Nenda kwa yaliyomo

Wavikingi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Upanuzi wa Waskandinavia wakati wa karne za 8 - 11

Wavikingi ni jina la kujumlisha makundi ya watu wa makabila ya Kigermanik katika Ulaya ya Kaskazini walioonekana kwa majirani kama wafanyabiashara na pia maharamia wa baharini.

Asili yao ilikuwa katika Skandinavia ya Kaskazini na kusini, wakatumia jahazi ndogo wakivuka nazo Bahari ya Kaskazini, Bahari ya Baltiki na kuingia pia barani kupitia mito ya Ulaya hadi Mediteranea.

Mara nyingi walishambulia tu miji na vijiji vya pwani wakipora mali na kurudi kwao.

Kulikuwa pia na vipindi ambako Wavikingi walifaulu kuteka eneo fulani na kukaa huko. Walifika Uingereza, Uskoti, Ufaransa, Hispania, Urusi hadi Bizanti na Sisilia.

Katika Uingereza, Ufaransa ya Kaskazini na Italia ya Kusini walianzisha makazi wakitawala maeneo huko kwa muda. Huko walijulikana pia kwa majina kama Wanormani au Rus, na Rus ndiyo asili ya jina la Urusi.

Walivuka pia Atlantiki na kufika Greenland na Kanada.

Walihofiwa mara nyingi kama majambazi wakali lakini walitafutwa pia kama wanajeshi wa kukodi.

Inaaminiwa ya kwamba waliondoka kwao kwa sababu hali ya hewa ilileta njaa na uhaba wa ardhi ya kulima na pia kwa sababu utajiri wa nchi za kusini iliwavuta vijana wao.

Jahazi ya Wavikingi

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wavikingi kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy