Kisw PP3

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 7

JINA……………………………………………………………...

NAMBARI YA
MTAHINIWA……………….
SAHIHI…………………………………………….
TAREHE…………………………………….
102/3

Kiswahi FASIHI
JULAI 2023
MUDA: Saa 2 ½

PANGANI GIRLS MORK 2023

MAAGIZO
a) Jibu maswali manne pekee.
b) Swali la kwanza ni la lazima.
c) Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe
kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani: tamthilia,
Hadithi Fupi, Riwaya na Ushairi.
d) Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
e) Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya
Kiswahili.
f) Karatasi hii ina kurasa 6 zilizopigwa
chapa.
g) Watahini lazima wahakikishe kwamba
kurasa zote za karatasi hii zimepigwa
chapa sawa sawa na kuwa maswali yote
yamo.
KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE:
SWALI UPEO ALAMA
1 20
20
20
20
JUMLA 80

SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI


1. Lazima
Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.
Zimepita siku ayami
Siku chungu tangu giza lipotanda
Wakati lipotazama kwa kiwewe na shauku
Pumzisho kipania, roho kupigania
Ziraili alipokakamaa aushiyo kufakamia.

Nilikwita kwa sauti


Ela mpenzi hukunitika
Machoyo litunga mbele
Kumkabili huyu nduli
Nikabaki kunyongonya
Jaala kitumainia,
Mtima kijiinamia
Hatima kungojea.

Ya mwisho lipopumua,
Alfajiri ya kiza kuu
Nalidhani wanichezea,
Mizaha yako kawaida
Lijaribu kupulizia
Hewa toka langu pafu,
Tumaini kiniambia pumzi zangu takuhuisha
Sikujua hizo likuwa juhudi za mfa maji muhebi.
Macho libaki kutunduiya, tabasamuyo kitaraji
Kumbe mwenzangu kaniacha!
Ukiwa ulinivaa, ukungu ukatwandama
Pa kuegemea sikujua fundo chungu linisakama
Tabibu alipoingia na kutangaza rasmi mauko.

Ilikuwa kana kwamba ndo jana lipofunga nikahi,


Kumbukizi zilinijia kwa chozi teletele
Japo kifo ni faradhi ndwele hino halieleweki
Ama jicho la hasidi,
Limekuangaza jamani?
Koja hili ninalokuwekea,
Kando ya kasri hili la shakawa
Ni hakikisho toka kwangu, nitatamba sana njia
Kutafuta alotwendea kinyume kutupoka,
Mauko kutuleteya.
a) (i) Ainisha utungo huu kwa kuzingatia kipengele cha maudhui.
(alama 1)
(ii) Andika sababu tatu kuthibitisha jibu lako la a(i).
(alama 3)
b) Bainisha sifa mbili za jamii inayosawiriwa katika utungo huu.
(alama 2)
c) Fafanua vipengele vinne vya kimtindo ambavyo vimetumiwa kufanikisha
uwasilishaji wa utungo huu.
(alama 4)
d) Tungo za aina hii zinaendelea kufifia katika jamii yako. Fafanua hoja tano
utakazotumia kuishawishi jamii yako kukinga dhidi ya hali hii.
(alama 5)
e) Unanuia kutumia mbinu ya kushiriki kufanya utafiti kuhusu tungo za aina hii.
Eleza sababu tano za kuchagua mbinu hii.
(alama 5)

SEHEMU B. Swali 2 na 3
CHOZI LA HERI (ASSUMPTA K. MATEI)
2. “Huyu ambaye mama alimwona kuwa gae, kumbe sasa ndiye chombo cha
kunivusha bahari hii ya dhiki?” alijisemea.
a) Fafanua muktadha wa maneno haya (alama 4)
b) Tambua mbinu tatu za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili
(alama 3)
c) Kwa hoja tatu onyesha nafasi ya mrejelewa katika kujenga hadithi hii

(alama 3)
d) Kwa kutolea hoja kwingineko riwayani, dhihirisha jinsi wahusika
mbalimbali wanakuwa ‘chombo cha kuvusha wengine bahari ya
dhiki’ (alama 10)

3. Fafanua kwa hoja kumi jinsi riwaya ya Chozi la Heri ilivyolenga kuadilisha
jamii (alama 20)

SEHEMU YA C: SWALI 4 NA 5
BEMBEA YA MAISHA (TIMOTHY M. AREGE)
4. Asubuhi niko skuli majira ya alfajiri, kiboko mkononi. Anayekuja baada yangu
hata kama hajachelewa hana lake.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
(alama 4)
b) Tambua mbinu mbili za mtindo katika dondoo hili
(alama 4)
c) Bainisha toni inayojitokeza katika dondoo hili
(alama 2)
d) Fafanua sifa mbili za msemaji kutoka kwenye dondoo
(alama 2)
e) Onyesha jinsi elimu ilivyosawiriwa katika Tamthilia Bembea ya Maisha
(alama 8)

5. Kumbuka mrina haogopi nyuki. {kimya}


Marehemu mama yangu alizoea kutuambia kuwa nguvu hazimwishi
mwanadamu wala hazipotei bure; humalizwa tu na mabuu. Mwanangu,
usifanye hofu. Nikujuavyo mimi, hukuingia katika bahari si yako. Wala hakuna
refu lisilokuwa na ncha. Yote yana mwisho eti! Ipo siku yote yatapita.
{kimya} Mkulima hodari libasi yake huwa imechakaa na kuchoka lakini
moyoni anabaki safi kama theluji kwa kutosheka na tija ya sulubu zake.
Huwezi kumlinganisha na mkulima wa nguo safi zilizopigwa pasi zikanyooka.
a) Changanua mtindo katika kifungu hiki (alama 6)
b) “Mila na desturi zetu zimewajenga hivyo walivyo na sisi hivi tulivyo”.
Imani na itikadi huthaminiwa sana na jamii zetu. Jadili ukweli wa kauli hii
kwa kurejelea tamthilia ya bembea ya Maisha
(alama 10
c) Onyesha jinsi msemewa hakuingia katika bahari si yake
(alama 4)

SEHEMU YA D: SWALI 6 NA 7
SHAIRI
6. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo:
1. Mkata ni mkatika,harithi hatoridhiwa
Sina ninalolishika,wala ninalochukuwa
Mlimwengu kanipoka,hata tone la muruwa!
Mrithi nini wanangu?

2. Sina ngo’mbe sina mbuzi, sina konde sina buwa


Sina hata makaazi, mupasayo kuyajuwa
Sina mazuri makuzi, jinsi nilivyoachwa
Mrithi nini wanangu?

3. Sina kazi sina bazi, ila wingi wa shakawa


Sina chembe ya majazi, mno nikukamuliwa
Nakwa’cheni upagazi, ngumu kwenu ku’tuwa
Mrithi nini wanangu?

4. Sina sikuachi jina, mkata hatasifiwa


Hata nifanye la mana, mno mi kulaumiwa
Poleni wangu sana, sana kwenu chakutowa
Mrithi nini wanangu?

5. Sina leo sina jana, sina kesho kutwaliwa


Sina zizi sina shina, wala tawi kuchipuwa
Sina wanangu mi sina, sana la kuacha kuraduwa
Mrithi nini wanangu?
6. Sina utusi na haki,mila yangu meuliwa
Nyuma yangu ili dhiki,na mbele imekaliwa
N’nawana na miliki, hadi nitakapofukiwa
Mrithi nini wanangu?

7. Sina ila kesho kwenu, wenyewe kuiongowa


Muwane kwa nyinyi mbinu, mwende pasi kupumuwa
Leo siyo kesho yenu, kama mutajikamuwa
Mrithi nini wananngu?

(a)Taja mambo yoyote mawili ambayo mtunzi


angewarithisha wanawe. (alama2)
(b)Taja sifa nne za kiarudhi alizotimia
mshairi (alama 4)
(c)Andika ubeti wanne
kwa lugha nathari.(alama4)
(d)Dondoa mifano miwili miwili ya: (alama2)
i) Inkisari
ii) Tabdila
(e)Chambua shairi hili kwa upande wa:
(i)Dhamira (alama2)
(ii)Muundo (alama4)
(f)onyesha bahari za shairi hili kwa kuzingatia
vigezo vifuatavyo: i) migao
ii) vina
iii) mizani

Swali 7.
Kiia nikaapo hushika tama
Na kuwazia hali inayonizunguka.
Huyawazia madhila
Huziwazia shida
Huiwazia dhiki

Dhiki ya ulezi
Shida ya kudhalilishwa kazini.
Madhila ya kufanyiwa dharau
Kwa sababu ya jinsia ya kike.

Hukaa na kujidadisi
Hujidadisi kujua kwa nini
Jamii haikisikii kilio changu
Wenzangu hawanishiki mikono
Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni

Hukaa na kujiuliza
I wapi raha yangu uiimwengu huu?
I wapi jamaa nzima ya wanawake?

MASWALI
(a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza
(alama2)
(b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
(alama 2)
(c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata.
(alama 2)
(d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili.
(alama 4)
(e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili.
(alama 2)
(f) Fafanua toni ya shairi hili.
(alama 2)
(g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili.
(alama 2)
(h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa.
(alama 2)
(i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
(alama 2)
(i) Madhila
(ii) Kudhalilishwa.

SEHEMU YA E SWALI 8: HADITHI FUPI


Kifo cha suluhu (Dominic Maina Oigo)
8. Mume wangu, ninapoandika waraka huu, naomba uelewe kuwa wanao wawili
wanazidi kuumia. Labda unadhani unayoyafanya ni siri ila usilolijua ni
kwamba kila ufanyalo nalifahamu.
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Tambua umuhimu wa mandhari katika dondoo hili katika kujenga maudhui
(alama 4)
c) Bainisha hulka nne za mzungumzaji (alama 4)
d) Onyesha toni inayojitokeza katika dondoo hili (alama 2)
e) Dhihirisha kuwa kila alilolifanya mumewa lilijulikana (alama 6)

You might also like

pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy