Ahadi yetu kuhusu usalama
Tungependa usafiri bila wasiwasi, utumie wakati vizuri na ukutanishwe na watu na maeneo muhimu kwako. Ndiyo maana tumejitolea kulinda usalama, kuanzia kuunda viwango vipya hadi kubuni teknolojia kwa lengo la kupunguza ajali.
Jinsi usalama unavyodumishwa kwenye usafiri wako
Vipengele vya usalama kwenye app
Kuwaonesha ndugu na marafiki maelezo ya safari Kufuatilia safari yako barabarani. Teknolojia yetu inasaidia kuondoa wasiwasi kwa urahisi.
Jumuiya inayojali maslahi ya kila mtu
Mamilioni ya wasafiri na madereva wanafuata Mwongozo wa Jumuiya na hivyo wanawajibika kufanya mambo yanayofaa.
Usaidizi popote ulipo
Timu yetu ya wataalamu inapatikana kila wakati. Wasiliana nayo kupitia programu, usiku au mchana, ukiwa na maswali yoyote au matatizo ya kiusalama.
Kuhakikisha safari salama kwa ajili ya kila mtu
Usalama wa dereva
Kuna usaidizi wa saa 24 siku 7 za wiki na msaada wakati wa matukio ya dharura. Onyesha safari yako kwa watu wako wa karibu. Tumeweka kipau mbele kwenye usalama wako, ili ujishughulishe na shughuli zinazokuingizia pesa.
Usalama wa msafiri
Mamilioni ya watu huomba safari kila siku. Kila msafiri anaweza kufikia vipengele vya usalama vilivyo kwenye programu. Na kila safari ina timu ya usaidizi kwa wateja inayopatikana wakati wowote.
Mustakabali wa usalama
Zaidi ya wafanyakazi 200 wa Uber, wakiwemo watafiti na wanasayansi, wasanifu na wahandisi, wanajitahidi kubuni teknolojia inayojumuisha usalama katika huduma zetu. Gundua wanachofanya.
“Kila siku, teknolojia yetu husaidia mamilioni ya watu kupata usafiri katika miji ulimwenguni kote. Jukumu la kuhakikisha usalama wa watu ni muhimu sana na tunalichukulia kwa makini zaidi.”
Dara Khosrowshahi, Afisa Mkuu Mtendaji wa Uber
Tunashirikiana ili kuleta mabadiliko.
Ahadi yetu ya usalama inadumu hata baada ya safari yako. Tumeungana na kikundi cha wataalamu wakuu - ikiwemo maafisa wa usalama wa umma na mashirika ya kupambana na vurugu - ili kusaidia kuimarisha usalama kwenye barabara na miji kwa ajili ya kila mtu.
*Baadhi ya masharti na vipengee hutofautiana kulingana na eneo na huenda havipatikani.
Kuhusu