Vichwa vya Habari
Chaguo la Mhariri
Makala Maalum
Tabianchi na mazingira
Mji wa Amazon wa Belém, Brazili, utakuwa kitovu cha juhudi za kimataifa za kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi mwezi Novemba 2025, wakati utakapoandaa moja ya mikutano muhimu ya Umoja wa Mataifa ya mabadiliko ya tabianchi hivi karibuni.
Habari kwa Picha
UKRAINE: Siku 1,000 za vita; msaada wa UN bado ni thabiti
Operesheni za Urusi dhidi ya Ukraine zikiingia siku ya 1,000, Umoja wa Mataifa umeendelea kutoa msaada muhimu unaohitajika, kwenye nyanja ya msaada wa kiutu, afya, huduma za kujisafi na usafi, na kuhakikisha usalama na ulinzi wa taifa hilo lenye mtambo mkubwa zaidi wa nyuklia barani Ulaya.
Habari Nyinginezo
Wanawake
Umoja Wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) walitufundisha ushoni na walitupatia cherehani ili tuweze kushona nguo tujitegemee na kusaidia familia yetu sisi wanawake wakimbizi wa ndani na pia manusura wa ukatili wa kijinsia katika kambi iliyoko Goma, amesema Naomi Kianga, ambaye jina lake limebadilishwa kwa usalama na heshima yake.
Haki za binadamu
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo Januari 7 mjini Geneva, Uswisi amesema amesikitishwa sana na ongezeko kubwa la watu walionyongwa nchini Iran mwaka jana. Takriban watu 901 waliripotiwa kunyongwa mwaka 2024, arobaini kati yao wakiwa walinyongwa katika wiki moja pekee mwezi Desemba. Takribani watu 853 walinyongwa mwaka 2023.