Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Afya

Mwanamke akifanyiwa kipimo cha COVID-19-Kutoka maktaba
© WHO

Ugonjwa wa HMPV: Kupata taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu wa afya ni muhimu kama ilivyo kujiandaa

Huku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa kupumua vikiwemo virusi vya metapneumovirus (HMPV) wakati huu wa msimu wa baridi nchini China na kuleta hofu ulimwenguni kuhusu uwezekano wa kutokea kwa janga jingine la ugonjwa kama ilivyokuwa Covid-19, mamlaka ya afya nchini humo inasema kiwango na nguvu za ugonjwa huo viko chini ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana, ameeleza Hans Kluge, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni kanda ya Ulaya akisisitiza ulimwengu kupata taarifa sahihi. Anold Kayanda na taarifa zaidi.

Sauti
2'9"
Watu wanaendelea kufungasha virago Haiti kutokana na magenge ya uhaliffu
© UNICEF/Ralph Tedy Erol

Mashambulizi dhidi ya sekta ya afya Haiti yanatia hofu kubwa: OHCHR

Mtaalam wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu kuhusu Haiti William O’Neill, leo amesema anatiwa wasiwasi mkubwa kwamba mashambulizi ya kikatili dhidi ya hospitali, zahanati, na wahudumu wa afya yaliyofanywa na magenge ya uhalifu nchini Haiti mwezi wa Desemba yamedhoofisha zaidi mfumo wa huduma za afya ambao tayari ulikuwa karibu kuporomoka.

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kaskazini mwa Gaza ulisaidia kuhamisha baadhi ya wagonjwa kutoka Hospitali ya Kamal Adwan hadi Hospitali ya Al-Shifa.
© WHO

Mashambulizi ya Israel yausukuma mfumo wa afya Gaza ukingoni kuporomoka: OHCHR

Ripoti iliyochapishwa leo na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imeweka wazi kuwa mtindo wa Israel wa mashambulizi mabaya karibu na dhidi ya hospitali katika Ukanda wa Gaza, yamesukuma mfumo wa afya kwenye ukingo wa kuelekea kuporomoka kabisa, hali ambayo imekuja na athari mbaya kwa Wapalestina kukosa uwezo wa kupata huduma za afya na matibabu.

Wafanyakazi wa WHO Rwanda wanatoa mafunzo kwa wahudumu wa afya katika mojawapo ya hospitali kubwa mjini Kigali.
© WHO

Maburg: Rwanda yatangaza mwisho wa mlipuko, WHO yapongeza

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeipongeza serikali ya Rwanda kwa kufanikiwa kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg. Hii leo Rwanda imetangaza mwisho wa mlipuko wa hivi karibuni wa ugonjwa huo baada ya kutokuwepo maambukizi mapya katika siku 42 na mgonjwa wa mwisho akiwa amepimwa mara mbili bila kukutwa na ugonjwa kama matakwa ya WHO yanavyotaka ili kutangaza kuisha kwa mlipuko wa magonjwa namna hii.

Sauti
2'3"
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy