Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres alaani mauaji ya watumishi wa WFP nchini Sudan

Malori yaliyobeba chakula muhimu yanavuka mpaka kutoka Chad hadi Sudan kupitia Adre.
© WFP/Sylvain Barral
Malori yaliyobeba chakula muhimu yanavuka mpaka kutoka Chad hadi Sudan kupitia Adre.

Guterres alaani mauaji ya watumishi wa WFP nchini Sudan

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amechukizwa na taarifa za mauaji ya wafanyakazi watatu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP nchini Sudan.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amemnukuu Guterres akisema mauaji hayo yalifanyika jana Desemba 19 kwenye ofisi ya mashinani ya WFP huko Yarbus, jimboni Blue Nile kupigwa na kombora kutoka angani.

“Anatuma salamu za rambirambi kwa familia za waliouawa na wafanyakazi wenzao WFP,” amesema Guterres kupitia taarifa hiyo iliyotolewa New York, Marekani leo na msemaji wake Stéphane Dujarric.

Amelaani mashambulizi yote dhidi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wale wanaotoa misaada ya kibinadamu, akitoa wito wa uchunguzi wa kina wa tukio hilo.

Wahudumu waendelea kufanya kazi licha ya vita

Guterres amesema tukio la jana linaonesha gharama za mzozo katili wa Sudan kwa mamilioni ya watu wenye uhitaji na kwa wafanyakazi wa kusambaza misaada ya kibinadamu wanaohaha kufikisha misaada muhimu.

Taarifa hiyo inasema mwaka huu wa 2024 ulivunja rekodi ya vifo vya watumishi wa misaada ya kibinadamu Sudan.

Licha ya vitisho hivyo, wameendelea kufanya wawezale kupeleka misaada ya kibinadam kule inakohitajika,” amesema Guterres.

Ni kwa mantiki hiyo, Katibu Mkuu anatoa wito kwa pande kinzani Sudan kuzingatia wajibu wao wa kulinda raia, wakiwemo watumishi wa kibinadamu.

“Mashambulizi hayapaswi kuelekezwa kwa raia na watendaji hao na tahadhari zote lazika zizingatiwe ili kuepusha kuwadhuru.”

Baada ya zaidi ya miezi 20 ya mzozo Sudan, Katibu Mkuu kwa mara nyingine tena anasisitiza umuhimu wa sitisho la mapigano. “Umoja wa Mataifa utaendelea na juhudi za usuluhishi na kufanya kazi na wadau wote kumaliza vita Sudan.”

Vita hivyo vilianza Aprili 2023 kati ya kiongozi wa serikali ya muda Abdel Fattah Al-Burhan na kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF) linaloongozwa na Naibu wa zamani wa Al-Burhan, Mohamed Hamdan Dagalo.

pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy