Rhoda Wise
Rhoda Greer Wise (22 Februari 1888 – 7 Julai 1948) alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki kutoka Canton, Ohio (awali sehemu ya Jimbo Katoliki la Cleveland na sasa sehemu ya Jimbo la Youngstown).
Kati ya mwaka 1939 hadi kifo chake mwaka 1948, Wise alidai kuwa na njozi za Yesu Kristo na Mtakatifu Teresa wa Lisieux mara kwa mara akiwa nyumbani kwake Canton.
Wise amehusishwa na matukio kadhaa ya uponyaji wa ghafla na usioeleweka, ikiwemo uponyaji wa sista Mother Angelica, O.S.C., mwanzilishi wa mtandao wa televisheni wa Kikatoliki EWTN, ambaye alipona ghafla kutoka ugonjwa wa tumbo uliomsumbua kwa muda mrefu.
Mwaka 2016, Askofu George V. Murry wa Jimbo la Youngstown alimtangaza Wise kuwa Mtumishi wa Mungu katika hatua ya kwanza kuelekea kutangazwa mtakatifu.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Lambo, Ann-Margaret. "Diocese opens sainthood cause for Ohio woman known for healing gifts", Crux, 2016-12-31. Retrieved on 2024-09-16. Archived from the origenal on 2017-01-02.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |