Hongera kwa miaka 100 ya siku ya kuzaliwa Brian Urquhart- Umetendea mema UN
Ikiwa leo ni miaka 100 tangu kuzaliwa Sir. Brian Urquhart, mmoja wa wafanyakazi waanzilishi zaidi wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Antonio Guterres ameumwagia sifa lukuki ikiwemo utumishi uliotukuka na uliosaidia kujenga misingi ya chombo hicho kilichoundw mwaka 1945 baada ya Vita Vikuu vya Pili vya dunia.