Content-Length: 126195 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/Maria_kupalizwa_mbinguni

Maria kupalizwa mbinguni - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Maria kupalizwa mbinguni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Tiziano, katika Basilika la Santa Maria Gloriosa dei Frari, Venezia, Italia. Labda mchoro huo wa mwaka 1516-1518 ni maarufu kuliko yote ya Kanisa la Magharibi kuhusu fumbo hilo.
Kulala kwa Bikira Maria katika ubao wa pembe za ndovu: kazi ya karne ya 10 au mwanzo wa karne ya 11 (Musée de Cluny, Ufaransa).

Maria kupalizwa mbinguni ni sherehe ya Kanisa Katoliki inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 15 Agosti[1]. Kadiri ya sheria za Kanisa, kimataifa ni sikukuu ya amri, ingawa katika nchi nyingine si hivyo, kutokana na serikali kutokubali tarehe hiyo kama siku ya pumziko.

Msingi katika imani

[hariri | hariri chanzo]

Adhimisho hilo la liturujia ni la zamani, lakini limepata nguvu mpya kutokana na dogma iliyotangazwa na Papa Pius XII kwa hati Munificentissimus Deus ya tarehe 1 Novemba 1950 baada ya kusikiliza maoni ya maaskofu wote duniani[2].

Fundisho hilo la imani Katoliki ni kwamba Bikira Maria, mama wa Yesu, alipomaliza maisha yake duniani alichukuliwa mwili na roho mbinguni, ashiriki mapema utukufu wa Mwanae mfufuka, Yesu Kristo kama alivyoshirikiana naye toka mwanzo hadi mwisho wa maisha yake.

Fundisho hilo linalingana na lile la Waorthodoksi, ingawa hao hawajalitangaza kuwa dogma. Tarehe hiyohiyo wao wanaadhimisha ya Kulala kwa Bikira Maria.

Hata baadhi ya Waanglikana na Walutheri wana adhimisho la Bikira Maria siku hiyo.

Umoja wa msimamo huo upande wa mashariki na wa magharibi wa Kanisa unatokana na mapokeo ya karne za kwanza za Ukristo, yanayoshuhudiwa na mababu wa Kanisa kama vile Efrem wa Syria, Timoteo wa Yerusalemu, Epifanio wa Salamina na Yohane wa Damasko.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria kupalizwa mbinguni kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/Maria_kupalizwa_mbinguni

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy