Mapema tu vita ilipoanza, UN ilifanikisha makubaliano ya kuendeleza usafirishaji wa shehena kutoka bandari za Ukraine, ili kupunguza ongeze la bei ambalo liliathiri vibaya nchi maskini. Juhudi awali zilifanikiwa lakini sasa makubaliano yamesambaratika. Mashambulizi ya Urusi yamarejea na bei zinaongezeka.
Makadirio ya mashirika ya kibinadamu ni kwamba zaidi ya watoto 2,000 wameuawa au wamejeruhiwa katika vita inayoendelea. Shirika la UN la kuhudumia watoto, UNICEF linaendelea kutoa msaada wa kuokoa maisha ikiwemo kuwapatia watoto elimu, msaada wa kisaikolojia na kuepukana na mabomu ya kutegwa ardhini.