Maelezo Kwa Watangazaji
Flora Nducha: Mkuu wa Idhaa
Assumpta Massoi: Mtangazaji
Arnold Kayanda: Mtangazaji
Leah Mushi:Mtangazaji
Selina Jerobon :Mtangazaji msaidizi
Thelma Mwadzaya :Ripota Kenya
Byobe Malenga:DRC
George Musubao Paluku : DRC
KUHUSU IDHAA YA KISWAHILI
Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa inaripoti shughuli za UM kutoka makao yake makuu mjini New York, Marekani na kote duniani.
Masuala ya amani na usalama, maendeleo na haki za binadamu ni masuala yanayotuhusu , hivyo habari za utatuzi wa migogoro, uchaguzi, afya, umasikini, elimu na mabadiliko ya hali ya hewa yanachukua nafasi kubwa katika orodha ya mada tunazoripoti.
Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, mbali na kutangaza habari, makala, kuandaa video na kupatikana pia kwenye mitandao ya kijamii kama vile Twitter na bila kusahau chaneli ya Youtube pia inatoa fursa ya bure kwa watu kupata sauti mbalimbali kupitia kwenye tovuti ya makataba yake ambayo ni (UN Audio Library website), sauti hizo ni kutoka kwenye mikutano inayoendelea na matukio ya kila siku , na pia sauti zilizohifadhiwa zamani maktaba. Pia sauti hizo zinapatikana katika ubora wa hali ya juu na mtu anaweza kurekodi moja kwa moja kutoka kwenye tovuti yetu kwa kutumia faili ya MP3 .
Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa – inaripoti kwa wakati na usahihi kuhusu UM.