliishi katika umaskini wakati walipoishi katika mji wa Central Falls. Kwa mfano, Viola aliishi na panya na yeye hakuwa na chakula cha kutosha.[2] Kutoroka matatizo yake nyumbani, yeye alitazama filamu nyingi na yeye aliamua kuigiza wakati yeye alipokuwa katika shule ya sekondari na baada ya yeye alihitimu kutoka shule ya sekondari, yeye aliendelea kufuatilia ndoto yake wakati yeye alipojiandikisha chuo cha Rhode Island, ambapo yeye alisoma drama.[5][2] Yeye alihitimu kutoka chuo cha Rhode Island katika mwaka wa 1988 na halafu yeye alipojiandikisha shule nyingine ya maonyesho katika jimbo la Rhode Island na baadaye yeye alipojiandikisha shule ya Juilliard katika mji wa New York ambayo alihitimu kutoka katika mwaka wa 1994.[2]

Kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Viola alianza kufanya kazi katika Broadway katika mwaka wa 1988 lakini kazi yake maarufu zaidi ilikuwa ni "Seven Guitars" (1996) wakati yeye alipoigiza kama Vera.[2][5]Yeye alipokea tuzo (tuzo ya Tony) kwa kuigiza kama Vera na baada ya yeye alipokea tuzo hiyo kazi yake ilianza kusonga mbele haraka. Kwa mfano, katika mwaka wa 1999 yeye alifanya kazi na Phylicia Rashad katika "Everybody's Ruby".[2] Ingawa Viola aliigiza filamu nyingi, filamu iliyomfanya kuwa maarufu katika Hollywood na mahali pengine ilikuwa "Doubt" na Meryl Streep na filamu ilitoka mwaka wa 2008.[5] Filamu hiyo ilikuwa kuhusu ubaguzi wa kimbari katika shule ya katoliki.[6] Halafu, Hollywood iliamua kwamba yeye acheze katika filamu ambazo zinaonyesha mapambano ya watu wa Afrika na utamaduni wa Afrika. Kwa mfano, katika mwaka wa 2011 na mwaka wa 2022, yeye aliigiza katika filamu "The Help" (2011) na "The Woman King" (2022). "The Help" ilikuwa kuhusu wanawake waliofanya kazi kwa wanawake weupe katika jimbo la Mississippi wakati enzi ya haki za raia. "The Woman King" ilikuwa kuhusu ufalme wa wanawake wa Afrika magharibi katika karne ya 17 ambao unajilinda dhidi ya wavamizi wa nje.[6] Viola aliigiza filamu nyingi ambazo zinahusiana historia ya watu wa Afrika, kwa hivyo yeye ni mwigizaji ambaye anawakilisha urithi wa Afrika.[6][2]

  1. "Who is Viola Davis? Everything You Need to Know". www.thefamouspeople.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-04-29.
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 "Viola Davis | Biography, Movies, Plays, The Help, EGOT, & Facts | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-29.
  3. "Who is Viola Davis? Everything You Need to Know". www.thefamouspeople.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-04-29.
  4. Closer Staff (2021-01-22). "5 Things You Don't Know About Viola Davis: Faith, Family and More". Closer Weekly (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-04-29.
  5. 5.0 5.1 5.2 "Viola Davis - Awards, Movies & Family". Biography (kwa American English). 2021-05-14. Iliwekwa mnamo 2023-04-29.
  6. 6.0 6.1 6.2 "Viola Davis". IMDb (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-04-29.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy